CCM Houston Ndani ya Radio Mbao!

Jazzie

Member
Jan 30, 2008
73
35
KOMBOLELA SHOW JUMAMOSI HII January 8, 2011 @ 01:00pm - 02:00pm EST, 9:00pm -10:00pm East African Time

Kama wewe ni mfuatiliaji wa mambo ya kisiasa, mojawapo wa mambo yametokea siku za karibuni ni uanzishaji wa matawi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) nje ya mipaka ya Tanzania kama vile India, Uingereza, n.k. Kujiunga na chama chochote ni haki ya kikatiba ya kila Mtanzania, kwa hiyo uanzishaji wa matawi ya chama chote chote cha siasa nje ya Tanzania sio kosa, hasa uanzishaji wa matawi unapokuwa hauvunji sheria ya nchi hizo za nje.

Tatizo, pengine ni hisia kwamba waanzishaji haya matawi ya chama nchi za nje, hasa ya CCM, ni wasaliti wa watanzania wengi ambao ni masikini. Hilo linatokana na matarajio kwamba Mtanzania ambaye amefanikiwa kutoka nje ya nchi amepanuka kimtazamo na kwamba mtu ambaye amepanuka kimtazamo na ana ujasiri, hawezi kukiunga mkono CCM, chama ambao kimekuwa madarakani muda mrefu bila kuleta maendeleo ya kweli kwa mtanzania masikini.

Radio Mbao kupitia Kombolela Show itakuwa na mahojiano na Michael Ndejembi ambaye ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) tawi la Houston, Texas ili kufahamu mtazamo wake juu ya uanzishaji wa matawi ya CCM nchi za nje.

Jiunge nasi kwa kupitia hapa: Radio Mbao ili usikose uhondo!
 
Lazima CCM iwe na tawi CCM si ndio kule Richmond ilipoanzia.
 
Walaaniwe wote wanaotumia nyazifa za wazazi wao...kudidimiza wapigania wanyonge. Ipo siku hao wanaodai kuanzisha matawi ya vyama.... Laana hizi za wanyonge zitawashukia...
 
Unajua kaka inabdi uelewe kuwa elimu wakati mwingine haimsadii mtu ina inamfanya kuwa na kiburi.Tena hasa walio nje ya nchi ndo akili zao hazisumbuki kabisa hata kuwaza jinsi ndugu zao wanavyohangaika ntymbani.Akili zao zote ni kusaka uraia wa nje kwa kuamini walipo ndo mwisho wa Dunia.Wasomi wengi ndo wametufikisha pabaya hapa tulipo kama hujui!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom