CCM haitaiacha ikulu kwa kura

Ukifikiria ujumbe ulioletwa hapa na hali halisi nina uhakika unashikwa na tumbo la kuharisha. Anza kutafuta kazi nyingine ya kufanya kuanzia 2015, serikali ijayo haitahitaji walamba viatu ili wapate mkate wao.

Ni kweli kabisa dalili za ccm kutotaka kuachia ikulu zinaonekana wazi tangu mwaka 2000, ila dawa 2015 ni kama Kenya, kuonewa kuna kikomo!
 
Mkuu umenena ila mimi naona ni suala la muda tu hata kina mama watatoka barabarani kwani watakapokosa unga wa kupika itabidi wajitokeze tu. 2015 may be too near for cdm or any other party but if ccm continue with the trend ya umimi or sisi tu they are on the road marching out of ikulu.
 
Wasi wasi wa mleta mada ni wa kweli kabisa, kuna kila dalili kuwa CCM haitakuwa tayari kuondoka Ikulu kwa sanduku la kura.

Mfano mmojawapo mkubwa kabisa ni haya mauaji ya polisi yanayoendelea nchi nzima, kwenye shughuli za CDM, huo ulikuwa mpango mahsusi wa CCM, kutaka kukipakazia Chadema kuwa ni chama cha fujo, ili baadaye vibaraka wa CCM, kina Tendwa wakifute.

Bahati nzuri sana kwa CDM, tukio la picha zilizoonyesha polisi wakimsulubu Mwangosi kule Nyololo, hadi kutoa roho yake, limeiokoa CDM, na mpango huo mchafu, uliokuwa ukiratibiwa kwa karibu na msajili wa vyama.

Ili kuamini kuwa ule ulikuwa mpango mahsusi wa chama tawala, hadi hivi leo, si Kamuhanda wala Mwema, waliokubali kujiuzuru, na bosi wao JK, hajawafukuza kazi ingawa ni dhahiri mauaji yale yalikuwa ya makusudi kabisa.

Kwa maana hiyo, huo ni ushahidi tosha CCM wanajua kabisa, uwezekano wa kushinda uchaguzi wa 2015, ushakuwa finyu sana, sawasawa na ngamia kupenya kwenye tundu la sindano. Sasa nini cha kufanya, ni kuongeza awareness kwa wananchi kuwa CCM, hawatakuwa tayari kuondoka Ikulu kirahisi.

Kwa hiyo kazi kubwa ya kufanyika kuanzia sasa hadi 2015, ni kutoa elimu ya hali ya juu ya kulinda kura hadi wakati wa kutangaza matokeo. Ninaamini hata wao wakishajua mbinu zao zote za kubaki madarakani zinajulikana, wataanza kujiandaa kisaikolojia kuondoka Ikulu.

Na wao hawatakuwa wa kwanza kukabidhi nchi kwa upinzani. Jirani zetu Zambia wamefanya hivyo, hivi karibuni. Ghana, Kenya, Malawi, weshawahi kufanya hivyo. Sioni kwa nini isiwezekane kwa wa-TZ.

La muhimu ni wananchi kujipanga tayari kwa kupokea mabadiliko. MUNGU IBARIKI TANZANIA
.
 
Kiongozi wa CCM atakayeng'ang'ania kubaki ikulu atatengwa na Jumuiya ya Kimataifa na anaweza kufikwa pia kama yale yaliyomfika Rais wa zamani wa Ivory Coast Laurent Ggabgo.
 
Umenena vema.

Bahati mbaya watanzania si waarabu. Mbowe alisema juzi kuwa watanzania ni wapole kupitiliza, na hawana munkari wa kimapinduzi na ndio maana hata CCM wakifanya mizengwe wanajua tu vumbi litapoa na maisha yatasonga.

CDM wafanye lipi la ziada zaidi ya kujaribu kuamsha watanzania waliolala bila mafanikio? Wasilaumiwe CDM maana watanzania ndio wanaopiga kura na kwa kudra CDM ikaongoza, na kwa makusudi CCM ikaiba, na kwa woga na upumbavu watanzania wakakaa kimya wakilalamikia tumboni. Mwenye jukumu la mwisho ni mwananchi.
 
Umeniacha hoi sana! No comments
Nani aachie ikulu? Nyie mna wivu nini? Au mna majungu yenu? Tutawaua wote lakini si kuachia ikulu

mnanionea wivu ninavyopiga misele ya ULAYA?, au mnaona wivu mwanangu RIZ 10alivyonunua magari(zile semi treler).?

