sulphadoxine
JF-Expert Member
- Nov 1, 2010
- 2,257
- 644
Waandaa kuleta vurugu kikao kijacho cha NEC. Wala njama kuzuia wafadhili wao wasing'olewe
BAADHI ya wenyeviti wa mikoa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wamepanga kuleta vurugu kubwa kwenye kikao cha mwezi ujao cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya chama hicho (NEC) ili kuzuia Waziri Mkuu wa zamani aliyejiuzulu kwa kashfa ya Richmond, Edward Lowassa, pamoja na waziri wa zamani, Andrew Chenge, wasing'olewe kwenye chama.
Wenyeviti hao wa CCM na wajumbe wengine wa NEC wamepangwa kusimama kwenye kikao hicho cha Septemba na kupingana na uamuzi wa chama hicho wa kuwataka wanasiasa wenye tuhuma za ufisadi kujiuzulu wao wenyewe kwenye nafasi za uongozi kabla ya kusubiri kufukuzwa.
Kundi hilo la wajumbe wa NEC, wakiwemo wengine kutoka Tanzania bara na Zanzibar, limepangwa ili kujaribu kuleta mapinduzi haramu ndani ya chama katika jitihada za kuzuia wanasiasa hao wasifukuzwe.
Genge hili la wajumbe wa NEC limeapa kuwa haliko tayari hata kidogo kuona "wafadhili" wao wanatimuliwa kwenye chama.