CCM Inaongozwa Kijeshi?

Hume

JF-Expert Member
Sep 25, 2007
340
108
Baada ya Ukuu wa mkoa kuwa mahsusi zaidi kwa wanajeshi,
CCm wameamua kuhamishia ujuzi huo ndani ya chama?

Sehemu kubwa ya uongozi wa juu umeshikiliwa na wanajeshi. Kulikoni?
Au ndo maana na wabunge wao wanawapelekesha kijeshi, Hoja ikija hivi wote tuwe hivi, kama ilivyo kulia geuka kwa wanajeshi ambao wote lazima kutii bila kuuliza kwa nini kulia na si kushoto!
 
Sijui wana ajenda gani,ndio maana wamekesha kuhubiri amani na utulivu.Labda wamegundua kwamba wanaweza kuondolewa kwa nguvu,waache tu kujishtukia wajenge hoja na watekeleze zile sera zao zikiwemo zile walizodandia.

Na waanze sasa na mahakama ya kadhi
 
wajanja wanang'amua. Nchi kwa sasa inadhibitiwa na CCM na jeshi, kwa hiyo, Profesa Baregu anajua vizuri sana kuna siku alichanganua vizuri kuhusu hiyo issue. Na siyo bahati mbaya, jeshi kupenda CCM iendelee na madaraka ni sawa na lenyewe kuendelea kuwepo madarakani.
 
Baada ya Ukuu wa mkoa kuwa mahsusi zaidi kwa wanajeshi,
CCm wameamua kuhamishia ujuzi huo ndani ya chama?

Sehemu kubwa ya uongozi wa juu umeshikiliwa na wanajeshi. Kulikoni?
Au ndo maana na wabunge wao wanawapelekesha kijeshi, Hoja ikija hivi wote tuwe hivi, kama ilivyo kulia geuka kwa wanajeshi ambao wote lazima kutii bila kuuliza kwa nini kulia na si kushoto!

Hiyo ni kweli Hume, Kuna kundi kubwa la maafisa wa jeshi linaingia kwenye age ya kustaafu so tegemea kuwaona wanajeshi kibao sana huko ccm na kwenye serikali.

Inaonekana jamaa wanataka kufanya kama Pakistan ambako wanajeshi hawastaafu kazi!
 
kama hao wanajeshi wanastahili kwa nini wasiingie ccm ?
itafika wakati hata wauza karanga nao wataanza kuingia ccm, sasa siju hapo mtasema nini !

kama ccm inataka kutumia wanajeshi, haina haja ya kuwapa vyeo(wasipostahili) bali pia wanaweza kuwatumia directly bila ya kuwapa vyeo !

hapa suala ni VIGEZO na si vinginevyo !

(Duh, masela eeh, siku hizi inakuwaje maana naona sina hamu kabisa kuingia JF, ) am wandaring !
 
Je Umeona Gazeti La Leo La Mwanahalisi ?

Viongozi Wa Juu Wote Wanagwanda

hebu tuelezee aisee wamaanisha nini kusema viongozi wa juu wote wana gwanda?as wengine tuko nje hilo gazeti ni ndoto kwetu unless utume website yao..
 
about ccm kuwa na viongozi wengi wajuu wa kijeshi...mhm something fishy yaendelea nchini kwetu...hala hala tuu yasije tokea ya pakistan
 
Uongozi wa juu CCM umekuwa ukihaha kubatiza vyama vingine sifa za kutunga kuligawa taifa: Ukabila, Udini n.k! Je, kwa safu ya uongozi wao hapo juu..nasi tuamini CCM ni chama cha Kijeshi?

Mwenyekiti: Luteni Kanali Jakaya Kikwete
Katibu Mkuu: Luteni Yusuph Makamba
Naibu Katibu Mkuu: Kapteni George Mkuchika
Katibu Itikadi/Uenezi: Kapteni John Chiligati
Meneja Kampeni: Kanali Abdulhamani Kinana!!
 
