Ccm hakina wanachama!!!!!!!!

Dangire

JF-Expert Member
Oct 5, 2011
221
68
kwa kuangalia sifa na kiapo cha uanachama wa mwanachama wa ccm (kwa mujibu wa katiba yao), kwa sasa ama hakuna kabisa wanachama wa ccm ama kama wapo ni wachache sana. wenge waliopo ni wa chaa kipya kinachoitwa chama cha magamba a.k.a cha mafisadi. hebu jimuvuzishe mwenyewe katika vifungu hivi vya katiba ya ccm.

Masharti ya uanachama(uk.11)
Mtu atakayekubaliwa kuingia katika CCM, au
kuendelea kuwa Mwanachama, ni yule
anayetimiza Masharti yafuatayo:-
(1) Kuwa mtu anayeheshimu watu.
(2) Kuwa mtu anayefanya juhudi ya
kuielewa, kuieleza, kuitetea na
kuitekeleza Itikadi na Siasa ya CCM.
Kuwa mtu mwenye kuamini kuwa kazi
ni kipimo cha Utu, na kuitekeleza imani
hiyo kwa vitendo.
(4) Kuwa mtu anayependa kushirikiana na
wenzake.
(5) Kuwa mtu ambaye siku zote yuko
mstari wa mbele katika utekelezaji wa
mambo yote ya Umma, kulingana na
Miongozo ya CCM.
(6) Kuwa wakati wote ni mfano wa tabia
nzuri kwa vitendo vyake na kauli yake,
kuwa mwaminifu na kutokuwa mlevi au
mzururaji.
(7) Kuwa ama Mkulima, Mfanyakazi, au
mwenye shughuli nyingine yoyote halali
ya kujitegemea.


AHADI ZA WANACHAMA WA CHAMA
CHA MAPINDUZI
(uk.201)
(1) Binadamu wote ni ndugu zangu na Afrika ni
moja
(2) Nitaitumikia nchi yangu na watu wake wote.
(3) Nitajitolea nafsi yangu kuondosha umaskini,
ujinga, magonjwa na dhuluma.
(4) Rushwa ni adui wa haki, sitapokea wala kutoa
rushwa.
(5) Cheo ni dhamana, sitatumia cheo changu wala
cha mtu mwingine kwa faida yangu.
(6) Nitajielimisha kwa kadri ya uwezo wangu na
kuitumia elimu yangu kwa faida ya wote.
(7) Nitashirikiana na wenzangu wote kujenga nchi
yetu.
(8) Nitasema kweli daima, fitina kwangu mwiko.
(9) Nitakuwa mwanachama mwaminifu wa CCM
na raia mwema wa Tanzania na Afrika.
 
Hizi mambo mbona kama nimeishawahi kuelekezwa kuzifuata wakati sijawahi kuwa mwana ccm?
 
kwa kuangalia sifa na kiapo cha uanachama wa mwanachama wa ccm (kwa mujibu wa katiba yao), kwa sasa ama hakuna kabisa wanachama wa ccm ama kama wapo ni wachache sana. wenge waliopo ni wa chaa kipya kinachoitwa chama cha magamba a.k.a cha mafisadi. hebu jimuvuzishe mwenyewe katika vifungu hivi vya katiba ya ccm.

Masharti ya uanachama(uk.11)
Mtu atakayekubaliwa kuingia katika CCM, au
kuendelea kuwa Mwanachama, ni yule
anayetimiza Masharti yafuatayo:-
(1) Kuwa mtu anayeheshimu watu.
(2) Kuwa mtu anayefanya juhudi ya
kuielewa, kuieleza, kuitetea na
kuitekeleza Itikadi na Siasa ya CCM.
Kuwa mtu mwenye kuamini kuwa kazi
ni kipimo cha Utu, na kuitekeleza imani
hiyo kwa vitendo.

(4) Kuwa mtu anayependa kushirikiana na
wenzake.
...

Hapo kwenye red. Kifungu hicho kililenga watu wa mwambao ndiko kulikojaa wavivu, wabishi, na walalamishi.
 
Hizi mambo mbona kama nimeishawahi kuelekezwa kuzifuata wakati sijawahi kuwa mwana ccm?

wakati huo ulikuwa ni wa chama kimoja hivyo iliaminika kuwa kila mtu anaipenda ccm.misingi yake ilikuwa inafundishwa ili kukufanya uwe mwana ccm.
 
Ktk vyote hapo ni vipi ambavyo viongozi wao kama mfano wanatekeleza? Kwa upande wangu sijaona hata moja linalotekelezwa!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom