mmaroroi, kumbe Dr. Slaa bado ni rais wenu mtarajiwa?, uchaguzi wa 2010 umeisha na mshindi amershatangazwa, sasa huyu mtarajiwa ni kwa mwaka 2015?, maana uchaguzi huo haujatangazwa, unless amebadili nia na kutangaza rasmi kuwa mwaka 2015 hagombei au?.Rais wetu mtarajiwa Dr.Slaa umenikuna na ninakuahidi na watanzania ni mashihidi kuwa wanajua wewe ndio Rais wao mioyoni mwao,uendelee kutujuza mambo na kutupigania kwani tunaamini Marehemu Baba wa Taifa hili J.K.Nyerere amerudi kupitia kwako.
nginda, asante kwa hili, na hili ndilo mimi nimekuwa nikilisemea, anatakiwa aseme neno moja tuu na roho zao zitaponywa!, nilitamani aseme siku ile ile baada ya kazi, wala sio kushikana mikono na mtu, wala sio kukubali matokeo wala kuyasaini, bali kuwaambia waliompa kura zao, asanteni, na kuwaeleza tuwe wavumilivu, tuvute subira na ustahilivu wakati wakuu wa chama wakitafakari hatua muafaka za kuchukuchua.I regret why Dr. Slaa you are not my president. Ombi langu kwako na chama kwa ujumla, Ukipata muda zungumza na wananchi wako uwashukuru ili wasijisikie wapweke.
Tuko, Asante sana kwa ushauri huu, ni kweli hapo mwanzo nilijiita mchambuzi wa siasa, baada ya kuelimishwa mchambuzi anatakiwa aweje, na moja ya sifa kuu ya mchambuzi ni kufanya scientific research kwa kutumia vile vigezo rasmi vya utafiti, kuanzia intro, preamble, then plausible major and minor ndipo unapata Scientific and logical conclusion toka kwenye "major and minor" na mwisho bila kusahau references.Pasco, naamini kuwa wewe ni mchambuzi wa mambo ya siasa...
Naomba kukupa homework..
Fanya utafiti wa kina, kuhusu suala la CHADEMA kuunda kambi ya upinzani peke yake. Katika hili naomba uje na analysis inayoonyesha 'Ni kwa vipi, na kwa nini CHADEMA imeunda kambi ya upinzani peke yake? Je, wameamua au wamelazimika? Je, wamefanya hivyo kwa maslahi yao, au kwa maslahi ya Watanzania. Je, kulikuwa na alternative gani katika hili?
Naomba utafiti wako uwe na data halisi zikihusisha majibu toka kwa wadau wote wa hili jambo. Naomba uzuie sana hisia zako binafsi katika uchambuzi wako. Nimeainisha haya katika thread niliyoanzisha, ya homework kwa wachambuzi wa siasa...
Pasco nadhani to be fair tuseme ukweli kwamba Kaulila Hakufukuzwa Chadema bali baada ya kumuondolea madaraka, kwa hasira alijiondoa yeye mwenyewe Chadema.Geza Ulole, amini usiamini, sina tatizo na Mbowe kuwa ndiye kiongozi wa upinzani bungeni tatizo langu ni si lazima awe yeye simply kwa sababu ni Mwenyekiti. Nimezungumzia point muhimu sana inaypotwa powers from within, Dr.Slaa anayo na Zitto anayo, sorry to say, Mhe. Mbowe hana!.
Victory yoyote hupatikana kwa consolidation of powers na kuzipangia strategies, ndio maana hata vitani, majemedari sio wakaao mstari wa mbele kwenye the line of fire, wanaokaa mbale ni wapiganaji, Mbowe ni Jemedari wenu, Zitto ni mpiganaji wetu. Nafasi ya kioungozi wa upinzani bungeni, haimuhitaji jemedari, inamhitaji mpiganaji kushusha vipigo tuu.
