CCM ijibu hoja za CHADEMA - Sumaye

Huyu ni mmoja ya wale waliokubwa na Rungu la fitina la Mkwere 2015, alipigwa kijembe kuwa anamilik 25 bil. Lakin alichokisema huyu bwana ni chamsingi, km chadema wametoa hoja, wanapaswa kujibiwa kwa hoja, sio kulaumu, kunung'unika na kulalama pasipo sababu za msingi! Vitisho havitaweza kamwe kufuta hoja za CDM kwa wananchi bt zitakiua chama chao.
naamini hapo kwenye nyekudu uliimanisha 2005.
 
HOWARD,

Makamba hatakiwi kutoka hapo, ndiyo CDM wanapopandia chati kwa kauli za makamba. Wakikusikia mwishowe wanaweza kumtoa kweli halafu walete mtu mwenye akili. Mwache makamba akae hapo. Akistaafu wampe Tambwe Hizza. Safi kabisa
 
Sumaye amepiga msumari wa moto, maana nani atajibu hoja; Makamba! au Hiza? thubutu!! Hamna hoja pale akili zao zipo kuzimu.

Hata hivyo kasema chama kinapaswa kuwa na viongozi waadilifu naongezea "wenye uwezo wakufikiri na kutambua haraka", Myt:Sio kama yule Dada wa Arusha na Makamba.

Anachosema Sumaye ndicho kilipaswa kufanywa na CCM siyo vitisho na kutumia nguvu za Dola. Nashauri CCM waachie ngazi waondoke kwa Amani kama wanapenda sana Amani kama wanavyosema
 
Sunday, 06 March 2011 09:21

tluwaysumaye_thumb.jpg
Claud Mshana
WAKATI CCM ikitaka dola ikidhibiti Chadema, Waziri Mkuu wa Serikali ya Awamu ya tatu, Fredrick Sumaye, amekitaka chama hicho tawala kukabiliana na hoja za Chadema kisiasa badala ya kuiachia Serikali ipambane nao.Juzi CCM kilisema nyendo za Chadema zina agenda ya siri ya kuking’oa madarakani kwa kutumia nguvu kinyume cha katiba hivyo kiliitaka Serikali na vyombo vya dola kuchukua hatua za kisheria haraka.

“CCM inaviomba vyombo vya dola viwe imara kuchukua hatua za kisheria… Wanachofanya Chadema ni kutuchonganisha na wananchi, kutoa kauli hatari za kujaribu kughilibu akili za watu ili kuchochea machafuko, umwagaji wa damu na uasi. “Wanachochea wananchi wakisema, ‘peoples’ na hujibu ‘power’! (nguvu ya umma), Je mpo tayari kufanya kama Tunisia, Misri? (ambako serikali zilipinduliwa kwa nguvu ya umma)” alisema Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (Nec) ya CCM, Itikadi na Uenezi, John Chiligati kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika juzi, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na gazeti hili bila kujua kwamba CCM wangekuwa wanazungumzia suala hilo, Sumaye alisema CCM inatakiwa kukabiliana kisiasa na hoja za Chadema na si kuiachia Serikali ipambane nao.

Kwa mujibu wa Sumaye, kazi ya siasa ni ya chama na si serikali, hivyo CCM wanapaswa kuwa mstari wa mbele kupambana na Chadema kwa sera na kujibu hoja zao zote ili kuongeza imani ya wananchi kwa chama hicho.Sumaye alisema si ishara nzuri kwa CCM kukaa kimya wakati wapinzani wanaendelea kukishtaki kwa wananchi kuwa kimeshindwa kufanya kazi.

Sumaye ambaye Mwananchi Jumapili ilimtafuta kusikia maoni yake kuhusu mfululizo wa mikutano ya Chadema na mustakabali wa CCM, alisema chama hicho tawala kinapaswa kujibu hoja zote za Chadema kisiasa na kama hakina majibu kiiombe Serikali majibu hayo na iyatoe kwa wananchi.

“Wale (Chadema) wanafanya kazi za siasa na hawa (CCM) wamekaa kimya, wanaiachia Serikali ndio inatoa majibu, hali hiyo si nzuri, chama kinapaswa kujibu hoja zote na kama hakina majibu, kiombe kwa serikali,” alisema Sumaye.Mjadala wa uhalali wa mikutano na maandamano ya Chadema uliibuliwa na Rais Jakaya Kikwete alipolihutubia taifa kupitia radio na televisheni Februari 28, mwaka huu na kuwaleza wananchi kuwa chama hicho cha upinzani kina lengo la kuleta machafuko nchini.

