CCM hawakuhitaji kura za wafanyakazi kushinda 2010 na hawazihitaji 2015

Ntemi Kazwile

JF-Expert Member
May 14, 2010
2,182
307
Kupitishwa kwa Sheria ya mafao ya uzeeni inayozuia wafanyakazi kulipwa withdrawal imedhihirisha kuwa CCM si chama cha wafanyakazi na wakulima bali cha wafanyakazi, kingekuwa cha wafanyakazi kingeheshimu matakwa ya wafanyakazi.

Mh Kikwete aliwahi kusema kuwa hata kama wafanyakazi wasipompatia kura bado atakuwa rais na ilikuwa hivyo, kwa kupitisha sheria hii mpya wanatudhihirishia kuwa hawahitaji kura za wafanyakazi 2015.

Binafsi nadhani kuzuia withdrawal itawanufaisha wafanyakazi wa mifuko hii ya pension na wanasiasa (watawala) zaidi kuliko wafanyakazi. Ingekuwa hii mifuko ipo kwa ajiri ya wafanyakazi basi menejiment yake ingekuwa inawajibika moja kwa moja kwa wafanyakazi na wafanyakazi kupitia vyama vyao ndio wangekuwa waajiri wa wafanyakazi wa mifuko si vinginevyo.

Hii ni miongoni mwa sheria feki zilizowahi kupitishwa na bunge letu dhwaifu
 
Back
Top Bottom