Bunge lililopita, Hamad Rashid ndio alikuwa kiongozi naye ni too diplomatic ila waelewa wanajua it was powers za Dr. Slaa ndizo zilizokuwa major factor of which I doubt kama Mbowe ataruhusu powers za Zitto zimbypass.
Dhana ikijengeka, hata kama ni ya uwongo, hugeuka sumu, maadamu chama Chenu Chadema, tayari kimegubikwa na dhana fulani fulani, msisubiri uchaguzi sijua miaka mingapi ijayo, you have to act fast, kama niliwashauri CCM, Makamba ni liability kwa chama chao, ameshawacost dearly, wakisubiri mpaka 2012 wakati wa uchaguzi wao mkuu, demage inazidi kuongezeka itafikia wakati itakuwa too little too late!.
Naomba nisieleweke kama nampigia chapuo Zitto, nimemtaja tuu kwa sababu nina uhakika na uwezo wake, kumfukuza kafulila was a mistake, lili lilikuwa jimbo lenu, kumuengua Mwera was a mistake, jimba mmelitoa sadaka, sasa vitu kama hivi ni vi cancer vidogo vidogo vinavyoitafuna Chadema from within, cancer ikigundulika, inakatwa kabla haijasaambaa, ama nayo isubiri uchaguzi?.
Tuko, Asante sana kwa ushauri huu, ni kweli hapo mwanzo nilijiita mchambuzi wa siasa, baada ya kuelimishwa mchambuzi anatakiwa aweje, na moja ya sifa kuu ya mchambuzi ni kufanya scientific research kwa kutumia vile vigezo rasmi vya utafiti, kuanzia intro, preamble, then plausible major and minor ndipo unapata Scientific and logical conclusion toka kwenye "major and minor" na mwisho bila kusahau references.
Ndipo nikajigundua kumbe mimi sio mchambuzi, ili kuwa mchambuzi lazima uwe mtafiti, hivyo nimesharekebisha, mimi sio mtafiti, bali just a political comentator, yaani mzungumziaji tuu from the poit of view ya a layman, yaani yule mtu wa chini kabisa.
Kwa ndugu yangu Tuko, tuendelee kuwa Tuko pamoja, homework yako hiyo siwezi kuifanya si unajua elimu zenyewe zetu za Watanzania, ila pia naomba kwa vile tuna maresearchers wengi, wakiona inafaa, watatusaidia.
NB. Linapotokea jambo, kama mtu ni mhusika, unajua A-Z na husemi, unategemea wasiojua watajuaje?, mimi na wananchi wenzangu tunasubiri hao wajuaji waseme nasi tusikilize, ndio maana wengine wetu, hatuna shughuli yoyote ya kufanya, bali tunapenda kujiendea tuu viwanja vya Bunge hapa Dodoma, mfano nilidokezwa Bunge kukaa siku ya Jumanne, mpaka leo ni wiki mzima imepita, waheshimiwa wetu wako hapa kwenye vikao muhimu tena busy kweli kweli, ili nasi kujichotea mawili matatu tunayayasikia hapa na pale na kuwatupia wananchi na members wenzetu hapa JF.
Mkuu wangu Mkandara,Pengine mimi ndio sielewi..
Hivi kosa la Pasco ni lipi hapa?..Kujiita yeye ni Political analyst kisha akamshambulia Dr.Slaa na Chadema ktk uchambuzi wake ambao wengi hatukubaliani!..Sasa kama hatuukubali kwa nini tusiandike ukweli wenyewe ni upi na kwa nini haikuwa hivyo badala yake tunamshambulia Pasco na utafiti wake binafsi hadi kumvika kofia za njano/kijani.
Pengine hata mimi sielewi siana za Bongo lakini kuna tofauti kubwa sana kati ya vyama vya Upinzani kushirikiana nje ya Bunge (coalition) na kuunda ushiurikiano huo ndani ya bunge. Na maadam Pasco kazungumzia ushirikiano wao ndani ya Bunge nadhani ni jukumu letu sisi kuelewa ushirikiano wa Upinzani ndani ya bunge unahitajika kwa sababu gani..