Sio cha kijeshi ni chama cha kivita na wapo tayari kwa lolote ,zana zote wanazo ,uwezo sababu ya kuzitumia wanazo.
 
Jeshi letu la Wananchi ni kikundi cha watu wenye nidhamu wa halii ya juu sana kwa miaka mimi sasa. Jamani mwizi ni mwizi tu na wala tusilihushishe taasisi zima la JWTZ humu.

Naju taifa linapobakwa kiasi hiki wananchi kwa hasira zetu hatukawii kuwavuta shati waliokwemo na hata wale wasiojua kitu kabisa. Cha msingi, tumalize kabisa kuking'oa hiki chama cha mafisadi kikae benchi kisha tuanze upya kama taifa.
 
Ni dhahiri kwani viongozi wa juu wote ni jeshi la wananchi, na jeshini hakuna mashauriano ila kutoa amri na wengine kutekeleza. Usipotekeleza basi watakukabidhi kwa military police wakushughulikie.
Siasa kitu kingine, si jeshi, kwani siasa ni nguvu ya umma. Na umma una muda wa kuvumilia na mambo yakizidi ni moto mkali hawashikiki tena.
Tunataka serikali ya kiraia si serikali ya ccm ya kijeshi iliyojivika ngozi ya kondoo wakati ndani ni mbwa mwitu wakali.
 
enyi wana JF hicho sio chama cha kijeshi bali ni walafi tu wanaojaribu kujilimbikizia kila chakula kitamu kilichoandaliwa kwaajili ya watu, wao wanajipakulia wakati wapishi ni sisi tunapaswa kuwapakulia kwa share zinazostahili but they don't care bout us.
 
Nadhani ni chama cha kigaidi. Wanatumia mbinu zao za kijeshi kwa maslahi ya kikundi fulani wanachakokijua wao.
 
Piga sana vita ufisadi uliomo ndani ya nafsi zao, uanajeshi wao sina uhakika kama ulitumika na kuwa kichocheo cha kuongeza zaidi madhara ya ufukara wote huu kwetu.

Na kama huo ndio ukweli wa mambo basio Ndg Denis Mwamnyange, mwajiriwa wetu namba mbili katika jeshi letu la wananchi, hana budi kutambua kwamba wananchi tunaanza kuwa na mashaka juu ya nidhamu yao ile ilotukuka, pindi wanapotia miguu uraiani kuja kupumzika.

Kwa mantiki hiyo, hawana budi kuwakumbusha wastaafu wote kota jeshini kwamba kila walitendalo uraini hata baada ya miaka mingi ya kustaafu huakisi picha zuri au baya linalorudi kinyumanyuma mpaka kulipakaza uchafu jeshi au kulijenga zaidi.

Mwisho, kwa kuwa RUSHWA umejidhihirisha kuwa ni adui hatari kiasi hiki lenye uwezo wa kuligawa taifa vipande vipande kwa kipindi kifupi tu basi, mara baada ya kuondoa hili kundi la mafisadi na serikali yao, kwa pamoja tukalifikirie kuunda mitaala mipya ya somo

Katika masomo hayo mapya juu ya 'RUSHWA: NIDHAMU YA NAFSI, HAKI na UZALENDO' kama taifa tuhakikishe kwamba yanafundishwa katika hatua na idara zote za mafunzo nchini kama hatua endelevu ya kutokomesha hii sura mbaya na ya aibu viongozi kuwaibia walipakodi wao na taifa.
 
Wanajeshi mara nyingi ni vilaza kwa hiyo tusishangae wao ndio wanaoongoza nchi kuelekea kwenye umasikini uliokidhiri na yanayoteka ni sawa maana wao kila kitu wanataka kutumia nguvu badal ya akili!
 
duh good analysis ndio maana serekali yao haisikilizi watu. na inawezekana kabisa kuwa kuwaondoa pia kutahitaji mtutu na mikikimikiki...
 
Back
Top Bottom