Mnataka wajomba zangu wasipate maisha mazuri eeh? Hamjui mi nina utitiri wa watoto? Wakale wapi?

Acheni majungu bana alaaaaaaa!!!!
 
Naweza kusoma kitu fulani katika Uongozi wa Kitaifa Chadema ukiongozwa na kamanda Mbowe. Mambo kadhaa ambayo yamenifikirisha kwa busara yao na umakini wao ni kama ifuatavyo:
  1. Kashfa ya utoroshwaji pesa na kuzificha Uswiss hawaligusii, limeachwa kiporo kwa wakati wake ukiwadia kulipua.
  2. Viongozi ndumila kuwili chamani wanafukuzwa mapema ili wasijeambukiza uozo kwa wengine
  3. Mabomu yaliyoandaliwa na CCM kuilipukia Chadema kama Shibuda na wenzake wanayachukua kwa tahadhari kubwa kwa manufaa ya chama.
  4. Jitihada kubwa ni kukijenga chama kuanzia matawini huko vijijini ambako CCM hujivunia, ndo maana tunaona CCM wanahaha kuvuruga uanzishwaji wa matawi Chadema vijijini kwani ngome ya CCM sasa inasambaratika.
  5. Kutambulika kimataifa, haya matawi ya huko ng'ambo ni njia tu ya kufikisha ujumbe kwa mataifa, majuzi tumeshuhudia Katibu Mkuu Chadema kuhudhuria mkutano wa kimataifa huko Ujerumani, maana yake sauti ya Chadema yaanza sikika kimataifa.
  6. Mauaji yanayofanya na serikali ya CCM yamesaidia kuitangaza zaidi Chadema Kimataifa, na hivyo ni dalili tosha ya kuanza kujulikana jitihada za Chadema kunusuru uchumi wa taifa letu na huduma bora kwa watanzania.
  7. Kashfa ya kuficha pesa Uswiss kwa viongozi waandamizi na wastaafu wa serikali ni ishara tosha ya uovu wa viongozi tulio nao tosha kwa jumuiya ya kimataifa badala ya kuelekeza nguvu kujenga nchi wao wanaliibia taifa pesa na kuzificha nje ya nchi.
  8. Mbinu chafu katika Uchaguzi mkuu uliopita ulivyoshuhudiwa na jumuiya ya mataifa kutamka wazi kuwa vyombo vya dola vimeisaidia CCM kushinda unazidikupata nguvu kutokana na Serikali kuendeleza ubabe kwa wapinzani kutumia vyombo vya dola.
  9. Matumizi ya dola dhidi ya raia wasio na hatia na mauaji yanayoendelea nchini yanazidi kuwaamsha wapiga kura udhalimu unaofanywa na serikali inayoongozwa na CCM.
  10. Historia inajieleza wazi jumuiya ya kimataifa inavyosaidia kudhoofisha tawala dhalimu kwa njia mbalimbali.
mkuu unanikumbusha mbali sana kipindi cha sekondari kwenye somo kama la history. point ni moja lakini unainyambulisha ili upate point yingi na uweze kum-convice msahishaji akupe maksi za kutosha,. I see many repeatation kwenye post yako.
 
