Nilikuwa nafikiria namna nyingine ya kutatua mgogoro uliopo sasa hivi kati ya CCM na CHADEMA kuhusu suala la matokeo ya Urais. Nimefikiria kuna kesi mbili ambazo nikiwasikiliza CCM na wale wenye kulaani kitendo cha "kutoka nje" kilichofanywa na CHADEMA wanaweza kuja nazo.
1. Kesi ya Kikatiba ya kuwalazimisha CHADEMA kumtambua Rais Kikwete kwa vile waliamua kutoka wakati Rais ambaye ni Amiri Jeshi Mkuu na Mkuu wa serikali ya JMT alipokuwa anazungumza. Kwa vile kitendo kile kimeelezewa na Kapt. Chiligati kuwa kilikuwa kinavunja Katiba basi mantiki inataka wale wanaotetea Katiba wachukue hatua za kuitetea Katiba hiyo kwa kufungua kesi ya Kikatiba dhidi ya CHADEMA.
2. Kesi ya pili nayo ni ya Kikatiba vile vile nayo iwe ni ya kulazimisha CHADEMA WATAMBUE matokeo ya Uchaguzi wa Rais kwani kutokutambua matokeo ya kura za Urais yanatuleta kwenye tatizo la kwanza hapo juu. Kwa vile CCM na wengine wanaamini kuwa kura zilizopigwa na kutangazwa zilikuwa ni halali na hakuna mashaka yoyote basi jawabu pekee ni kuwalazimisha CHADEMA KUKUBALI matokeo hayo. Katiba inazuia kuhoji kutangazwa kwa Rais lakini HAKUZUII kutetea kutangazwa huko mahakamani! Hivyo, CCM na wanasheria wake wafikirie namna ya kuthibitisha au kuutetea ushindi mahakamani. Hapa napendekeza wao CCM waitishe kura zote za Urais kutoka majimbo yote ili kuonesha kiasi cha kura alizoshinda. Watakapofanya hivyo watafunga kelele zote za Chadema na kuwaridhisha Watanzania kuwa hakuna kura zilizochakachuliwa. Hapa itakuwa ni goli kama la Maradona au lile goli la elfu moja la Pele.
Kwa ufupi naamini CCM wanaweza kutoa mfano wa utawala wa sheria kwa kwenda mahakamani kufungua kesi hizo za Kikatiba.
Umelewa pingu!!!!Tatizo Mzee Mwanakijiji.................Mahakama hazina mamlaka ya kisheria kuingilia majukumu ya NEC yakiwemo kumtangaza Raisi aliyeshinda.........hivyo kwa mantiki hiyo mahakama haiwezi kupokea migogoro itokanayo na maamuzi ya NEC yawe ni kutambua au hata kutotambua maamuzi ya NEC kuhusiana na uraisi............................kwa hiyo hayo yote uliyoyandika hapo juu hayatekelezeki kwa maana ya kisheria...................................
lakini ipo sababu nyingine kwa nini CCM haina sababu ya kuumiza kichwa na kelele za Chadema...........................ni kuwa Chadema wamkubali au wamkatae JK bila ya kwenda mahakamani ni sawsawa kabisa na kutwanga maji kwenye kinu.............................CCM wao watakaa kimya na kuvuta pumzi tu hawana jingine la kufanya................................
Chadema kama wana ushahidi wa kuwa NEC ilikiuka taratibu za kisheria katika kumtangaza JK na ushahidi wanao basi itabidi watinge mahakamani na vinginevyo hizo purukshani nyingine ni ubabaishaji tu...mwaka 1995 mahakama hiyo hiyo ilikwisha sema pamoja na Ibara ya katiba inayokataza kuchunguza matokeo yaliyotangazwa na NEC lakini mahakama yaweza kuichunguza NEC kama ilifuata sheria katika kumtangaza aliyeshinda Uraisi................
Naomba tuungane kutaka CCM ifungue kesi ya kuwalazimisha CHADEMA kutambua matokeo.. na kumtambua Kikwete.. lets join hands wale wote tunaotaka utawala wa sheria na ambao tunaamini kitendo cha Chadema kutoka Bungeni hakikuwa sahihi..
Mada haijaenda shule
Nilikuwa nafikiria namna nyingine ya kutatua mgogoro uliopo sasa hivi kati ya CCM na CHADEMA kuhusu suala la matokeo ya Urais. Nimefikiria kuna kesi mbili ambazo nikiwasikiliza CCM na wale wenye kulaani kitendo cha "kutoka nje" kilichofanywa na CHADEMA wanaweza kuja nazo.
1. Kesi ya Kikatiba ya kuwalazimisha CHADEMA kumtambua Rais Kikwete kwa vile waliamua kutoka wakati Rais ambaye ni Amiri Jeshi Mkuu na Mkuu wa serikali ya JMT alipokuwa anazungumza. Kwa vile kitendo kile kimeelezewa na Kapt. Chiligati kuwa kilikuwa kinavunja Katiba basi mantiki inataka wale wanaotetea Katiba wachukue hatua za kuitetea Katiba hiyo kwa kufungua kesi ya Kikatiba dhidi ya CHADEMA.
2. Kesi ya pili nayo ni ya Kikatiba vile vile nayo iwe ni ya kulazimisha CHADEMA WATAMBUE matokeo ya Uchaguzi wa Rais kwani kutokutambua matokeo ya kura za Urais yanatuleta kwenye tatizo la kwanza hapo juu. Kwa vile CCM na wengine wanaamini kuwa kura zilizopigwa na kutangazwa zilikuwa ni halali na hakuna mashaka yoyote basi jawabu pekee ni kuwalazimisha CHADEMA KUKUBALI matokeo hayo. Katiba inazuia kuhoji kutangazwa kwa Rais lakini HAKUZUII kutetea kutangazwa huko mahakamani! Hivyo, CCM na wanasheria wake wafikirie namna ya kuthibitisha au kuutetea ushindi mahakamani. Hapa napendekeza wao CCM waitishe kura zote za Urais kutoka majimbo yote ili kuonesha kiasi cha kura alizoshinda. Watakapofanya hivyo watafunga kelele zote za Chadema na kuwaridhisha Watanzania kuwa hakuna kura zilizochakachuliwa. Hapa itakuwa ni goli kama la Maradona au lile goli la elfu moja la Pele.
Kwa ufupi naamini CCM wanaweza kutoa mfano wa utawala wa sheria kwa kwenda mahakamani kufungua kesi hizo za Kikatiba.
Kwani kutambua matokeo lazima ?
Hakuna Kesi Hapo na Hata hao CCM wanajua na wala vichwa haviwagongi.Kwani hii ni nusu mchezo CUF Waliweka full nondo na mwisho wa yote walisalimu amri.Kama CDM Wanafikiri katiba mpya italetwa kwa Drama za unaharakati wanapoteza wakati wakae chini na wazumgumze kwa kuwakilisha hoja na kufanya ushawishi wa kihoja ili hoja zao zikubalike iwe kitaifa kwa kutumia vyombo husika au kimataifa kwa kutumia jumuiya za kimataifa.Vinginevyo CCM Wanawalia timing tu....................!Naomba tuungane kutaka CCM ifungue kesi ya kuwalazimisha CHADEMA kutambua matokeo.. na kumtambua Kikwete.. lets join hands wale wote tunaotaka utawala wa sheria na ambao tunaamini kitendo cha Chadema kutoka Bungeni hakikuwa sahihi..
Mada haijaenda shule