CCM hata wakiweka ng'ombe, aweza kushinda!

Saint Ivuga

JF-Expert Member
Aug 21, 2008
54,363
58,385
KWA wiki kadhaa sasa nimejaribu kudadisi mambo kadhaa ambayo yamekuwa yakitokea ndani ya Chama Cha Mapinduzi na jinsi yanavyoathiri mustakabali wa demokrasia nchini.

Kuna wakati nilifanya hitimisho gumu ambalo baadhi ya wasomaji hawakulipenda. Kwamba CCM, ambacho kimekuwa kama kokoro, kitaendelea kukaa madarakani kwa muda mrefu tu.

Nikasema sababu moja kubwa ni kwamba CCM ni Chama dola na hivyo kila anayetaka kufanikiwa – haswa kibiashara na kimaslahi – ni lazima ajiunge au ajihusishe nacho. Na kwa mantiki hiyo, CCM kinakuwa na watu wenye fedha zaidi za kukisaidia kushinda uchaguzi.

Pili, nilisema CCM kimekuwapo miaka mingi na kina mali nyingi ambazo zilichangiwa na Watanzania wote kwa ujumla. Kinapata ruzuku kubwa mno ikilinganishwa na vyama vingine vya siasa. Kina mtandao wa ofisi nchi nzima katika kila kijiji na kitongoji.

Tatu, wapiga kura wengi ni watu wasiotaka shida. Wengi wamepigika lakini wasingependa kujisumbua sana. Halafu ni watu wenye shukrani. Wakipewa fulana au kanga au sukari kilo tano au wakanunuliwa pombe, wanashukuru kila siku kwa muda wa miaka mitano. Na bado wapo wapiga kura ambao wakienda kupiga kura wao huuliza ni kipi chama cha Mwalimu Nyerere?

Wasiwasi tu ni kwamba kadiri miaka inavyosogea wapiga kura wa aina hii – wanaoulizia chama cha Nyerere – wanazeeka na kupungua. Lakini wapigakura wa kuuliza: "Yule katoa nini hata tumchague?" hao bado wataendelea kuongezeka.

Na madhali wanauliza 'yule katoa nini' na siyo: "yule ni nani na anatuambia anaamini katika nini?", basi, CCM wataendelea kutawala hata kama wakiwaweka ng'ombe kama wagombea katika nafasi mbalimbali, ikiwamo ya urais wa nchi.

Leo ningependa kuupeleka udadisi wangu mbali kidogo. Na ninaanzia na hilo la wapiga kura wetu na maswali wanayouliza. Kwamba badala ya wao kuuliza mpiga kura ni nani, anaamini katika nini, ana rekodi gani, na anatoa sababu gani za kuwashawishi wapiga kura wamchague yeye, wao wanauliza katoa shilingi ngapi, au katoa nini ili achaguliwe!

Ni dhahiri sasa kwamba Tanzania ya sasa imeingia katika ubepari kwa spidi kubwa na kuna viashiria vingi, hasa mijini, vya ubepari. Lakini, kama walivyojadili wachambuzi wengine kuhusu jambo hili, katika vitu ambavyo vimevuruga misingi ya utaifa na uzalendo wetu ilikuwa ni namna tulivyoingia katika ubepari. Kwanza kilichofanyika wakati huo wa mpito, ilikuwa kama hadaa. Serikali na asasi zingine hazikuchukua hatua za kutosha kuwaandaa Watanzania kuingia na kukabili changamoto za mfumo mpya.

Nimesema hadaa kwa sababu viongozi walipokubali msukumo wa kufanya mabadiliko ya kiuchumi, waliyafanya kwa kuvizia.

Wakahakikisha Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inabaki ikisema hii ni nchi inayofuata siasa za Ujamaa na Kujitegemea hata pale ambapo asilimia kubwa ya mashirika ya umma na migodi viliuzwa kwa wageni na kuwasaidia wao kujitegemea zaidi na sisi kuendeleza utegemezi.

Pamoja na kwamba nimehitimisha huko nyuma kwamba CCM watakaa sana madarakani bado kuna sababu za kisayansi zinazoazima ukweli kutoka katika historia, zinazoonyesha kuwa chama hicho kikongwe kitatengeneza mazingira ya kuchokwa na kuchukiwa na siku kiking'olewa kitatupiliwa mbali na kisipate tena nafasi ya kutawala. Moja ya mambo waliyoyafanya viongozi wa nchi, baada ya kukubali kufakamia ubepari, ni kuanza kuuza na kugawana rasilmali za nchi wao na familia zao, huku kapuku wapiga kura wakiendelea kufukarika.