Rais Kikwete alisema hayo alipokuwa akilihutubia taifa mwishoni mwa mwezi Februari mwaka huu.Kauli hiyo ya Rais Kikwete ambaye Chadema waliipuuza, ilisisitizwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mahusiano na Uratibu Steven Wassira, aliyesema kuwa Chadema wasije kuilaumu serikali ikikosa uvumulivu na kuanza kutumia dola kukishughulikia.

Akihojiwa na gazeti hili Sumaye hakuishia kuishauri CCM kuja na hoja za kisiasa kujibu mapigo ya Chadema, bali pia alieleza aina ya watu wanaofaa kukiongoza chama hicho tawala wakati huu wa mabadiliko makubwa ya kisiasa.Sumaye alisema CCM inahitaji viongozi waadilifu, wachapakazi na wasio waoga kumshauri rais ili kuwa na mabadiliko ya kiutendaji yanayoendana na joto la kisiasa lililopo. “Tunahitaji viongozi wasioogopa kumshauri rais juu ya masuala mbalimbali, kama utakuwa na viongozi waoga, lazima kutakuwa na matatizo,” alisema Sumaye.

Kuhusu mabadiliko ndani ya CCM ambayo Rais Kikwete alisema ni lazima yafanyike, Sumaye alisema anakubaliana msimamo huo na anampongeza Rais kwa kutambua kuwa chama kinahitaji mabadiliko makubwa ya kiutendaji.“Kwanza nampongeza Mwenyekiti, maana ameona hilo. Watu wengi wanaona kuna umuhimu chama kurekebishwa na eneo muhimu ni utendaji wa viongozi wa ngazi mbalimbali ndani ya chama,” alisema Sumaye.

Sumaye alieleza kuwa CCM kitaendelea kushika dola, lakini kama kinataka hayo yatimie, mabadiliko ndani ya chama ni muhimu.Alisema umuhimu wa CCM kujifanyia tathmini ya utendaji ulianza kujionyesha katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010, ambapo ikilinganishwa na chaguzi nyingine, chama kilipata upinzani mkali."Sasa ni dhahiri kunahitajika mikakati madhubuti ili kuhakikisha mwaka 2015 unakuwa mrahisi kwa CCM," alisema Sumaye.

Ndejembio atabiri anguko
Habel Chidawali anaripoti kutoka Dodoma kuwa, Kada maarufu wa CCM, Pancras Ndejembi amekitabiria chama hicho kikongwe kuzama.Kada huyo ambaye ni Mwenyekiti Mstaafu wa CCM Mkoa wa Dodoma alisema jana kuwa hali ilipofikia kwa sasa, CCM inaonekana kupoteza mwelekeo na kutia shaka mustakbali wa chama hicho siku za usoni.

Ndejembi ambaye aliwahi kutumikia nyadhifa mbalimbali ndani ya serikali na chama katika utawala wa Serikali ya awamu ya kwanza, alisema CCM bado haijaingia shimoni ila inaelekea huko.“Ni kweli chama hakifuati utaratibu uliokuwepo ndio maana nasema kuwa kinaelekea kuzama tofauti kabisa na enzi zetu ambapo Mwalimu Julius Nyerere alikuwa anasisitiza kuwa turudi kwa wanachama tukae nao na kuzungumza, jambo ambalo sasa hilo halipo na viongozi wamebaki huko juu,” alisema Ndejembi.

Alisema viongozi wa ngazi ya taifa wamebaki katika maofisi yao na kushindwa kurudi katika ngazi za chini kuimarisha chama na matokeo yake wanaishia kupiga kelele bila ya kuwa na uhakika wanachama ngazi ya chini wanataka nini.Ndejembi hivi alisema hakuna mshikamano wa dhati ndani ya chama jambo linalowafanya wanachama kumuachia mzigo wote Mwenyekiti wa Taifa.

