CCM imekuwa ya hovyo zaidi chini ya JK na Makamba -- yes or no?

Zak Malang

JF-Expert Member
Dec 30, 2008
5,404
234
Wadau,

Tumeshuhudia sisi wenyewe kwamba tangu JK na Makamba washike uongozi wa chama hiki kikongwe nchini, mwenendo wa chama hicho umezidi kudhoofika na kuwa wa hovyo hovyo tu -- ni kama vile hakuna uongozi kabisa wa kuweza kukemea wale wanaosababisha uhovyo huo.

Baadhi ya makada wa chama hicho wamefikia hadi kutishiana kuuwana kutokana na tamaa ya kufanya ulaji wa nchi (soma gazeti la Habari Leo la leo -- kuhusu waziri mmoja aliyeshindwa kura za maoni kutishiwa kuawawa).

Jee, hii si inamaananisha hitma ya CCM inakaribia?
 
hapana tena kubwa...CCM IMEJIIMARISHA ZAIDI NA ZAIDI......SI MIJINI TU KAMA CHADEMA BALI HATA VIJIJINI......! NCHI NZIMA CCM INARINDIMA NA IMEDHIHIRIKA KAULI YA NYERERE KUWA UPINZANI WA KWELI UTATOKA CCM BAADA YA WABUNGE ZAIDI YA 60 KUANGUSHWA KWENYE KURA ZA MAONI.........halafu wewe unasema imefanya vibaya zaidi kwa ushahidi wa habari ya gazeti?
 
CCM ya JK imejaa mizengwe kibao! Wakati wa kura wananchi siku hizi wanauita ni wakati wa "kuvuna!" Ni ufisadi kwa kwenda mbele!
 
Ni meli isiokuwa na nahodha mweledi na hatma yake haiko mbali.
 
CCM ya Jk imeweza kurudisha heshima iliyokuwa inataka kuondoka,imejiimarisha sana na hata demokrasia imepanuka kuliko wakati mwingine wowote katika historia yake.
Katika hali hii hata vyama vya upinzani navyo vimeweza kupumua kutoandamwa kama zile enzi za Mrema na mabomu,na kusema kweli demokrasia na uwazi uliomo ndania ya CCM sasa hivi umetanuka na kuingia hadi kwenye vyama vya upinzani.
 
Yeyote anayetetea CCM ni msaliti mkubwa! Hata hamuoni haya!!! Mafisadi wamejaa katika ngazi za juu za CCM, hata hakuna hatua zinazochukuliwa, bado tunaona wanapeta tu, na wengine kupatiwa majina kama 'kingmaker'. Hivi hamuoni wizi wa nje nje, ubinafsi na ujengaji wa 'dynasties' ulioibuka katika kipindi hiki cha utawala wa CCM? Nyie hamtaki mabadiliko uozo huo uondoke?
 
Kikulach ki nguoni mwako. Wakipigana sana zengwe, ndio wataweza kuona umuhimu wa kurudisha nidhamu na kufanya usafi ndani ya chama. Yote haya hayaji kwa bahati mbaya. Ni matokeo ya mambo yanayoendelea kufanyika hapa na pale
 
anayebisha kwamba CCM haijafanya mambo ya hovyo anahita kupelekwa Milembe.
 
Yeyote anayetetea CCM ni msaliti mkubwa! Hata hamuoni haya!!! Mafisadi wamejaa katika ngazi za juu za CCM, hata hakuna hatua zinazochukuliwa, bado tunaona wanapeta tu, na wengine kupatiwa majina kama 'kingmaker'. Hivi hamuoni wizi wa nje nje, ubinafsi na ujengaji wa 'dynasties' ulioibuka katika kipindi hiki cha utawala wa CCM? Nyie hamtaki mabadiliko uozo huo uondoke?

Inategemea usaliti dhidi ya Chadema au CUF??Au usaliti dhidi ya nchi?Mafisadi walikuwapo tangu enzi na wapo dunia nzima na serikali zinajitahidi kupambana na ufisadi kwa njia tofauti.Tatizo ni njia zipi za kuondoa ufisadi.Serikali ya JK imetumia njia tofauti na ile ya Mkapa.Si rahisi kupigana na ufisadi wa nchi inahitaji ushupavu wa akili na busara.
 
