CCM inaingilia kazi ya viongozi wa dini ambayo ni kupinga uovu na kusimamia haki

mabadilikosasa

JF-Expert Member
Dec 23, 2010
379
85
Wana JF
Kitendo cha CCM kuwapinga viongozi wa dini ambayo wamepinga dhambi iliyofanywa na CCM katika mchakato wa kupata meya wa Arusha na mauaji ya makusidi ya Arusha ni kuingliza kazi yao. Viongozi wa dini waliona haki ikitendeka ktk uchanguzi huu amani itakuwepo kwa wote ndo maana hawakuunga chama chochote mkono bali wakashauri uchaguzi urudiwe ili haki itendeke. Kitendo cha CCM kupinga kauli takatifu ya maaskofu ambayo ni ya kutenda haki kwa pande zote husika ni LAANA KWAO. CCM itapata laana kubwa na itasambaratika. Kitakacho saidia CCM sii udikta na wizi bala kusimamia na kutenda haki vinginevyo vilio, manunguniko, sala za maaskofu, taabu, mauaji ya raia, na wizi wa mali za raia, ni laana kubwa kwa uongozi wote wa CCM. wanaweza kufa mmoja baada ya mwingine au kupata misusukosuko, na taabu saana. Viongzoi wa dini ya kikristo hawakurupuki wanaongozwa na MUNGU. Kati ya mambo ambayo Mungu anasimamia kwa dhati ni HAKI. HAKI ni HAKI hata kama sheria ikiamua vinginevyo.Maana sheria wakati mwingine haitendi haki. After all mahakama pia ni sehemu ya ccm.
 
Serikali ya JK lazima iwaogope. Remember the first time JK kuanguka ilikua Mwanza ktk hafla ya kidini, the second time ilikua Bongo - Jangwani ambako wanaupako wanapigaga neno la Mungu kila kukicha - nako akaanguka. Sehemu za Mungu na wana-Mungu hazipendi/hawapendi zinamuadhirisha/wanamuadhirisha. Analindwa na Sheikh Yahya unategemea CCM inayoongozwa na JK wasiingilie wana-Mungu wanaomdharirisha ktk haki?
 
pale viongozi wa dini wanaposema ukweli alafu ccm inawabeza na kuwatisha, je viongozi wa dini wasipokema uovu ktk siasa, serikali, na jamiii, tutaendelea vipi? dhambi haina siasa. sharti ccm wafanye siasa kwa haki bila kuleta machafuko. Ina naana ccm wanataka viongozi wa dini wasikemea dhambi na uonevu ktk siasa? dhambi ni dhambi tuu haijalisha kama inafanyika kwenye siasa, jamii, au serikali.
kama wasivyofanya hivyo nani atafanya hiyo kazi? nani atatetea wangonge was watanzania,kuondoa ufisadi unaofanywa bila hao maaskofu?viongozi waadilifu wa dini ndo njia pekee ya sisi kupona. Maana serikali imeshindwa kazi ya kujenga ustawi wa jamii, na kutenda haki. Kimbilio la maskini wa tanzania ni viongozi wema wa dini zao. viongozi wa dini wasikate tamaa, waendelee kupinga dhuluma, wizi, na ufisadi wa ccm. hiyo ndo ajira yako kwa Mungu. Hadi hapo ccm itakapobadilika na kufanya siasa za kistaarabu na kujenga demokrasia ya kweli. By the way, wale viongozi waovu wa dini wanopigia magodi ccm na ufisadi wake, ccm haisemi wanachanga dini na siasa. wakikema uovu wa ccm, ccm hawataki. kuna uwezekano kabsa siasa kufanyika kwa haki, kama chi nyingine. ccm waombe radhi maaskofu kwa kuingili a kazi yao ya kupinga maovu na dhambi ktk jamii
 