“Watu wanaishia kulaumiana kila kona kwamba chama kimefanya nini, mara wanasema bado kimesimama wengine wanasema kuwa kinayumba, ila ukweli utabaki palepale kuwa CCM tunazama sasa,” alisisitiza.Kuhusu nguvu ya wazee ndani ya Chama Ndejembi alisema: “Sisi tumestaafu hivyo tupo tupo na kama hawataki kutuita unadhani tutakwenda ? Lakini, wakisema tuende tuko tayari kukaa pamoja nao kutengeneza utaratibu wa kukinusuru chama kisizame kabisa katika tope”.Ushauri

Kuhusu nini kifanye ili kukinusufu CCM, alisema unahitajika mshikamano wa dhati kati ya viongozi na wanachama: “viongozi wanahitaji kutambua kwa dhati kuwa chama kiko ngazi ya chini kuanzia kwa wajumbe wa nyumba kumi sio ngazi ya mikoa”.Alishauri kuwa Mwenyekiti wa CCM Taifa anatakiwa abaki kama kiongozi wa kutoa ushauri kwa juu, lakini awe na watu wanaochukua mawazo kutoka kwa wanachama wa ngazi ya chini.

Hata hivyo, alisema viongozi wa taifa bado wana mfumo mbovu wa mawasiliano, kwani kila mtu katika nafasi ya juu ni msemaji, jambo linalofanya wajichanganye katika taarifa zao.
 
''Sumaye alisema CCM inahitaji viongozi waadilifu, wachapakazi, na wasio waoga kumshauri rais juu ya masuala mbalimbali ili kuuwa na mabadiliko ya kiutendaji yanayoendana na joto la kisiasa lililopo.''

Nimesoma hoja ya mheshimiwa SUMAYE,NAMHESHIMU SANA TENA SANA.NINACHOTAKA KUSEMA HAPA NI HOJA YA MSINGI KWAMBA SUMAYE NI MJUMBE WA HALMASHAURI KUU YA CCM AMABAYO KWA MUJIBU WA KATIBA YA CCM HALMASHAURI KUU NDIYO CHOMBA KIKUU CHENYE MAAMUZI JUU YA MUSTAKABALI WA KISIASA NA HATA UCHUMI KWENYE CHAMA TAWALA,ANAPOSEMA CCM WAJIBI HOJA YEYE ANAJITOA? ATWAMBIE KAMA YEYE NI CHADEMA AU CUF TUJUE MAPEMA. BILA SHAKA WATANZANIA WOTE WANAJUA KWAMABA UOZO WA MAADILI UMETOKEA KATIKA SERIKALI YA MKAPA NA SUMAYE ALIKUWA KIONGOZI MKUU WA SERIKALAI,NANI HAJUI MIKATABA YOTE MIBOVU ILIANZIA KWA SUMAYE NA MKAPA NA KWAMBA SERIKALI YA SASA INABEBA MAKOSA YAO?YEYE NA WENZAKE NDO WALIOINGIA MIKATABA YA KUUZA KILA KITU MPAKA NYUMBA ZA WATUMISHI NA LEO WANAISHI HOTEL ! UADILIFU WA SUMAYE UKO WAPI? ONDOA BORITI JICHONI KWAKO KABLA HUJAONA LA MWENZAKO.
 
sisiemu wanadhani kuwa amani inajengwa kwa ujinga wa wananchi, sasa wanatakiwa kuwa na ufahamu kuwa wananchi wamesha elimika na kufahamu kuwa wananchi tumaechoshwa na kupuuzwa kwa matakwa yetu na punde tu hatutahitaji hata cdm kufanya wanayo yahofia yaani mandamano yasiyo na kikomo mpaka wamestep out na siyo down.
 
haata dola walishawachoka ila wanatimiza tu wajibu, kwani unadhani wenyewe hawana ndugu,jamaa na marafiki??
kwani unadhani wenyewe hawayaoni maisha yalivyo??
Binafsi nina wachukia polisi vibaya sana, lakini jana wamenifanya nifikilie upya baada ya kumkuta polisi mmoja tena huku akiwa ameva sare akiponda wazi wazi serikali ya CCM, na kuwalaumu viongozi wake wajuu kwa maamzi yao ya kishabiki/kipenzi zaidi kwani yawana wasababisha wawe na uadui na wakazi wa Arusha.
 
ccm is dead tunaongozwa na serikaki mfu! serikali inashindwa kukamata wezi wa ma bilioni eti inawapa siku warudishe pesa walizokwiba kweli huo ndo uadilifu kweli? no wonder hata shirika la ndege linatushinda kuendesha soon tutafanya arobaini ya ccm. chadema hoyeee!!!
 
hoja ujibiwa kwa hoja na si mabomu risas na virungu naomba huyu bwana aonyeshe njia kwa mkwere aache taarab ajib hoja
 
Ni sawa na kumpa mtoto wa chekechea afanye quiz ya form four.
Kigoma kuwa Dubai; sidhani kama kuna mtu wa CCM mwenye ujasiri wa kuwaambia wananchi raisi kadanganya
 
''Sumaye alisema CCM inahitaji viongozi waadilifu, wachapakazi, na wasio waoga kumshauri rais juu ya masuala mbalimbali ili kuuwa na mabadiliko ya kiutendaji yanayoendana na joto la kisiasa lililopo.''

Nimesoma hoja ya mheshimiwa SUMAYE,NAMHESHIMU SANA TENA SANA.NINACHOTAKA KUSEMA HAPA NI HOJA YA MSINGI KWAMBA SUMAYE NI MJUMBE WA HALMASHAURI KUU YA CCM AMABAYO KWA MUJIBU WA KATIBA YA CCM HALMASHAURI KUU NDIYO CHOMBA KIKUU CHENYE MAAMUZI JUU YA MUSTAKABALI WA KISIASA NA HATA UCHUMI KWENYE CHAMA TAWALA,ANAPOSEMA CCM WAJIBI HOJA YEYE ANAJITOA? ATWAMBIE KAMA YEYE NI CHADEMA AU CUF TUJUE MAPEMA. BILA SHAKA WATANZANIA WOTE WANAJUA KWAMABA UOZO WA MAADILI UMETOKEA KATIKA SERIKALI YA MKAPA NA SUMAYE ALIKUWA KIONGOZI MKUU WA SERIKALAI,NANI HAJUI MIKATABA YOTE MIBOVU ILIANZIA KWA SUMAYE NA MKAPA NA KWAMBA SERIKALI YA SASA INABEBA MAKOSA YAO?YEYE NA WENZAKE NDO WALIOINGIA MIKATABA YA KUUZA KILA KITU MPAKA NYUMBA ZA WATUMISHI NA LEO WANAISHI HOTEL ! UADILIFU WA SUMAYE UKO WAPI? ONDOA BORITI JICHONI KWAKO KABLA HUJAONA LA MWENZAKO.

Toa ushahidi wa maneno yako dhidi ya Sumaye, pia husitumie methali za Biblia kama Makamba kinyume na dhamira ya maandiko yenye, husidhani Watanzania wote ni wajinga kupumbazwa kirahisi kama unavyotaka kufanya; hii thread ina tumia maneno ya Sumaye kuhoji uhalali wa Serikali kutoa vitisho kwa CDM badala ya kujibu hoja za CDM, kama unadhani Sumaye aliingia mikataba mibovu kwahiyo hasiongelee uozo wa hii Serikali na CCM ya Kikwete anzisha hiyo thread tutakujibu hapa toa hoja juu ya thread husika.

Au wewe ndio Makamba, maana unakuja na staili hiyo hiyo ya kutokujibu hoja na kutumia vitisho kwa Sumaye; Pole sana.
 
Viongozi wa serikali na chama tawala, naona busara zimewapungua, wanatumia pesa na nyadhifa kama busara, ndo maana tunahitaji katiba mpya ambayo viongozi wa serikali watakuwa na displine katika utendaji wao, mimi na wananchi wenzangu ambao tunateseka na hali ngumu ya maisha, tunatoa tamko, kuwa viongozi wa serikali wajue mipaka yao katika kutoa tamko, vile vile viongozi wa vyama wajue mipaka yao, hivi tendwa wewe ni mwanasiasa! nakuuliza? we Chiligati bei za bidhaa zimepanda au bado chiligati nakuuliza, wananchi wanahali ngumu ya maisha au hawana nataka majibu enyi viongozi wa serikali mabao mmeamua kuwanyongea baharini wa piga kuwa wenu bila kuwa kumbuka hata kwa maji ya kunywa, hivi lengo lenu nini TUfe?? maana hawa wanaotutetea hamtaki hata kuwa ona, na ninyi hamtakikutusaidia, sasa tunasema hivi! FUTENI HIYO CHADEMA HALAFU TUONE KIFUATACHO, NA WEWE TENDWA NAKUONYA USITUMIWE NA WANASIASA KUWA NA BUSARA, sisi ndo nguvu ya umma tutakufikisha pabaya. am seriouse,
 
Kinachoendelea sasa ni utata wa kimfumo na kiuendeshaji ambao CCM inakumbana nao baada ya kushindwa kujifanyia mabadiriko ya kweli ya ndani kutokana na kutopenda kuendana na hali halisi. CCM sasa hivi bado kinaendeshwa kama chama cha kikomunisti ambacho serikali huchukuliwa kama wakala wa chama na chama na serikali havitenganishiki. Angalia hali ilivyo katika nchi zote za kikomunisti, huwezi kutofautisha kati ya chama na dola.

