CCM imeteka vyombo vyote vya Habari na Mawazo ya Watanzania

Unakumbuka CCM ilidai kuwa CHADEMA ni chama cha msimu, na kwa kupuuza hoja za CHADEMA ya Ufisadi na orodha ya watuhumiwa wa Ufisadi, wakati wa kampeni Kikwete akazunguka nchi nzima akikumbatiana na MAFISADI PAPA? Leo "mende kadondosha kabati" yule yule aliyekuwa akiwakumbatia Mafisadi Papa na kuwanyanyua mikono juu anadai MAFISAI HAO wanachafua taswira ya CCM.

CHADEMA ni chama kinachojisimamia na kubuni hoja zake ambazo ni endelevu kama ile ya Ufisadi, watuhumiwa wa Uifisadi ambazo zimekuwa zikiipeleka puta CCM since 2007. CHADEMA ilibuni na kusimamia hoja ya Katiba Mpya; kwa kuwa CCM is a reactive party ikarukia hoja hiyo japokuwa haipo katika Ilani yake ya Uchaguzi ya 2010. Based on those facts between CCM nad CHADEMA which is reactive party kila kinachobuni hoja zake au kile kinachoacha Ilani yake na kurukia hoja za chama kingine?

I think you have a good argument here Jatropha, but hii dhana ya kujivua gamba haikuanza sasa na mafisadi katika CCM.
Sijui kama unakumbuka enzi za KUNG'ATUKA katika uongozi wa chama miongo kadhaa iliyopita.
CCM inahistoria ya kujisahihisha bila kutibua wananchi na hili la sasa tulilitegemea baada ya makelele mengi.
Ni kweli kwamba sauti nzito na publicly katika siasa za karibuni zilianzia CDM na vyama vingine.
What I can tell you is, hivi karibuni CCM ni kama chombo kilichovamiwa na pirates, na wakaiteka nyara chombo hicho cha watu wengi ambao ni masikini.
Si kwamba wana CCM hawakuona matatizo haya, waliyaona mapema sana lakini ilikuwa nani amfunge paka kengele.
Mimi mwenyewe niltoa hoja ya kuwa chama tawala inaanzankukosa muelekeo na dira-and I was shouted down.
Tuache fikira ambazo mimi naona si za kizalendo, kufikiria it is either CCM or CHADEMA. Vyama vya upinzani vimefanya kazi nzuri tu ya kukiamsha chama na kukikumbusha muelekeo wake-na wamesikia.
Ufisadi haukuwagusa wana CDM tu katika jamii, bali kila mtanzania.
Na kwa hakika nitakuwa mnafiki nisipowapongeza wanaharakati,CDM na wengine wengikwa kampeni ya kuwaamsha CCM toka usingizi mzito wa kutekwa na mafisadi.

Yes sasa CCM wameamka , CDM itaingia usingizini, thats my view.
CDM hawana siasa inyoeleweka vile vile maana hata kama wataingia serikalini mpagilio wa wa kutatua mtatizo ya wananchi hawajaueleza bayana.
Na je CDM ni chama cha kibepari au kisoshalisti?na je juu ya umilikaji wa mali na ardhi wana maono gani?
Masuala ya kodi kwa biashara na wafanyakazi kwa maono ya CDM yakoje?
Hay ni mambo ya muhimu kwa watu kujua na si kukishabikia chama ambacho malengo yake hayajulikani baada ya kukamata dola.
 
You can say it again!
 
Jamani nisaidieni hivi kunz tofauti kati ya Anna Makinda na Anne Semamba Makinda angalia mjumbe no 19 na 32 ndo yuleyule au watu wawili tofauti
 
Mkuu Kiloni, this is a good observation, it only lacks the historical perspective.
Upinzani kwa mafiisadi ulikuwa sehemu zote kutoka CDM,ndani ya CCM na hata katika Baraza la Mawaziri.
Mbona watu mnasahau haraka, mmeshamsahau Mwakyembe,Sitta,Selelii,Ole ,Manyanya na wengine?Hata JF wamefanya mchango mkubwa katika hili.
Na je hawa walikuwa CDM?
Kwamba CCM ilikuwa na matatizo makubwa halina ubishi, kwamba wamegutuka vile vile halina ubishi.Mimi siwatetei kwa ufisadi nawatetea kwa KUTAMBUA mwelekeo wa hisia za wananchi wa Tanzania.
As for policies lazima tukubali kuwa tupo katika transition kutoka socialism(ujamaa) na kuelekea kusikojulikana.
Hapa ndipo panakangaya,thinkers katika chama tawala ni wachache mno kuelezea kule tunakoelekea.
Mbaya zaidi ni hivi vyama vyetu vya upinzani,CDM included,havina policy inayoeleweka.
Kukosoa serikali kila mtu anajua lakini mpangilio wa njia ya maendeleo, kisiasa hakuna anayethubutu ku propound hilo.
Wengi wetu si wajinga sana maana makundi yaliyomo CCM ni yale yale yaliyomo CDM, ukiondoa wachache.
Hata ndani ya CDM kuna walio fanya ufisadi ndani ya mabenki yetu na wako kimya! as if hawapo.
What I am saying is -enough with the noise-lets start thinking again.

