Sangarara
JF-Expert Member
- Sep 29, 2011
- 13,100
- 5,649
Kuna uwezekano mkubwa kwamba katika jitihada zetu za kujikwamua kutoka kwenye umasikini tulio nao, watanzania tunatumia nguvu nyingi sana kukisakama chama cha mapinduzi kimakosa kwa sababu hakina ushawishi mkubwa kama tunavyofikiria kwenye mchakato mzima wa kuongoza serikali yetu zaidi ya kwamba viongozi wengi wa serikali ambao wameteuliwa kwa msingi wa kisiasa wanatoka chama hicho.
Moja ya Fact ni kwamba, sio Chama cha Mapinduzi, kwa maana ya kwamba hakuna organ yoyote ndani ya chama cha mapinduzi ambayo hukaa na kutoa maoni, au kupitia maoni au kuteua kiongozi yoyote katika serikali yetu. Kwa haraka haraka tunakilaumu chama cha mapinduzi kwa sababu viongozi wa serikali wanatokea huko kama mawaziri, wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya na kwa muda mrefu wabunge karibia wote na madiwani kwenye halmashauri zetu wamekuwa wakitokea chama hicho, lakini UKWELI ni kwamba hawa wote wamekuwa wakipatikana kutokana na mchakato wa uchaguzi wa kitaifa na sio wa kichama.
KIUKWELI KABISA, hata viongozi wa Chama cha Mapinduzi wanapodai kwamba ndio wanaoongoza serikali inatokana na uroho wa kuonekana kwamba wao ndio wenye madaraka, na labda kwa sababu wamekuwa wabunifu wa kujinufaisha na hisia za wao kuongoza serikai eti kwa sababu tu viongozi karibia wote wa serikali wana kadi au wanajitambulisha kama wa CCM.
Chukulia mfano Mbichi, Mwiguru nchemba anajitanua kwamba yeye yuko jikoni na kupigana kuitetea bajeti iliyowasilishwa bungeni, huu ni ujuha na utoto, sababu hakuna wakati wowote katika process ya kuandaa bajeti hiyo chama cha mapinduzi kinashirikishwa including mwigulu mwenyewe hata kwa nafasi yake ya uweka hazina wa chama,anachokifanya ni kuchukuliwa na hisia za utawala na kuanza kupayuka kama vile mtu amepandwa na pepo mchafu bila kujua anachokifanya ni nini, ndio maana katikati ya mjadala wa muhimu kabisa kwa watanzania watu wanaanza kubehave kama waganga wa kienyeji.
Bajeti hii wenyeviti wa kata, mashina,tarafa, vijiji,wilaya mikoa wala viongozi wa mabaraza yoyote yale ya chama cha mapinduzi hawajashiriki kuiandaa kama vile ambavyo hawatashiriki kwenye mchakato wowote ule wa utekelezaji wa bajeti hii, kama ambavyo haijawahi kutokea huko nyuma pia.
Wito wangu kwa watanzania, Hii ni serikali yetu na tusiwaachie mafisi wakaiharibu wakati sisi tunakimbiza kivuli.