Hata huko vijijini ccm wanakofikiri kuna watu wasioelimika watakaowapa kura wataelimishwa mwaka huu. Vijana wa vyuo vikuu serikali ya ccm inayowaondoa vyuoni kila ifikapo uchaguzi ili waifanyie vurugu taaluma, wamejitolea kutoa somo la uraia. Ccm baada ya kuwa na viongozi king'ang'azi waliowasukumia mbali waasisi wa chama na kukumbatia mtandao ambao msingi wake ni ufisadi lazima chama kiwe cha hovyo hovyo. jK na makumba wamekuja kwa wakati muafaka wa kusudi kamilifu la Mungu kuizika ccm iliyofikiri itatawala milele.
 
CCM ya Jk imeweza kurudisha heshima iliyokuwa inataka kuondoka,imejiimarisha sana na hata demokrasia imepanuka kuliko wakati mwingine wowote katika historia yake.
Katika hali hii hata vyama vya upinzani navyo vimeweza kupumua kutoandamwa kama zile enzi za Mrema na mabomu,na kusema kweli demokrasia na uwazi uliomo ndania ya CCM sasa hivi umetanuka na kuingia hadi kwenye vyama vya upinzani.

Tatizo kubwa la watanzania sio "demokrasia" bali ni umaskini uliokithiri, ambapo CCM iliahidi kuleta Maisha Bora kwa kila mtz! Hebu tuambie demokrasia ya CCM imesaidiaje kuleta maisha bora iliyoyaahidi? Kusema ukweli CCM si tena "Chama cha Wakulima na Wafanyakazi" ndio maana JK anaweza kutamba kwamba hahitaji kura za Wafanyakazi kwa kuwa hawathamini tena! Ni Chama cha Wafanyabiashara na wenye fedha! Bila fedha siku hizi shahau uongozi ndani ya CCM! Hiyo ndiyo "Demokrasia" ndani ya CCM!
 
zamani wakati nakua CCM ilikuwa chama cha wakulima na wafanyakazi, leo hii CCM imepora na wafanyabiashara na mataijiri wachache. Ni chama kinachochezea uhai wa taifa. NATAMANI SIKU MOJA IFIKE AMBAPO WANACHAMA WA CCM WATASEMA TANZANIA KWANZA CHAMA BAADAE. UZALENDO UTAFUFUKA TOKA KTK MIOYO YA WATU. TODAY THERE IS NO NATION SPIRIT NI KILA MTU SHAURI YAKE. MCHAKATO ULIOFANYWA NA CCM KTK KURA ZA MAONI KILA MTU NI SHAHIDI SASA KUWA CCM INAMWAGA DAMU NA TAYARI IMEMWAGA DAMU WANACHAMA WAKE WAMEWAMEPIGANA LAITI INGEKUWA IMEFANYWA NA VYAMA VINGINE UNGESIKIA TULIWAAMBIA HAO NI WAGOMVI LAKINI LEO WAKO KIMYA NI AIBU KWA CCM, AMBAO WAMEKATAA KUMRUDISHIA MUNGU UTUKUFU KWA AMANI TULIYO NAYO WANADAI ETI WAO NDIO WAMELETA NA KUTUNZA AMANI TANZANIA, WAKATI AMANI YETU NI KWA UWEZA WA MUNGU, DAWA NI MOJA TU NDUGU ZANGU WATANZANIA LET US VOTE THEM OUT OF POWER. INAUMA SANA INAUMA SAAAANAAAAMMMM JAMANI AAAAAAAH:rant:
 
wasioamini ubovu wa huyu bwana ni ndugu zake tu na makamba ambo hakika wapo tayari hata kufa nae au kwa vyovyote vile wapiga debe na kumpaka manukato yalioyooza.........
Kura yako kwa nani mwaka huuu?????????
 
unatakiwa kuwa na moyo wa kichaa au mwenda wazimu kusapoti ccm...lakini ccm watuymia vizuri elimu ndogo ya watz wanaoishi vijijini.....eee Mungu tusaidie
 
Kama tunazungumzia CCM katika historia yake, naweza kusema ilikuwa mbaya zaidi wakati wa Mwinyi na Kolimba ambapo ilibidi hata Nyerere aingilie kati kuokoa chama 'chake'.
 
Kwa maoni yangu, CCM imekuwa na demokrasia zaidi kuliko wakati wote wa uhai wake... na hata rushwa zilizorepotiwa karibuni ni juhudi za CCM yenyewe kujisafisha... Wenye akili ni muhimu kuangalia mambo kwa mapana yake.
 
Back
Top Bottom