CCM imeshindwa kuendesha shule zake itawezaje kuongoza nchi?

thereitis

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
297
41
Chama cha Mapinduzi kupitia jumuiya yake ya wazazi kimeshindwa kuendesha shule zake za sekondari. Siku chache zilizopita tumeshuhudia naibu waziri wa elimu na Ufundi akifunga shule mojawapo inayomilikiwa na CCM mkoani Morogoro. Muda mfupi uliopita TBC1 imeripoti maandamano ya wanafunzi wa shule ya sekondari Pwani inayomilikiwa na CCM mbele ya ofisi ya mkuu wa mkoa wa Pwani wakitaka matatizo makubwa yanayoikabili shule hiyo yatatuliwe. Wanafunzi hao wanadai shule hiyo haina walimu wa kutosha, majengo mabovu na upungufu wa huduma muhimu kwa ajili ya kuwezesha upatikanaji wa elimu bora.

Nieshuhudia uchakavu mkubwa wa shule ya sekondari Kibohehe iliyopo wilayani Hai mkoa wa Kilimanjaro. Pia shule hiyo haina walimu wa kutosha, uongozi dhaifu unasababisha ufaulu duni ktk mitihani.

Je, kama CCM kimeshindwa kuendesha shule zake itawezaje kuongoza nchi hii ambayo ni kubwa na ina shule nyingi kuliko inazomiliki? nchi ambayo wananchi wake wanahitaji kupatiwa huduma mbalimbali za jamii kutokana na kodi wanazolipa? CCM itawezaje kukusanya kodi na kuwekeza katika miundombinu mbalimbali kwa lengo la kumwezesha mwanachi wake aendeshe shughuli binafsi?

Mimi nasema CCM haiwezi kuongoza wala kuendesha serikali ya JMT.
 
Mdhaifu sana!
 
Chama kinaongozwa na mwenyekiti DHAIFU na nchi pia inaongozwa na rais DHAIFU, unategemea nini hapo???
 
Udhaifu wa CCM unadhihirishwa na makundi yanayofikiria urais 2015 badala ya kutumikia watanzania
 
Back
Top Bottom