Marekani kumetokea kundi la mageuzi wanaojiita Tea party hawa wamekuwa sumu ndani ya chama chao wenyewe na pengine kulingana na siasa za Bongo hawa wangeitwa wasaliti na kunyang'anywa uanachama.
Lakini mbali na hivyo leo hii ndani ya bunge lao Republican wanajaribu kila hali kushirikiana na kundi hili ili kuunda umoja wa Upinzani ambao Republican hata pasipo kundi hili wanaweza kabisa kuendesha Upinzani ndani ya Bunge kwa sababu wao ni majority tena kukizidi hata chama tawala lakini maadam maswala yanayokuja bungeni yatakuwa na ushawishi mkubwa wa kuendeleza ya Obama na serikali yake, Republican wanataka kuongeza nguvu ya Upinzani zaidi kwa sababu ndani ya bunge wapo wabunge ambao ni swingers pia.
Hivyo leo Chadema ina wabunge wasiofika 50, kweli wamepata nguvu ya kuunda Upinzani lakini idadi hii haina nguvu ya ushindani bungeni ikiwa wao Chadema hawatafuti support ktk maswala muhimu ambayo wao watasimamia Bungeni iwe hata kubadilisha katiba ya nchi. Chadema kama chama wanatakiwa kutafuta support ya wabunge wengine kuhusiana na hoja zao lakini sio ushirikiano utakao waunganisha na kuwa chama kimoja.
CUF wameweza kufanikiwa ktk maswala kutokana na support ya Chadema nje na ndani ya BUnge blakini wameshindwa kulipa fadhala baada ya kupata wao. Hii ni desturi ya mswahili siku zote hulia shida kabla hajapata na akisha pata hukuacha solemba hadi siku zitakapo mwioshia ndipo huwatafuta marafiki zake. Hii ni Hulka yetu, hivyo tusiwalaumu CUF kwa yote waliokwisha Achieve kwani leo hii CUF wameweza kubadilisha katiba ya Muungano pasipo kupitishwa na bunge letu. wameweza kuunda serikali ya mseto kabla ya uchaguzi hivyo kuwafanya wao ni part of CCM na watatekeleza sera za CCM wakiwa CUF kiitikadi - Hatujayaona haya popote duniani lakini ndivyo ilivyokuwa na Chadema wamekaa kimyaa..
Pengine ukimya huu ndio ulomsukuma Pasco kuanza kuhoji uongozi wa Chadema, na pengine hata kuona ni udhaifu ktk siasa za Bongo lakini wakuu zangu ni vizuri sana kumwambia Pasco kile kilichofanyika na kwa sababu gani Chadema hawakufanya hivi ama vile kulingana na dhana yake. CUF kuungana na CCM haina maana Chadema wachoke kutafuta support yao ama ya vyama vingine kwa maslahi ya wananchi kwani tukitaka kuundwa kwa katiba mpya, ushirikiano wa wabunge wetu wa Upinzani hauwezi kuondoa ushirikiano baina ya CUF na CCM, au ushirikiano huo kuwaunganisha Chadema na CUF bali ni hoja yenyewe ndio inahitaji nguvu ya vyama hivyo vya Upinzani ili kuweza kusimama kwa maslahi ya Taifa... Na kama mlivyokwisha sema Bunge ni mhimili tofauti na ule wa serikali, waacheni CUF waungane na CCM ktk maswala ya kuunda serikali lakini tunapofika Bungeni, Upinzani unatafuta ushirikiano mwingine kabisa tofauti na ule wa kuunda serikali.
Mkandara,Kaa la Moto,
Kumbuka Chadema hawana ulazima wa kuunda baraza la mseto, wao ndio wameshika nafasi ya pili na wana uwezo wa kuunda chombo hicho kisheria pasipo kuwahitaji CUF, lakini pia ikiwa ahadi hizi za ushirikiano kulitangulia kabla ya Chadema kuchagua safu ya viongozi wa Upinzani bungeni basi tukubali tumeamua kufanya hivyo kwa sababu Chadema haiwahitaji CUF wala vyama vingine ktk kuhitaji kura zao ktk mapendekezo ya kambi hiyo ya Upinzani.
