Pundamilia07
JF-Expert Member
- Oct 29, 2007
- 1,439
- 54
Yafuatayo ni machache kati ya mengi ambayo CCM na serikali yake iliahidi 2005 kwa wananchi na imetimiza.
AHADI: KUENDELEA KUBORESHA MIUNDOMBINU YA BARABARA
Ujenzi wa miradi 15 ya barabara kwa kiwango cha lami yenye jumla ya urefu wa
Km. 1,398.6 imekamilishwa katika kipindi cha 2005 - 2010 huku ujenzi ambao
unaendelea ukiwa ni wa miradi 29 ya barabara zenye jumla ya Km. 2,536.4
AHADI: KUONGEZA BAJETI YA KILIMO NA KUKUZA SEKTA YA VIWANDA
Bajeti ya sekta ya kilimo imeongezeka kutoka asilimia 4.5 mwaka 2005
hadi asilimia 7.9 mwaka 2010 huku ukuaji wa sekta ya viwanda ukiongezeka kutoka asilimia 8.4 mwaka 2005 hadi asilimia 9.9 mwaka 2008.
Idadi ya wakulima wanaopata mbolea ya ruzuku imeongezeka kutoka wakulima 750,000 mwaka 2005/2006 hadi 2,076,710 mwaka 2009/2010 huku bajeti ya ruzuku ya pembejeo ikiongezeka kutoka bilioni 7.5 hadi bilioni 101.4 katika kipindi hicho cha miaka mitano.
Idadi ya wataalamu wa ugani walioajiriwa katika halmashauri imeongezeka kutoka wataalamu 3,379 mwaka 2007/2008 hadi 4,439 mwaka 2009/2010.
AHADI: KUKUZA NA KUBORESHA SEKTA YA ELIMU
Wanafunzi wanaojiunga na vyuo vikuu vilivyopo nchini Tanzania waliongezeka kutoka 55,296 mwaka 2005/2006 hadi 118,000mwaka 2009/2010.
Idadi ya vyuo vikuu imeongezeka kutoka vyuo vikuu 23 mwaka 2005 hadi kufikia vyuo 31 mwaka 2010.
Kuweza kujenga chuo kikuu cha Dodoma chenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 40,000 kwa mwaka na kwa sasa kina wanafunzi 17,282
Wanafunzi wanaomaliza elimu ya msingi na kuendelea na elimu ya sekondari wameongezeka kutoka 493,636 hadi 999,070 huku idadi ya wanafunzi wanaogharamiwa na serikali toka familia zenye kipato duni ikiongezeka toka 16,345 hadi 58,843. Ongezeko hili ni kati ya mwaka 2005 hadi mwaka 2009.
Uandikishaji katika elimu ya awali umeongezeka kutoka wanafunzi 638,591 hadi wanafunzi 889,363.
AHADI: KUKUZA NA KUBORESHA SEKTA YA AFYA
Kutoka mwaka 2005 hadi 2009,jumla ya zahanati 464,vituo vya afya 98 na nyumba za waganga 394 zilijengwa. Zahanati 1,037 vituo vya afya 285 na hospitali 112 zimekarabatiwa.
Vifo vya watoto wachanga vimepungua hadi kufikia 58 kwa kila watoto 1,000 wanaozaliwa hai mwaka 2009/2010.
AHADI: KUKUZA NA KUBORESHA SEKTA ZA MAJI
Huduma ya maji safi na salama kwa wakazi wa vijijini hapa nchini imeongezeka kutoka asilimia 58.7 mwaka 2005 hadi asilimia 60.1 mwaka 2009.
Fedha katika Mifuko ya maji zimeongezeka kutoka Sh bilioni 1.4 mwaka 2005 /2006 hadi bilioni 1.8 mwaka 2009/2010.
AHADI: KUBORESHA MASUALA YA KIJINSIA
Nafasi za wanawake katika ngazi ya maamuzi zimeongezeka kutoka asilimia 26 mwaka 2005 hadi 31 mwaka 2010.
Nitasema kweli daima fitina kwangu mwiko! CCM inapanda mbegu ya maendeleo, amani na utulivu.