Mstahiki Lole,
Umegusia mengi bila kutoa ushahidi na uhalisia....pengine muda ukifika unaweza fanya hivyo.

Mi nimeguswa na point moja tu, Tz ifuate sera gani. Hilo nadhani ni more unstringed so ungeligusia. Woga walio nao hao wengine naona nawe unao...kwa nini usiseme unafikiri mfumo/sera/siasa gani ifuatwe?

Mi for one, I delare once more my opposition and rejection of ujamaa but I proponents ubepari for politics and economics. Kijamii mwaweza wasoshalist au mabepari wa kati it will reflect how best the two are to the society.
 
Nimekua nikufuatilia kwa makini tangu wiki iliyo pita baada ya kile kilicho elezwa nkuwa ni kujivua gamba kwa CCM ssa ni dhahili kila mtanzania ameanza kuimba wimbo wao wa kujivua gamba iwe ni kwa kusifia au kupinga hatua hiyo ya kujivua gamba! Ukiangalia hap JF thread nyingi zinazunguka na CCM! Magazeti mengi na vyombo vya habari Radio,Tv na hata tovuti navyo vinajadili habari ya CCM kujivua gamba! Suala la kujivua gamba kwa CCM limefanya hata Dr Slaa asahua na ile habari yake ya kuipa Serikali siku 21 kule Arusha juu ya Meya alie ingia madarakani kiujanjaujanja! Watalaamu wa Siasa wanasema hata habari ya Dr Slaa kule tabora kuongeza orodha mpya ya Mafisadi nayo ni taharuki ya CCM kujivua gamba! Wengine wanasema orodha mpya ya Dr Slaa ambayo imemhusiha na Dr Magufuli haijapokelewa kwa umakini na Watanzania kwani wingu liliopo ni habari ya kujivua gamba! Nape Nnauye amekua kinara kwa kuogelea juu ya agenda ya kujivua gamba! Leo Katibu wa Uenezi Chadema bila kujijua nae ameingia kwenye hoja hii ya kujivua gamba! Leo gazeti la Mwananchi ukurasi wa mbele imeandikwa kuwa Dr Slaa amempa Kikwete siku 90 ajivue gamba ikumbukwe tayari Dr Slaa anakipolo chake cha siku 21 kule Arusha alicho ipa serikali! pia Dr Slaa amekaririwa akisema kitendo cha kutakuwafukuza Lowasa,Rostam na Chenge ndio anguko la CCM vipande vipande!,lakini amesahau kuwa Lowasa,Rostam na Chenge hakuna chama chochote hapa Tanzania kinacho weza kuwapokea kwa sasa wananuka na wamekosa mvuto wa kisiasa kabisa,kuondoka kwao CCM ni sawa na kutupa mzoga na nzi wasikufuate tena! Hivyo imekua gamba gamba gamba kila kona.......!

My take: Siasa mara nyingi inahitaji uwe focused na mambo unayo yasimamia,lakini kuna utalaam wa kupindisha hoja ya mwenzako kwa kuibua jambo fulani kwa jamii!
Chadema ni mhimu kupima suala hili lasivyo itajipotezea muda wake kwa kurukia agenda wasiyo ijua!

Kwanini iko hivyo?

Kwanza, nchi nyingi za Africa na Asia hazijapokea vizuri suala zima la demokrasia shirikishi ya vyama vingi. Kwa hiyo watawala wameendelea kutumia mifumo kandamizi ikiweamo vyombo vya habari, majeshi, rushwa, vita na/au vitisho ili mradi ulaji wao na milki zao zinaendelea kutamalaki.