Naweza kusoma kitu fulani katika Uongozi wa Kitaifa Chadema ukiongozwa na kamanda Mbowe. Mambo kadhaa ambayo yamenifikirisha kwa busara yao na umakini wao ni kama ifuatavyo:
  1. Kashfa ya utoroshwaji pesa na kuzificha Uswiss hawaligusii, limeachwa kiporo kwa wakati wake ukiwadia kulipua.
  2. Viongozi ndumila kuwili chamani wanafukuzwa mapema ili wasijeambukiza uozo kwa wengine
  3. Mabomu yaliyoandaliwa na CCM kuilipukia Chadema kama Shibuda na wenzake wanayachukua kwa tahadhari kubwa kwa manufaa ya chama.
  4. Jitihada kubwa ni kukijenga chama kuanzia matawini huko vijijini ambako CCM hujivunia, ndo maana tunaona CCM wanahaha kuvuruga uanzishwaji wa matawi Chadema vijijini kwani ngome ya CCM sasa inasambaratika.
  5. Kutambulika kimataifa, haya matawi ya huko ng'ambo ni njia tu ya kufikisha ujumbe kwa mataifa, majuzi tumeshuhudia Katibu Mkuu Chadema kuhudhuria mkutano wa kimataifa huko Ujerumani, maana yake sauti ya Chadema yaanza sikika kimataifa.
  6. Mauaji yanayofanya na serikali ya CCM yamesaidia kuitangaza zaidi Chadema Kimataifa, na hivyo ni dalili tosha ya kuanza kujulikana jitihada za Chadema kunusuru uchumi wa taifa letu na huduma bora kwa watanzania.
  7. Kashfa ya kuficha pesa Uswiss kwa viongozi waandamizi na wastaafu wa serikali ni ishara tosha ya uovu wa viongozi tulio nao tosha kwa jumuiya ya kimataifa badala ya kuelekeza nguvu kujenga nchi wao wanaliibia taifa pesa na kuzificha nje ya nchi.
  8. Mbinu chafu katika Uchaguzi mkuu uliopita ulivyoshuhudiwa na jumuiya ya mataifa kutamka wazi kuwa vyombo vya dola vimeisaidia CCM kushinda unazidikupata nguvu kutokana na Serikali kuendeleza ubabe kwa wapinzani kutumia vyombo vya dola.
  9. Matumizi ya dola dhidi ya raia wasio na hatia na mauaji yanayoendelea nchini yanazidi kuwaamsha wapiga kura udhalimu unaofanywa na serikali inayoongozwa na CCM.
  10. Historia inajieleza wazi jumuiya ya kimataifa inavyosaidia kudhoofisha tawala dhalimu kwa njia mbalimbali.

i like your comments!

Labda utusaidie na hili; KUSHINDA UCHAGUZI KWA KURA na KUTANGAZWA MSHINDI ni vitu viwili tofauti.
Tunafahamu mwenyekiti wa tume ya uchaguzi ameteuliwa na serikali ya ccm na hutekeleza majukumu yake kwa utashi wa serikali ya ccm kwa chaguzi zote za uraisi zilizopita.Je CDM ikishinda uchaguzi wa kura na CCM ikatangazwa mshindi wa Uraisi, JE
1. Hauoni Chadema watalazimishwa wakapinge matokeo mahakamani, mahakama ambayo raisi alishateua majaji wake b4?
2. Hauoni kwamba wafuasi wa chadema watadhibitiwa na jeshi la Polisi baada ya matokeo hayo , Jeshi la polisi ambalo linaendelea kuimarishwa kwa zana za kijeshi kuwakabili chadema ambao tayari wataongozwa na woga wa kumbukumbu za mauaji?
 
Ccm wanajua dhahiri kwa namna yoyote ile hawawezi kuendelea kushika dola 2015. Uzuri wa hili, hata sisi wananchi tumesha lifahamu mapema kuliko wao wanavyo fikiri.

Cha kuwasaidia ccm kwa sasa ni kuwajenga kisaikolojia ili wawe chama tulivu cha upinzani mara baada ya uchaguzi huku wakiwa wameicha sebule ya ikulu yetu bila mikwaruzo ya risasi au harufu ya mabomu.

Wanachotakiwa kikijua.

1. Wanatakiwa watambue kuwa wao hawana hati miliki ya kuiongoza Tanzania kwa namna wanayotaka wao kama wenye nchi wamewachoka na wana taka mbadala wa chama kingine.

2. Ccm na viongozi wao waache kufikiri kuwa wao ndio watanzania zaidi kuliko watanzania wengine kwenye jamhuri ya muungano na hivyo wana uwezo wa kusema flani afe/auwawe kwa kuwa anataka mabadiliko yanayo tishia uhai wa chama chao.

3. Ccm wanatakiwa kujua kuwa kuruhusiwa vyama vingi ile 1992 ilikuwa ni kuruhusu fursa ya chama kingine kuja kushika dola ccm ikichokwa, hivyo hawatakiwi kuwa na mawazo ya kutawala watu walio wachoka.

4. Ccm Wanatakiwa kujua kuwa mabadiliko ni mpango wa Mungu na sasa Mungu yuko upande wa wanaotaka mabadiliko, hivyo waache mara moja kumhusisha Mungu na dhamira zao chafu za kutumia polisi ili kutafuta uhalali wa kutawala kwa mkono wa chuma au kusingizia vitu vizito kutoka angani.

