CCM imewafanya wasomi watumwa?

Mukuru

Member
Apr 14, 2009
40
0
MWANASIASA mkongwe nchini, Musobi Mgeni ameibuka na kukishambulia Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa madai ya kuwafanya wasomi kuwa ni watumwa.

Akizungumza na Mwananchi Jumapili, jana mkoani hapa, mwanasiasa huyo alisema kuwa CCM imewapumbaza hata wasomi kiasi cha kuwafanya hata wasithaminike kwa elimu yao.

“Niwaulize wasomi wa madigrii yao, wewe mwandishi wa habari na wenzio ndio mjiulize, mimi sina shida yoyote na sijawahi kuwa mtumwa, lakini sasa hivi wasomi wote ni watumwa, mmekuwa watumwa katika nchi yenu,” alilalamika.

Alieleza moja ya athari za hali hiyo ni watu kuthamini fedha kuliko utu wala haki za wanyonge.

“Kama huna pesa hutakiwi wala kusikika,” alisema Mgeni katika mahojiano yaliyofanyika Kijijini kwake, Ndugu Wilaya ya Kwimba.

Mgeni ambaye aliwahi kuwa Mwenyekiti wa CUF mwaka 1995, alisema umaskini na njaa iliyopo nchini sasa hivi, haikuletwa na Mungu na badala yake imeletwa na utawala usiojali unaofanywa na CCM.

Alisema umaskini umewafanya Watanzania kuwa wajinga na kwamba hayo ndiyo matunda ya mauaji ya albino.

Alifananisha CCM na nyoka akasema mtoto atakayezaliwa na nyoka hawezi kutofanana na nyoka akiwa na maana kwamba kiongozi yeyote kutoka CCM atakuwa na mtazamo sawa na wenzake waliomtangulia.

-----------------------------------------

Najua humu JF kuna wasomi wengi tu...je, ni kweli tumefanywa watumwa na CCM kama anavyodai huyu jamaa? Au ni mtazamo finyu?
 
Najua humu JF kuna wasomi wengi tu...je, ni kweli tumefanywa watumwa na CCM kama anavyodai huyu jamaa? Au ni mtazamo finyu?

Nakubaliana naye kwa 220% ila nina bahati mie hata Chipukizi sikushurikia yaani nilikuwa mjanja kabla muda haujaisha .
 
MWANASIASA mkongwe nchini, Musobi Mgeni ameibuka na kukishambulia Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa madai ya kuwafanya wasomi kuwa ni watumwa....je, ni kweli tumefanywa watumwa na CCM kama anavyodai huyu jamaa? Au ni mtazamo finyu?

Mimi nadhani ametumia maneno mazito sana, ingawa kuna ukweli wa aina fulani katika aliyoongea, ukweli mkubwa unabaki palepale kuwa wasomi wetu wamejigeuza wenyewe kuwa watumwa nchini mwao kwa kutokutumia usomi na shahada zao vizuri na badala yake kuwa wanakimbiza mlio wa shilingi popote uliapo!
Na kwa hilo huwezi ilaumu CCM bali wasomi wenyewe kukubali kuwa watumwa.
 
Wasomi wenyewe wanajidharau! Wasomi wanakubaliana na mawazo ya kipuuzi ya wanasiasa et tu kwa sasababu ya ulaji! Wasomi wa Tanzania wanahitaji ukombozi wa kifikra. Hawana mwelekeo wa kuliletea taifa maendeleo zaidi ya kufundisha material ya miaka ya 47.
 
Tatizo huyo jamaa naye hajitambui kuwa naye si mwelewa. Kunatofauti kubwa kati ya msomi na mwelewa, mtu anaweza kusoma sana na akawa msomi somi lakini asielewe.

Tatizo la TZ na mimi hakika nikiwemo tumesoma vitabu na tumepta shule lakini uelewa sasa ndio mbinde ,sisi sio walewa ndivyo tulivyo na huyo jamaa akiwemo pia.
 
Mkuu wewe je ni Mwelewa? ama ndo wale wale watumwa?
 
TMtaisingizia sana ccm lakini tuna matatizo sana,kama mkuu umejibu bila kuelewa hapo unafikiri mambo magumu utaelewa??