Pili, ni historia ya mfumo/sera/desturi nk. Nchi nyingi za Africa zilifuata siasa za usoshalist/ukomunist (kila mtu kwa nafasi na uwezo wake). Moja ya nguzo kuu za ujamaa ni kuthibiti uchumi/mali, uhuru wa fikra, mawazo na mienendo, kisha njia ya ukiritimba (kofia mbili nk) ambao mara zote ulizaa rushwa na madudu kibao. So kwa ufupi Tz na vyombo vyake vya habari kuhodhiwa/kuratibiwa na mawazo/habari za ki-CCM CCM ni matokea ya kawaida kwa historia ya hapo nyumbani.

Kwa hiyo ni kazi kwa ukombozi kwa kila nyanja na kwa kutumia utandawazi kufikisha ujumbe wa ukombozi kwa umma. Njia kama ni nzuri, pia kuanzisha tv/redio/magazeti na makongamano ili mradi njia ambayo ni muafaka kufikisha ujumbe. CCM wakati huo watatumia propganda, vitisho nk lakini will be too late.

Haiwezekani Chadema idhani kuwa CCM itatoa hisani ya uhuru sawa wa vyombo vya habari. Wasilalamike, wabuni njia ya kupata vyao.....lakini mwisho wa siku ni kama ulivyosema ...lazima waangalifu unasoma nini unasikia nini.
 
Mlengo wa Kati, kuna wengi wa aina yako ambao mko alarmed kwa CDM kuwa overtaken na events za kujivua gamba kwa CCM-kitu ambacho watu wengi wamefurahia.
Kwa upande wa CDM ni kama wamenyang'anywa hoja, zaidi ya ufisadi hawana cha kuwaambia wananchi!
CCM wamecheza mchezo safi kabisa wa kisiasa na kuwafunga goli CDM kwa hoja yao na sasa hakuna hoja tena.Hata CDM ikija na orodha nyingine ya mafisadi haina mshiko wala manufaa kwa vile sasa hivi suala hili linashughulikiwa.
Watu hawali kelele za ufisadi.
Kwa muelekeo wa sasa CDM kitabaki kuwa chama cha kuchambua mapungufu ya CCM huku wao wenyewe kutokuwa na siasa mbadala ya maendeleo na isije ikajidanganya kuwa an alternative party yenye uwezo wa kutawala kwa sasa.
Asalaam Aleikhum!

Kwenu mnasherehekea kwa joka kujitoa gamba. Wanaharakati ni msiba. Kwani tunajua ndiyo mwanzo wa werevu na ujanja wa kugonga (ufisadi). Dawa ya lijoka ni kuliua siyo kujitoa kwake gamba. Ushalogwa ufahamu wako na mwenge.
 
Mstahiki Lole,
Umegusia mengi bila kutoa ushahidi na uhalisia....pengine muda ukifika unaweza fanya hivyo.

Mi nimeguswa na point moja tu, Tz ifuate sera gani. Hilo nadhani ni more unstringed so ungeligusia. Woga walio nao hao wengine naona nawe unao...kwa nini usiseme unafikiri mfumo/sera/siasa gani ifuatwe?

Mi for one, I delare once more my opposition and rejection of ujamaa but I proponents ubepari for politics and economics. Kijamii mwaweza wasoshalist au mabepari wa kati it will reflect how best the two are to the society.

Mkuu Ronal(d?) Reagan, kati ya posti nyingi nilizoweka nafikiri wewe ndio umenipata drift ya argument yangu.
Kupata mlengo wa siasa inayotakiwa kwa malengo makubwa zaidi ya maendeleo ya kasi ndiyo suala ambalo karibu vyama vyote vinakwepa kutoa michanganuo.
Hili suala si rahisi kama linavyoonekana maana linahitaji vision ya uhakika kutoka kwa wanasiasa wakitilia maanani matakwa ya maendeleo na matatizo ya wananchi.
Wale wa kupanga mikakati hiyo ni economic theorists and planners kabla ya kuingia serikalini.
Ni lazima hiyo vision iwe inatokana na economic model inayotekelezeka.
Kati ya watu waliothubutu kuwa na vision ya kule tunakotaka kwenda ni Mwalimu,kwamba hakufaulu pengine ni kwa sababu ya umasikini,uhaba wa wasomi na watekelezaji kwa wakati ule.
Siamini kuwa ujamaa umeshindwa maana China, Vietnam imeweza,Vile vile nchi za mifumo ya kibepari kama India na Malaysia etc nazo zinasonga mbele.
Sisi tusiishie katika kupigana vikumbo vya ufisadi tu tapange yajayo kulingana na dira tunayo jitakia.
 
Back
Top Bottom