CCM inaugua kansa ya uongozi - Mwalimu Julius Nyerere

Fareed

JF-Expert Member
Apr 13, 2010
328
135
Salaam,

Naomba kuwasilisha makala hii nzuri inayosambazwa kwenye email ili wana JF wenzangu muisome na kutafakari maneno ya busara sana ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Ingawa alikuwa mwanzilishi wa CCM, kwa nia njema ya kuendeleza mapinduzi katika nchi yetu, miaka ilivyozidi kwenda Mwalimu Nyerere alishuhudia jinsi CCM ilivyobadilika na kuwa mzigo kwake na pia tishio kwa usalama wa Taifa.

Mwaka 1993 Mwalimu alichapisha kitabu kiitwacho Uongozi Wetu na Hatima ya Tanzania (Harare: Zimbabwe Publishing House, 1993). Pamoja na mambo mengine katika kitabu hiki, Mwalimu alisema kuwa kuna kansa katika uongozi wa CCM. Nanukuu baadhi ya maneno yake:

Chama cha Mapinduzi, kwa sababu ya uzito wa historia yake, hadhi ya jina lake, mfumo wa wavu wake, mazoea ya watu, na ubovu wa Vyama vya Upinzani, kinaweza kuchaguliwa na Watanzania, pamoja na kansa ya uongozi wake. Au watu wanaweza wakachoka, wakasema, "potelea mbali:" wakachagua Chama cho chote, ilimradi tu watokane na kansa ya uongozi wa CCM. Hainifurahishi kuyasema haya, lakini uhai wa Nchi yetu unataka yasemwe. (Ukurasa 61)
Mwalimu hakuishia hapo, bali aliongezea namna hii:

Nilisema awali kwamba kansa ya uongozi ndani ya Chama cha Mapinduzi isingekuwa ni jambo la kutisha sana kama tungekuwa tumeanza kuona Chama kizuri cha upinzani kinachoweza kuiongoza Nchi yetu badala ya CCM. Ubovu wa uongozi ndani ya CCM ndio uliofanya nikapendekeza tuanzishe mfumo wa Vyama Vingi. Nilitumaini kuwa tunaweza kupata Chama kingine kizuri ambacho kingeweza kuiongoza Nchi yetu badala ya CCM; au ambacho kingekilazimisha Chama cha Mapinduzi kusafisha uongozi wake, kwa kuhofia kuwa bila kufanya hivyo kitashindwa katika uchaguzi ujao. Lakini bado sijakiona Chama makini cha upinzani; na wala dalili zo zote za kuondoa kansa ya uongozi ndani ya CCM. Bila upinzani mzuri wa nje, na bila demokrasia halisi ndani ya Chama cha Mapinduzi, Chama hiki kitazidi kudidimia chini ya uzito wa uongozi mbovu. Kwa hali yetu ya kisiasa ilivyo nchini hili si jambo la kutarajia bila hofu na wasi wasi! (Ukurasa 66)

Ni wa-Tanzania wangapi wenye utamaduni wa kusoma vitabu? Ni wangapi wanaosoma vitabu vya Mwalimu Nyerere?

Isambaze kwa Wanamapinduzi na Wanaoipenda CCM wapate kuyajua haya

MY TAKE:


  • It is ironic that 6 years after this book was published, Nyerere died of leukaemia, a type of cancer of the blood.

  • Under Jakaya Kikwete's reign, the leadership cancer within the ruling CCM party that Mwalimu talked about has reached Stage IV, which is the most deadly form of the condition.

  • Being the humble/honest man he was, If Nyerere was alive today, he would have publicly declared that CHADEMA is the party to oust CCM from power. CCM has become too bureaucratic and too corrupt. With the exception of a few bad apples (less than 3) in CHADEMA's top leadership hierarchy with questionable ethical standards, CHADEMA has the best pool of leaders in any political party in Tanzania. In my opinion, Nyerere would have given his seal of approval for Dr. Willibrod Slaa to become Tanzania's president.

  • The book was published in 1993, the same year that CHADEMA got it's permanent registration, so Nyerere did not have ample opportunity to assess the party as a credible alternative to CCM. Indeed, if I'm not mistaken, Dr. Wilibrod Slaa himself was a CCM member in 1993.

  • Nyerere was quoted saying later after his book was published that CHADEMA has "very good" policies. And he famously noted that the real opposition in Tanzania would emerge from within CCM itself. Dr. Slaa was initially a CCM member before joining CHADEMA, so Nyerere was absolutely right on this one.

  • If we appoint an independent electoral commission, amend the unconstitutional law that prohibits any legal challenge on the results of presidential elections, register to vote, turn out to vote in 2015, and stay vigilant against vote rigging, we shall banish this deadly leadership cancer that is eating away at our beautiful country and replace it with new people-centred leadership.

  • For, it was Mwalimu who once said: "It can be done, play your part."
 
RIP mwalimu, wenzio huku cancer ndio imepamba moto, usithubutu kufufuka ukaona, viongozi wa ccm wako hoi hatujui mionzi gani itasaidia, labda itapatikana 2015 let us pray!!!!!
 
That was then Now CCM is a DEAD MAN WALKING.... tatizo ni kwamba that dead man is so infectious yaani inaacha madhara si polepole
 
Back
Top Bottom