Response ya Kitumwa tumwa hii......jaribu kuwa mwelewa kaka....achana na hilo jinamizi CCM
 
Sidhani kama CCM imewafanya wasomi kuwa watumwa ila wasomi wenyewe ndio wamejifanya kuwa watumwa,woga na magoigoi. Wasioogopa tumewaona na waliochoka kufanywa watumwa tunawaona ,wakiikimbia CCM. Wasomi hawa wanatumika katika kuendeleza dhulma ,wapo wanaotumia maneno mazuri katika kuwalaghai wapiga kura na wapo pia wanaotumia vishindo na vitisho ,wote hawa wamesahau walipotoka baada ya kuonjeshwa utamu wa madaraka ya kibabe.
 
Strategically 99.99% walioko madarakani si waelewa pia 99.99% ya wapinzani nao si waelewa,kwa hiyo 99.99999% ya wananchi nao si waelewa. kwa kifupi sote ndivyo tulivyo
 
Mimi nadhani ametumia maneno mazito sana, ingawa kuna ukweli wa aina fulani katika aliyoongea, ukweli mkubwa unabaki palepale kuwa wasomi wetu wamejigeuza wenyewe kuwa watumwa nchini mwao kwa kutokutumia usomi na shahada zao vizuri na badala yake kuwa wanakimbiza mlio wa shilingi popote uliapo!
Na kwa hilo huwezi ilaumu CCM bali wasomi wenyewe kukubali kuwa watumwa.
ni kweli tumeshindwa kujitambua pamoja na usomi wetuu ila kwa kiasi kikubwa mfumo wa utawala ulisaidia kutufanya kutokujitambuaa..

natumai nafasi nia na uwezo bado tunao sanaa kubadilika na kusonga mbele kwa kuachana na utumwa huoo.

TUJITAMBUEE ....TUTAFANIKIWAAA
 
Naona itakuwa haku tukisema wasomi wamepeleka kwenye utumwa wa CCM. Si haki kuilaumu CCM kwa kila kitu, mbona Dr Mkumbo hayuko CCM. Nakumbuka kuna siku Shivji alikuwa anawaasa sana maprof wenzake kuwa wasiingie kwenye mchezo huo wa kujichafua na kuharibu sifa yao. Mmoja anaitwa Baregu alimtukana sana Shivji, lakini baadaye ikajaonekana alichosema Shivji ni kweli, Baregu sasa hivi hata akitaka kujiunga na chama chohcote ataonekana hana maana labsa ccm tu.
 
Mbona Baregu ni memba wa Chadema! fanya utafiti kabla ya kupost mambo hapa!
 
Tatizo huyo jamaa naye hajitambui kuwa naye si mwelewa. Kunatofauti kubwa kati ya msomi na mwelewa, mtu anaweza kusoma sana na akawa msomi somi lakini asielewe.

Tatizo la TZ na mimi hakika nikiwemo tumesoma vitabu na tumepta shule lakini uelewa sasa ndio mbinde ,sisi sio walewa ndivyo tulivyo na huyo jamaa akiwemo pia.

Mkama hakuna msomi (sio msomaji) asiye mwelewa. Tatizo ni kwamba baada ya kuelewa unafanya nini hapo ndo kuna mgogoro mkubwa. Kila mtu ukimuuliza sababu za umaskini wa nchi hii utapata majibu lukuki, lakini hakuna anayechukuwa hatua. Bunge letu leo lina idadi kubwa ya maprofesa na madaktari wa PhD achilia mbali zile PhD za ccm. Inawezekana kabisa kwamba wengi wao taaluma zao si za kisiasa lkni kwa level yao, kuelewa mambo mengine ya kawaida ni rahisi zaidi. Haya basi wanafanya nini? Kwa kuwa wameshindwa ku-argue nao kisomi wamejiunga nao kufilisi nchi. Ni watumwa tu tena watumwa kwa sababu ya uroho tu!

Alifanya aloweza, kuijenga Tanzania
wala sio namkweza, kaiweza Tanzania
Hata mkimpuuza, hampuzi Tanzania
Mola mpe pumziko, tena pumziko la amani

Ole wenu warithi, muipuzaao nchi,
Elimu wenu urithi, mlipewa jenga nchi,
Mmegeuza huu urithi, mrija nyonyea nchi,
Mola wape ufunuo, wakumbuke wajibu wao
 
Back
Top Bottom