Mkuu mabadilikosasa natambua umuhimu wa mabadiliko na hamu yako kubwa ya kutaka hayo mabadiliko.
Pamoja na hitaji hilo lakini pia tusisahau wajibu wakila mmoja kwa nafasi yake kuhakikisha haki inatendeka kwa kufuata taratibu.
Binafsi sina matatizo sana na tamko la maaskofu kulaani mauaji ingawa lililalia upande mmoja, na kikubwa hasa ambacho natofautiana na maaskofu ni tamko lao la KUTO KUMTAMBUA MEYA.
hayo mamlaka ya kutotambua viongozi waliochaguliwa na mamlaka husika kisheria wao wameyapata wapi na wametumia vifungu gani kutambua kuwa hakuwa halali?
 
ndugu paulss sharti uwe mkweli hata kama mungu wako ni ccm. watanzania wote tunajua hakuna uchaguzi wa haki wa meya ulifanyika arusha. siasa maana yake siyo kudanganya jamii. ccm wamefanya umafia arusha, kuchagua meya bila kura za wajumbe wa chadema. je hii ni haki????! Je siasa ni wizi na ubabe? je ccm inajenga demokrasia kwa njia hii? hamna haja ya kufunika ukweli hapa? ukweli ndo utatuletea maendeleo ya kweli. kilichofanyika arusha ni uharamia!. maskofu ambao ni watu wakutetea haki wamefanya kazi yako kutokana na ukweli wa hali halisi. tuache siasa chafu hapa, na tusema ukweli kwa mapenzi ya Mungu. CCM inabiga watu risazi mitaani arusha inageuza story kwamba raia walivamia kituo cha polisi. je hii ni haki? ccm imeshika madaraka ili kulinda haki,na maskini au mafisadi? jamani watanzania tuamke tutee haki. haki uinua nchi. hata nchi zilizoendelea zimeendelea kwa sababu ya kusimamia haki. haki ni haki tuu hata kama ni haki ya adui yako. vyama vya siasa pia vina wajibu wa kutendeana haki.
 
Tutawakomesha kwenye uchaguzi 2015. Labda waombe tusifike!
 
viongozi wema wa dini wasipokema udhalimu, wizi, ufisadi, chuki, na dhuluma ktk serikali, jamii, na siasa, mafisadi wa ccm watatumaliza???! pamoja na kuiibia raslimali zetu, itatuwekea viongozi mafisadi kama kina rostam, etc. kuingiza viongozi waovu ktk siasa ni kupalilia ufisadi. viongozi wa dini watusaidi kukemea ili tupate viongozi safi waliochaguliwa kwa njia ya haki na ya kidemokrasia, angalao tuweze kupiga hatua kimaisha. ccm ni chama cha watu wanaopenda maslahi binafsi. cheo kwao ni kula na sii utumishi.
 
Mkuu nakubaliana na wewe kwa kiwango kikubwa kwa mantiki ya kuwa ccm inawezekana wakawa wamefanya faulu na pia naweza kubaliana na wewe kuwa polisi wameua raia, pia nakubaliana na msingi mzima wa kudai haki kama ulivyo uainisha.
Nisicho kubaliana na maaskofu ni kitendo cha kufikia hatua ya kuanza kukataa kuwatambua viongozi, hivi leo wameanza na meya kesho watakuja kumkataa hata rais, jaribu kwenda mbali zaidi ya ukristo wetu, kesho wahindu nao hawa mtambui fulani kwa vigezo vyao, na kesho kutwa waislam nao hawamtambui pm, wapagani, mwingira nk, hii si itakuwa fujo.
kama hatuta kubali kila asasi inauwanja na mipaka yake kesho siasa zitahubiriwa makanisani na misikitini kwa kigezo hicho hicho.
Kinachotokea arusha ni mchezo wa kisiasa,ni ngoma ya kisiasa inayotaka umakini kutoa hukumu, niajabu kuona maaskofu wanatumbukia ktk kucheza ngoma hiyo upande mmoja.
Siasa ni mchezo mchafu na ndio maana wewe na wengi wanaona kama wanasiasa wanawakosea adabu maaskofu,hapana maaskofu wameyataka wenyewe ukiingilia siasa ukubali na adha zake, wewe unadhani jk majina na kejeli zote anazipenda? hivyo na maaskofu wasidhani ktk siasa kuna utakatifu, no.
 