Wapigakura fukara wakaanza kuwa manamba katika mashirika yaliyouzwa kwa wageni na wakawa wanatendewa kama walivyotendewa babu zao na wakoloni. Na baada ya hapo wananchi wenye uzalendo walipohoji wakawa wanaambiwa waache wivu.

Ikafikia mahala kiongozi mkuu kabisa wa muhimu akawaambia Watanzania waache wivu wa kike! Na kuna gazeti moja juzi lilimnukuu rais mstaafu akirejea tena kauli hiyo hiyo kwamba watu waache wivu.

Inawezekana kweli wapo wanasiasa ambao katika ushindani wanaposhindwa huweza kuwa na wivu kwamba wamekosa nafasi ya kukalia kiti fulani au kupata 'ulaji' fulani. Na kwa mantiki rahisi kama maana ya madaraka ni kupata utukufu wa kiti fulani au kupata ulaji, basi matumizi ya neno "wivu" ni sahihi kabisa.

Lakini kama maana ya madaraka ni dhamana ya kuwatumikia watu wote bila ubaguzi, basi matumizi ya neno 'wivu' dhidi ya wale wanaokosoa hayawi na mantiki. Na madhali viongozi wetu hawa hawa wametuingiza katika mfumo ambamo wao wanautumia kutengeneza utajiri wao binafsi na familia zao huku asilimia takriban 50 ya Watanzania wanawaza pa kupata mlo wa pili wa siku, basi watarajie sana kuona wenye 'wivu' wakiongezeka.

Madhali viongozi wetu wanaona ni sahihi kutumia dhamana ya madaraka waliyopewa na wananchi – au waliyonunua katika uchaguzi –kuchuma rasilmali za nchi kwa ajili yao na familia zao, basi watarajie 'wivu' mbaya zaidi huko tunakoelekea. Moja ya hulka ya binadamu ni kujisahau. Na hasa viongozi wa Afrika wanapokuwa madarakani hujisahau mno. Hujenga kiburi. Hudhani kuwa wanaweza kukanyagilia mbali haki za wananchi wao ilimradi wasipigiwe kelele wanapokuwa wanakula. Lakini ni viongozi majuha wanaojisahau kiasi hicho.

Niliwahi kusimulia madhila yaliyowakuta viongozi wa Afrika madikteta na wabinafsi ambao walidhani wao kuwa madarakani ni fursa ya kujiletea furaha binafsi wao na familia zao.

Nikatoa hadi mifano ya jinsi mmoja baada ya mwingine, akiwamo Samuel Doe wa Liberia, alivyofikia mwisho wake kwa fedheha. Na katika demokrasia ya leo kiongozi anaweza kujifanya mungu mtu lakini ajue kesho kutwa kipindi chake kuwa madarakani kinafikia ukomo.

Na hata wapambe wa viongozi ambao wakati mwingine hawawashauri kwa umakini au huamua kuwapotosha, pia hujikuta wamewekwa kando na mfumo mpya na ndipo hujidai eti wamefunguka macho.

Leo hii Tanzania imetengeneza mjadala usiokwisha kuhusu ufisadi. Na mjadala huu umewagawa watu wengi katika makundi mawili makuu. Wapo wanaounga mkono juhudi za kupiga vita ufisadi na wapo wanaounga mkono mafisadi.

Wanaounga mkono vita dhidi ya ufisadi wamegawanyika makundi mawili pia. Katika hao, wapo wenye 'wivu' kwa sababu walikosa fursa kwani hata wao wakizipata watakuwa mafisadi, na kundi la pili ni la wale wanaoamini kuwa ufisadi unajenga ubinafsi na kufru ya kitabaka ambayo itakuja kuleta maafa huko mbele.

Wanaowaunga mkono mafisadi pia wamegawanyika katika makundi mawili makuu. Wapo wanaowaunga mkono mafisadi kwa sababu nao ni wanufaika, ama wa michongo au makombo yao. Na wapo pia wanaounga mkono ufisadi kwa sababu wanaamini kuwa hakuna namna mfumo wa kibepari – ambao viongozi waliufakamia – unaweza kufanikiwa bila kuwapo ufisadi. Kwamba mfumo wa kibepari wenyewe unajenga mazingira ya watu wachache kujilimbikizia mali kupitiliza na wengi kubakia manamba wa kuwafanyia kazi wale wachache ili kupata mkate wao. Suala hili , hakika, linahitaji mjadala zaidi.


SOURCE:RAIA MWEMA
 
"hata ccm wakiweka ng'ombe,aweza kushind"
Tena ushindi wa sunami/kimbunga!!!!!!
 
nani anabisha???? hapa hata akiwekwa nyani au chui lazima ashinde
 
huoni wanasimamisha vichaa na wenye mitindio ya akili na wanashinda?so hata ngombe,mbuzi kuku atatetewa sna na wazee wa chama na serikali
 
Nadhani unaposema Ng'ombe unamaanisha kiongozi feki asiye na sifa. Maana kwa jinsi nionavyo kama kweli waweke ng'ombe kwa zama hizi i believe watashangaa kitakachotokea. Kwani uamko upo japo kidogo sana na unaendelea kukua.

Mengine ni kawaida kwani hata haya mambo yote kufumka ni kwa sabababu kuna baadhi hawakupata mgao hivyo wakaamua kuyaweka wazi. Vinginevyo mpaka sasa tungekuwa tunaumizwa tu. Naamini sasa hivi wizi umepungua siyo kama kipindi kile hata wakifanya jasho linawatoka siyo kama kipindi wanafanya wakijua huwafanyi kitu.
 
Si hivyo tu, hata wasipoweka mgombea, watashinda tuuuuu

Hilo halina ubishi. Si unakumbuka kura za maruhani kule Pemba? CCM walishindana na maruhani baada ya CUF kujitoa kwenye uchaguzi. CCM ikashinda kwa kishindo kama kawaida yake.
 
ngoja tuangalie zanzibar tuone itakuwaje? manake wanaanza kujishindisha kule mapemaaaaaaaaaaaaaaaaaa
 
Nadhani unaposema Ng'ombe unamaanisha kiongozi feki asiye na sifa. Maana kwa jinsi nionavyo kama kweli waweke ng'ombe kwa zama hizi i believe watashangaa kitakachotokea. Kwani uamko upo japo kidogo sana na unaendelea kukua.

Mengine ni kawaida kwani hata haya mambo yote kufumka ni kwa sabababu kuna baadhi hawakupata mgao hivyo wakaamua kuyaweka wazi. Vinginevyo mpaka sasa tungekuwa tunaumizwa tu. Naamini sasa hivi wizi umepungua siyo kama kipindi kile hata wakifanya jasho linawatoka siyo kama kipindi wanafanya wakijua huwafanyi kitu.

Ng'ombe mnyama sio mtu. Ili mradi awe amebeba bendera ya kijani.
Watu wanaangalia CCM zaidi ya mgombea. Ila kikubwa zaidi si watu bali ni system inayosimamia uchaguzi. Maana wizi wa kura kwa ktumia tume yao ya Makame umekuwa kama mchezo wa kawaida na hakuna asiyeujua. Maana kama ni kipofu kishashikwa mkono ila wao wanajivunia kutumia mabavu ya polisi na UWT katika kunyamazisha watu.

Hebu tuliwashe kama Kenya tuone nini kitatokea, watasalimu amri. Ila kwao ni bora watanzania wapoteze maisha kuliko CCM kutolewa madarakani maana wanajua kuwa mali zote walizoiba ni lazima zirejeshwe mikononi mwa umma. Na hili ndilo linalowafanya wawe na usemi wa "LAZIMA TUSHINDE KWA VYOVYOTE".

Mungu Ibariki Tanzania
 
Matayarisho ya kumpata mwenye meno yanaendelea
HappyCow.jpg

Lipstick kesha pakaa, tunamalizia kumrembesha ngozi yake. Ndugu zangu tuvumilieni hii kazi bado siyo rahisi mwaka 2010
 
Matayarisho ya kumpata mwenye meno yanaendelea
HappyCow.jpg

Lipstick kesha pakaa, tunamalizia kumrembesha ngozi yake. Ndugu zangu tuvumilieni hii kazi bado siyo rahisi mwaka 2010
Mleteni huyu Kyela, tutamla kitoweo kabla hata ya kufika kuchukua form.
 
"hata ccm wakiweka ng'ombe,aweza kushind"
Tena ushindi wa sunami/kimbunga!!!!!!

Naam huo ndiyo ukweli halisi hata wakiweka Nyani 2010 watashinda, ni hali ambayo inasikitisha sana hasa ukitilia maanani jinsi Viongozi wengi wa juu wa CCM walivyogubikwa na kashfa mbali mbali tena nzito za ufisadi lakini ndiyo ukweli wa mambo.
 
Back
Top Bottom