Kuna hatari ya maamuzi kama haya hasa inapoingia uhasama bungeni kiasi kwamba wabunge wakashindwa kufikiri na kutimiza yale wananchi tulowatuma bungeni.. Hizo siasa za maji taka zikaingia hadi bungeni tena upande wa Upinzani wakawaacha CCM wakipeta na kuchekelea, jambo ambalo athari yake itakuwa kubwa zaidi kwa wananchi ambao wanategemea mageuzi ya hata policies zilizokuwepo.
Ni zipi hizi kijana! maana hizi unazosema zilitanguliwa na zile siasa za ngangali. Kwa hiyo almost everything has got its starting point. Bila shaka na Chadema kitaeleweka. Don't worry!Jamani kinachoendelea ni kawaida ingawa kinachochewa sana na siasa za tuhuma na kudharauliana kati ya vyama hivi viwili kwa muda mrefu sasa. Hata 2005, CUF pia waliunda serikali pekee yao hadi baada ya wiki kadhaa ndipo wakaweza kuongea kistaarabu na kukubaliana kushirikiana na ndio maana Hamad akaendelea kuwa kiongozi wa upinzani na Dr Slaa kuwa naibu wake huku Halima Mdee akiwa Naibu Chief Whip.
Lakini ni kweli hali ya sasa ni tofauti kidogo kwani CUF wanamakubaliano ya siasa za kistaarabu na CCM na huku CHADEMA imeamua kuchukua siasa za ngangari hadi kieleweke.....
Lakini pia wakati CUF walikuwa na Hamad Rashid ambaye ilikuwa ni rahisi kufanya naye kazi kwa nianjema kabisa. CHADEMA wanaye Freeman Mbowe ambaye hulka yake sio ya ushirikiano na zaidi kumuamini ni vigumu.....Wakiweza kuyazungumza haya kwa uwazi na lile la CHADEMA kuwaona CUF ni Waislamuwaislamu na CUF kuwaona CHADEMA Wakristowakristo...ni wazi hekima zinaweza kushika hatamu na Watanzania wote wakafaidika na mafanikio ya vyama hivi na wenzao wa NCCR mageuzi
Izi hoja ni nzito kweli kweli, sijui ni Wa TZ. wangapi watakuwa na uwezo wa kuziaccess na kuzielewa. Ingawa watu wamehamasika sana na mambo ya kisiasa kwa sasa, uchache wa waliojitokeza kupiga kura unaonesha bado watu wengi hawataki kukubaliana na reality na wanaendelea kung'ang'ania emotions zao.
Hivyo nashawishika kuamini hata kama kitu hakina mantiki yoyote, kukifanyia kazi ni muhimu kama unataka kupata ushindi kwenye siasa za TZ sababu watu wengi hawana muda wa kufikiri au kusikiliza facts nzito zilizopo. Ni bora hoja za kwanini ni shida kuunganisha vyama vya upinzani au hata upinzani bungeni ziwekwe wazi kwa waTZ ili kufuta ile mentality ya kwamba watu ni wapinzani ni wabinafsi na hivyo hawana jipya katika matatizo kama ya ukosefu wa maadili.
Kweli Jamiiforums ni shule/chuo cha ukweli, nimekuwa nikijifunza na kupata habari nyingi sana humu, ila leo nimejifunza na kuelewa zaidi.
HONGERENI SANAAAA & keep it up.
HISIA KALI, kiukweli mimi ni just a layman, kwa hiyo nikiwa layman ndio nikose credibility ya kutoa maoni yangu au ushauri wa maana?.Sasa bwana mkubwa kama wewe ni layman unajiondolea mwenyewe credibility ya kutoa ushauri wa maana. Kwani ukisema tu wewe ni layman wale ambao wanaelewa zaidi wa mambo watakupuuza tu.