Tutawakomesha kwenye uchaguzi 2015. Labda waombe tusifike!
Mkuu kwanza tuingie kwenye mchakato wa mabadiliko ya katiba kwa nguvu na akili zetu zote na tujiandae kupambana na wizi wa kura kwa nguvu zote...
 
watanzania nia amkeni....angalie swala ya arusha kwa busara ana nusu sahihi. msingalie nani kasema nini bali nini kimesemwa. maaskofu wamezungumza jambo la msingi. haki itendeke ktk siasa pia. haki isipondeka ktk siasa pia haitatendeka serikali. haki inaanzia ktk siasa. kiongozi anayechaguliwa kwa haki itatenda haki. haki lazima inaanze na uongozi wa siasa. midanganywe na ccm. viongozi wao wana mahela mengi ya kifisadi. cha kuzungumza hapa ni je maneno ya maaskofu kuwa uchaguzi haukuwa wa haki ni ya ukweli??? anachaneni na sera ya udini ya ccm ya kuwagawa watanzania, wakati mahitaji yao wote ni sawa. hakuna wa kutetea haki ya wanyonge tanzania zaidi ya maaskofu. mkiruhusu ccm ikawafunga midomo maaskofu nchi itaangamia. hakuna kaki polisi, wala mahakani, wala serikalini ila tuu kwenye vyombo ya dini sasa. maaskofu ndo sauti zetu sisi ambao hatuna silaha, sauti, fedha, wala magereza
 
viongozi wema wa dini wasipokema udhalimu, wizi, ufisadi, chuki, na dhuluma ktk serikali, jamii, na siasa, mafisadi wa ccm watatumaliza???! pamoja na kuiibia raslimali zetu, itatuwekea viongozi mafisadi kama kina rostam, etc. kuingiza viongozi waovu ktk siasa ni kupalilia ufisadi. viongozi wa dini watusaidi kukemea ili tupate viongozi safi waliochaguliwa kwa njia ya haki na ya kidemokrasia, angalao tuweze kupiga hatua kimaisha. ccm ni chama cha watu wanaopenda maslahi binafsi. cheo kwao ni kula na sii utumishi.

Mkuu hivi hao viongozi wa dini unawaona miungu watu? sindio hawa hawa wanatuambia jk ni chaguo la Mungu!!!, si ndio hawa hawa wanawapa mafisadi madhabahu kutole madukuduku yao? si ndio hawa hawa wanawapa mimba waumini wao na kuwabaka,si ndio hawa hawa akina mwingira wanaibia watu tu,si ndio hawa hawa wanagombea misikiti kujinufaisha wao, si ndio hawa hawa wanaopigana bakora kwa misaada ya tende na nyama za misaada.
Mkuu ufisadi na maovu yote yatatoka iwapo mimi na wewe na yule tutaamua na wala si hawa viongozi wa dini.
Dini ni issue sensitive sana, ni zaidi ya ufahamu wa kawaida, na ndio maana unaona mtu anauza malizake zote anakabidhi kwa kanisa, huku wengine wanavaa mabomu viunoni.
Achana na hii kitu bana, tufanye siasa imani zetu tuweke kando
 
ndugu paulss. Siasi si mchezo mchafu kama wengine wanaotaka kutuaminisha. Siasa imefanywa chafu tanzania na ccm ya sasa. kama siasa ni kama ccm walivyofanya arusha then hamna haya ya uchaguzi. lazima watanzania tufanye siasa kuwa mchezo safi kwa kuhakikisha haki inatenda. anayeiba uongozi hawezi kuwa mtumishi wa watu. Umeya ni utumishi na wala sii nafasi.

lazima watu wachaguliwe kwa demokrasia. Mie sio askofu lakini hata mimi meya aliyachaguliwa arusha sitaki hata kumwona maana najua ameiba uongozi. mie nadhani raia wote wa arusha wana wajibu kumkataa huyo meya kwa sababu hakuchaguliwa kwa misingi ya demokrasia bali kidicteta na ccm
 
Mkuu kwanza tuingie kwenye mchakato wa mabadiliko ya katiba kwa nguvu na akili zetu zote na tujiandae kupambana na wizi wa kura kwa nguvu zote...

Mkuu wewe ndio umekata mzizi wa fitina, katiba ikiwa nzuri mchezo umekwisha
 
Back
Top Bottom