Elections 2010 CCM hii kiboko !

chama

JF-Expert Member
Aug 6, 2010
8,001
2,418
Bado naikumbuka ccm ya Mwl. Nyerere; wakati ule chama kilikuwa na maadili na miiko ya uongozi. Chama hakikuwa sahihi 100% lakini angalau kilikuwa kikimjali kila mtanzania. Wengi tulitegemea ccm kingemuendeleza mtanzania hasa kwenye kipindi hiki cha vyama vingi, leo hii chama kimegeuka kama club ya wahuni watupu, viongozi tulio nao wapo mstari wa mbele kwenye kuliangamiza taifa letu, kila kukicha kashfa, sijui ni kiongozi yupi kumuamini; cha ajabu viongozi hao wamekuwa mstari wa mbele kukanusha hata mambo ambayo ni dhahiri, hebu wana ccm tuliangalie hili jipya la Bw. Kinana, maishani mwangu sijasikia hata siku moja mchaga wala muhaya wakawinda tembo, siku zote wawindaji haramu ni wasomali haya unganisha hesabu hapo, wawindaji haramu wasomali, Kinana msomali halafu mtu Kinana leo hii anakataa kwamba hajui mzigo aliokuwa anasafirisha? Kweli watanzania tumekuwa mbumbu lakini haya mengine hebu tuyaangalie kwa makini nadhani wakati ccm tumekuwa mstari wa mbele kuwa wapinzani yupi ni raia au si raia hebu tujichunguze wenyewe kwa maslahi ya taifa letu.
 
Nyerere alikuwa na nafasi ya kubweteka maana kwanza ilikuwa chama shika adabu ops hatamu hakuna upinzani na ukileta fyoko unatoswa baharini na jiwe shingoni.
lakini aliweka mbele TANZANIA na watanzania ili waweze kujikwamua na kusonga mbele
ila ccm hii ya sasa wanakoroma na shibe ya matunda ya uhuru huku wakiendelea kupopoa mwembe uliomaliza msimu wake
 
Back
Top Bottom