5. Ccm wanatakiwa kujua kuwa kiwango cha akili kilicho sababisha matatizo ndani ya miaka 50 ya uhuru kinahitaji mbadala wa akili ya kiwango kingine cha juu zaidi kwa sababu watu haohao, wa chama kilekile, mtazamo uleule na akili ileile iliyo sababisha matatizo na kuyaacha yakomae hawawezi kutatua matatizo hayo.

HITIMISHO.

Mipango mingi ya hila ambayo ccm wameipanga dhidi ya chadema imekuwa inasanuka mchana kweupe kabla ya kutekelezwa, hata mauwaji ya Mwangosi achana na kutekwa na kuteswa kwa Dr Ulimboka kama kusingekuwa na picha za tukio ule uzushi wa changonja, utabiri wa Nape, kauli za Shigella + nchimbi + wasira + sitta + Tendwa = kuifuta au kuizua chadema kufanya mikutano. Mungu aliwaumbua mapema ndio maana nasema mabadiliko yanayo ratibiwa na chadema kwa sasa ni mpango wa Mungu.

Sent from BlackBerry 8520 authorized by JamiiForums.
 
Case in point is that while planning ahead is always an irreplaceable factor, but we need also to familiarize with "don't cross the bridge...till you reach one" approach.
 
Ni kweli kabisa dalili za ccm kutotaka kuachia ikulu zinaonekana wazi tangu mwaka 2000, ila dawa 2015 ni kama Kenya, kuonewa kuna kikomo!
Haya ni maneno matupu, CCM haiwezi kutoka kwa kura wala kwa nguvu. Nyie kajipangeni mstari siku nzima kuchagua mtu hewa, hizo kura ni kupoteza karatasi tu. CCM inachagua jimbo gani wapewe upinzani ili kuonyesha demokrasia ipo Tanzania. 2015 CCM itashinda kwa kura chache lakini wabunge wa upinzani watapungua sana. Hakuna wewe wala wenzako mtakalo weza kulifanya kwa sababu haya mambo yamesha amuliwa siku nyingi. Nyie bora wala msijishughulishe na haya mambo, mnatafuta ugonjwa wa moyo tu.
 
Ccm wanajua dhahiri kwa namna yoyote ile hawawezi kuendelea kushika dola 2015. Uzuri wa hili, hata sisi wananchi tumesha lifahamu mapema kuliko wao wanavyo fikiri.

Cha kuwasaidia ccm kwa sasa ni kuwajenga kisaikolojia ili wawe chama tulivu cha upinzani mara baada ya uchaguzi huku wakiwa wameicha sebule ya ikulu yetu bila mikwaruzo ya risasi au harufu ya mabomu.

Wanachotakiwa kikijua.

1. Wanatakiwa watambue kuwa wao hawana hati miliki ya kuiongoza Tanzania kwa namna wanayotaka wao kama wenye nchi wamewachoka na wana taka mbadala wa chama kingine.

2. Ccm na viongozi wao waache kufikiri kuwa wao ndio watanzania zaidi kuliko watanzania wengine kwenye jamhuri ya muungano na hivyo wana uwezo wa kusema flani afe/auwawe kwa kuwa anataka mabadiliko yanayo tishia uhai wa chama chao.

3. Ccm wanatakiwa kujua kuwa kuruhusiwa vyama vingi ile 1992 ilikuwa ni kuruhusu fursa ya chama kingine kuja kushika dola ccm ikichokwa, hivyo hawatakiwi kuwa na mawazo ya kutawala watu walio wachoka.

4. Ccm Wanatakiwa kujua kuwa mabadiliko ni mpango wa Mungu na sasa Mungu yuko upande wa wanaotaka mabadiliko, hivyo waache mara moja kumhusisha Mungu na dhamira zao chafu za kutumia polisi ili kutafuta uhalali wa kutawala kwa mkono wa chuma au kusingizia vitu vizito kutoka angani.

5. Ccm wanatakiwa kujua kuwa kiwango cha akili kilicho sababisha matatizo ndani ya miaka 50 ya uhuru kinahitaji mbadala wa akili ya kiwango kingine cha juu zaidi kwa sababu watu haohao, wa chama kilekile, mtazamo uleule na akili ileile iliyo sababisha matatizo na kuyaacha yakomae hawawezi kutatua matatizo hayo.

HITIMISHO.

Mipango mingi ya hila ambayo ccm wameipanga dhidi ya chadema imekuwa inasanuka mchana kweupe kabla ya kutekelezwa, hata mauwaji ya Mwangosi achana na kutekwa na kuteswa kwa Dr Ulimboka kama kusingekuwa na picha za tukio ule uzushi wa changonja, utabiri wa Nape, kauli za Shigella + nchimbi + wasira + sitta + Tendwa = kuifuta au kuizua chadema kufanya mikutano. Mungu aliwaumbua mapema ndio maana nasema mabadiliko yanayo ratibiwa na chadema kwa sasa ni mpango wa Mungu.

Sent from BlackBerry 8520 authorized by JamiiForums.
Wewe kweli umelala, CCM inayo hati miliki ya hii nchi kama ulikua hujui. Watanzania hawana jeuri ya kufanya lolote, wanapenda raha sana na ni waoga wa kufa.
 
Atakayeshinda uchaguzi ataingia ikulu, ili kuepusha umwagikaji wa damu. Usicheze na wananchi, mkoloni aliondoka sembuse haka ka CCM.
Mkoloni alitolewa na nani? Waliamua kutuachia nchi na kumweka mtu wao. Hakuna damu itakayo mwagika zaidi ya wale mbuzi wa sherehe.Wananchi wa nchi nyingine sawa lakini wa Tanzania hakuna kitu.
 
Ccm wanajua dhahiri kwa namna yoyote ile hawawezi kuendelea kushika dola 2015. Uzuri wa hili, hata sisi wananchi tumesha lifahamu mapema kuliko wao wanavyo fikiri.

Cha kuwasaidia ccm kwa sasa ni kuwajenga kisaikolojia ili wawe chama tulivu cha upinzani mara baada ya uchaguzi huku wakiwa wameicha sebule ya ikulu yetu bila mikwaruzo ya risasi au harufu ya mabomu.

Wanachotakiwa kikijua.

1. Wanatakiwa watambue kuwa wao hawana hati miliki ya kuiongoza Tanzania kwa namna wanayotaka wao kama wenye nchi wamewachoka na wana taka mbadala wa chama kingine.

2. Ccm na viongozi wao waache kufikiri kuwa wao ndio watanzania zaidi kuliko watanzania wengine kwenye jamhuri ya muungano na hivyo wana uwezo wa kusema flani afe/auwawe kwa kuwa anataka mabadiliko yanayo tishia uhai wa chama chao.

3. Ccm wanatakiwa kujua kuwa kuruhusiwa vyama vingi ile 1992 ilikuwa ni kuruhusu fursa ya chama kingine kuja kushika dola ccm ikichokwa, hivyo hawatakiwi kuwa na mawazo ya kutawala watu walio wachoka.

4. Ccm Wanatakiwa kujua kuwa mabadiliko ni mpango wa Mungu na sasa Mungu yuko upande wa wanaotaka mabadiliko, hivyo waache mara moja kumhusisha Mungu na dhamira zao chafu za kutumia polisi ili kutafuta uhalali wa kutawala kwa mkono wa chuma au kusingizia vitu vizito kutoka angani.

5. Ccm wanatakiwa kujua kuwa kiwango cha akili kilicho sababisha matatizo ndani ya miaka 50 ya uhuru kinahitaji mbadala wa akili ya kiwango kingine cha juu zaidi kwa sababu watu haohao, wa chama kilekile, mtazamo uleule na akili ileile iliyo sababisha matatizo na kuyaacha yakomae hawawezi kutatua matatizo hayo.

HITIMISHO.

Mipango mingi ya hila ambayo ccm wameipanga dhidi ya chadema imekuwa inasanuka mchana kweupe kabla ya kutekelezwa, hata mauwaji ya Mwangosi achana na kutekwa na kuteswa kwa Dr Ulimboka kama kusingekuwa na picha za tukio ule uzushi wa changonja, utabiri wa Nape, kauli za Shigella + nchimbi + wasira + sitta + Tendwa = kuifuta au kuizua chadema kufanya mikutano. Mungu aliwaumbua mapema ndio maana nasema mabadiliko yanayo ratibiwa na chadema kwa sasa ni mpango wa Mungu.

Sent from BlackBerry 8520 authorized by JamiiForums.
Unajua Mtu kama wewe huwa kwanzanaanza kuwapa reputation kama thinkers, halafu nachangia. Yaanai ni mwendawazimu tu ndie anayeweza kufikiri kuna chama kitatawala milele, yaani ni mtu asiyesoma trend mbalimbali duniani. hata CDM yenyewe ikiingia 2015 inajua kwamba haitawala milele. Acha tu ule wa uhakika wa hicho chama kuwepo milele ni infinitely small. You are a thinker. Sio akina Rejao na Ritz2.
 