Mfumo tuliouchukua ni mfumo wa kibepari, mfumo wa vyama vingi, mfumo ambao hutaka kutenganishwa kwa shughuli za serikali na shughuli za chama. Huo mfumo tumeuchukua, lakini CCM bado haijauchukua mfumo huo na kuutafsiri kimuundo na kiutendaji. CCM imeshindwa kujibadili kwenda na mabadiriko yaliyo tokea.

Matokeo yake CCM imeishiwa na "resources" kwani wanaharakati wengi na watendaji wa chama wote wamejazana serikalini. CCM imebaki kama mtoto yatima asiye na mwenyewe. Wanarakati wa CCM ambao ilitakiwa wajibu hoja za Chadema wote wako serikalini na ni sehemu ya serikali. Ni wakati gani watafanya kazi za chama, ambazo kwa uasili wake ni kazi za kujitolea zaidi, au kufanya kazi za serikali? Serikalini kuna maslahi na ndo kwenye resources zote. Kwa hiyo ni rahisi kwa watu wengi wa CCM kukimbilia serikalini huku wakivaa kofia mbili mbili, yaani za kichama na za kiutendaji serikalini. Katika hali hii panapoumia ni kwenye chama!

Anachokisema Sumaye ni halali kuwa hoja za Chadema inatakiwa zijibiwe na wanasiasa ndani ya CCM. Tatizo wanasiasa wote ndani ya CCM wako serikalini kutokana na tatizo la kimfumo nililoeleza hapo juu. Sasa wakiongea ni vigumu kutofautisha kauli zao kama wanasiasa au watendaji wa serkali. Kwa hali kama hii inakuwa ni vigumu kushindana na Chadema chenye wanasiasa full time ambao masaa yote wanafikiria na kufanya siasa.

Hapo ndo mahali CCM ilipo na isipoangalia itapoteza zaidi kwenye uwanja wa siasa na matokeo yake itakuwa ni kufurushwa ndani ya serikali vile vile. CCM inatakiwa wajibadili kimfumo ili kutofautisha chama na serikali. Na hili tatizo la watendaji wengi wa chama kukimbilia serikalini inatakiwa walifanyie kazi. Wabaki na watendaji wa chama ambao hawako serikalini. Sasa hivi kina Tendwa wakiongea kukitetea chama, kuna ukakasi unaonekana wazi kwa sababu hawa ni watendaji ndani ya dola. Wataonekana wanakitetea chama kwa kutumia dola. Inatakiwa watu kama kina Tendwa waende wakapewe ofisi chamani ili nao kazi zao iwe ni kupambana na kina Slaa. Vinginevyo mambo yatakuwa mabaya!

Kwa hiyo, kauli za Sumaye kuwa chama ndo kiijibu Chadema ni kauli halali kabisa na ndio inavyotakiwa iwe. Lakini Chama kina wanasiasa gani tena? Hamna! Resorces zote za maana ziko serikalini, kwa hiyo ndo maana chama kinakimbilia kuomba msaada wa dola. Kwa CCM dola ni sehemu ya chama! Na hili halifai!
 
Angekuwepo Phillip Mangula kama katibi mkuu ya ccm yeye alikuwa na uwezo wa kujibu hoja lakini huyu father X-Mas, Makamba uwezo alionao ni wa uvuvuzela tu!!
 
Subiri watakavyomjibu sumaye badala hoja za chadema ndio uje ccm ya mipasho badala hoja na sera
Sure Mkuu!
Sumaye ataambiwa kuwa hayo ni mnafiki, na kwamba hayo maoni yake binafsi, na watahoji kwanini asikisaidie chama akiwa serikalini, kama anavyodai ifanyike sasa!
CCm imejaa vipofu, ambapo hawawezi kuongozana sasa!
Wanapewa hoja, wanajibu kashfa!...too awkward!
 
''Sumaye alisema CCM inahitaji viongozi waadilifu, wachapakazi, na wasio waoga kumshauri rais juu ya masuala mbalimbali ili kuuwa na mabadiliko ya kiutendaji yanayoendana na joto la kisiasa lililopo.''

Nimesoma hoja ya mheshimiwa SUMAYE,NAMHESHIMU SANA TENA SANA.NINACHOTAKA KUSEMA HAPA NI HOJA YA MSINGI KWAMBA SUMAYE NI MJUMBE WA HALMASHAURI KUU YA CCM AMABAYO KWA MUJIBU WA KATIBA YA CCM HALMASHAURI KUU NDIYO CHOMBA KIKUU CHENYE MAAMUZI JUU YA MUSTAKABALI WA KISIASA NA HATA UCHUMI KWENYE CHAMA TAWALA,ANAPOSEMA CCM WAJIBI HOJA YEYE ANAJITOA? ATWAMBIE KAMA YEYE NI CHADEMA AU CUF TUJUE MAPEMA. BILA SHAKA WATANZANIA WOTE WANAJUA KWAMABA UOZO WA MAADILI UMETOKEA KATIKA SERIKALI YA MKAPA NA SUMAYE ALIKUWA KIONGOZI MKUU WA SERIKALAI,NANI HAJUI MIKATABA YOTE MIBOVU ILIANZIA KWA SUMAYE NA MKAPA NA KWAMBA SERIKALI YA SASA INABEBA MAKOSA YAO?YEYE NA WENZAKE NDO WALIOINGIA MIKATABA YA KUUZA KILA KITU MPAKA NYUMBA ZA WATUMISHI NA LEO WANAISHI HOTEL ! UADILIFU WA SUMAYE UKO WAPI? ONDOA BORITI JICHONI KWAKO KABLA HUJAONA LA MWENZAKO.

Lakini mkuu hivi ukiwa mwovu huruhusiwi kukemea maovu? Nadhani alichosema Sumaye ni sawa hata kama ni kwa unafiki.
 
The steps to take on difending oneself is to be i a right stensil. Sasa ccm inahitaji kusafisha nyumba ili iweze kujibu hoja. Hizi hoja ni rahisi kujibika, lakini kama akina EL na RA na wenzao bado wapo ndani ya uongozi hazijibiki. Chama chochote kile duniani kikikaa mbali na watu kitaangushwa na ni vigumu sana kurudi madarakani (Haki na Watu by JKN):decision:
 
Huyu ni mmoja ya wale waliokubwa na Rungu la fitina la Mkwere 2015, alipigwa kijembe kuwa anamilik 25 bil. Lakin alichokisema huyu bwana ni chamsingi, km chadema wametoa hoja, wanapaswa kujibiwa kwa hoja, sio kulaumu, kunung'unika na kulalama pasipo sababu za msingi! Vitisho havitaweza kamwe kufuta hoja za CDM kwa wananchi bt zitakiua chama chao.

Ni vizuri ikaeleweka kua kupanda kwa bei ya mafuta kumesababisha mfumoko wa bei sio Tanzania tu bali ulimwenguni kote. Nilichokifahamu ni kua CCM ilijibu hoja in general not in detailes pale waliposema "Kila chama kilitaja mambo yake kwenye campain lakin wananchi wakachagua CCM, sasa iweje baada ya miezi mitatu unataja tena hoja zilezile. Swali kubwa linalojitokeza ni kua nini wantegemea kuachieve ktk nchi ambayo rais amechaguliwa kidemocracia.

Kesi ya Tanzania in terms of polilitical point of view ni tofauti sana na LIbya, Misri na nchi nyingine ambapo marais waligeuka kua madikteta. Ni vizuri ikafahamika kua kua mabadiliko yoyote makubwa ya kisiasa yanaweza kutokea uchaguzi unaokuja kwakua hata kama serikali iliyopo ikiondolewa kimabavu, watakaoiondoa watakosa support ya International community kwa kua watakua hawana legitimacy ya kuongoza. No sio ktk karne hii tulionayo
 
Lakini sijui kwa nini serikali na sisiem wanataharuki. Mbona CDM walifanya hivyo hata 2005. Baada ya bajeti ya kwanza ya Mkwere, CDM walizunguka nchi nzima kuwaambia wananchi kuwa ile bajeti ilikuwa ni ya kufunga mkanda. Tunakumbuka pale napo walitikisa. Mawaziri ndiyo walizunguka tena maeneo mbalimbali ya nchi kuwaambia wananchi kuwa ile bajeti ilikuwa ya maisha bora kwa kila mtz. Mwaka huu wameshindwa kujibu hoja wanaanza kuzua suala la uchochezi. Mhariri wa gazeti la mwananchi ndiye amewaambia kweli. kwamba wananchi ndiye wataamua ni nani kati ya CDM, sisiem na gvt anayesema ukwelli.
 
Back
Top Bottom