Wasi wasi wa mleta mada ni wa kweli kabisa, kuna kila dalili kuwa CCM haitakuwa tayari kuondoka Ikulu kwa sanduku la kura.

Mfano mmojawapo mkubwa kabisa ni haya mauaji ya polisi yanayoendelea nchi nzima, kwenye shughuli za CDM, huo ulikuwa mpango mahsusi wa CCM, kutaka kukipakazia Chadema kuwa ni chama cha fujo, ili baadaye vibaraka wa CCM, kina Tendwa wakifute.

Bahati nzuri sana kwa CDM, tukio la picha zilizoonyesha polisi wakimsulubu Mwangosi kule Nyololo, hadi kutoa roho yake, limeiokoa CDM, na mpango huo mchafu, uliokuwa ukiratibiwa kwa karibu na msajili wa vyama.

Ili kuamini kuwa ule ulikuwa mpango mahsusi wa chama tawala, hadi hivi leo, si Kamuhanda wala Mwema, waliokubali kujiuzuru, na bosi wao JK, hajawafukuza kazi ingawa ni dhahiri mauaji yale yalikuwa ya makusudi kabisa.

Kwa maana hiyo, huo ni ushahidi tosha CCM wanajua kabisa, uwezekano wa kushinda uchaguzi wa 2015, ushakuwa finyu sana, sawasawa na ngamia kupenya kwenye tundu la sindano. Sasa nini cha kufanya, ni kuongeza awareness kwa wananchi kuwa CCM, hawatakuwa tayari kuondoka Ikulu kirahisi.

Kwa hiyo kazi kubwa ya kufanyika kuanzia sasa hadi 2015, ni kutoa elimu ya hali ya juu ya kulinda kura hadi wakati wa kutangaza matokeo. Ninaamini hata wao wakishajua mbinu zao zote za kubaki madarakani zinajulikana, wataanza kujiandaa kisaikolojia kuondoka Ikulu.

Na wao hawatakuwa wa kwanza kukabidhi nchi kwa upinzani. Jirani zetu Zambia wamefanya hivyo, hivi karibuni. Ghana, Kenya, Malawi, weshawahi kufanya hivyo. Sioni kwa nini isiwezekane kwa wa-TZ.

La muhimu ni wananchi kujipanga tayari kwa kupokea mabadiliko. MUNGU IBARIKI TANZANIA
.
Naunga mkono hoja, majibu ya kura tuliyaona Arumeru watu walijipanga kulinda kura zao, nchi nzima wakiwa na mwamko wasipokubali kushindwa wakatumia majeshi na Polisi kuangamiza watu wanaodai haki zao, The Hague inawangoja!!!

Mkoloni alitolewa na nani? Waliamua kutuachia nchi na kumweka mtu wao. Hakuna damu itakayo mwagika zaidi ya wale mbuzi wa sherehe.Wananchi wa nchi nyingine sawa lakini wa Tanzania hakuna kitu.

Nadhani wewe Watanzania huwajui, wakipata msukumo usiombe kukutana nao, waulize Arusha ilikuwaje pressure kwenye halimashauri ??? Siku hiyo mtu ajaribu kudhulumu haki za kura za Watanzania aone moto utakao waka sijui ni nani atauzima, sema tu CCM wawe wastaarabu wakishindwa wakabidhi nchi kwa wenyewe!!!

Haya ni maneno matupu, CCM haiwezi kutoka kwa kura wala kwa nguvu. Nyie kajipangeni mstari siku nzima kuchagua mtu hewa, hizo kura ni kupoteza karatasi tu. CCM inachagua jimbo gani wapewe upinzani ili kuonyesha demokrasia ipo Tanzania. 2015 CCM itashinda kwa kura chache lakini wabunge wa upinzani watapungua sana. Hakuna wewe wala wenzako mtakalo weza kulifanya kwa sababu haya mambo yamesha amuliwa siku nyingi. Nyie bora wala msijishughulishe na haya mambo, mnatafuta ugonjwa wa moyo tu.
Majebere=chuchu ya nyau kikwetu, sishangai. Lakini bwana majebere hivi wewe unanufaika nini na huu mfumo mbovu wa serikali ya ccm? ukinijibu vema swali hilo nitashawishi kabila langu kubadilisha hilo jina na kuwa dhahabu badala ya chuchu ya nyau.
 
Back
Top Bottom