Elections 2010 CCM haishindi Iringa (kihalali!)

Nyamgluu

JF-Expert Member
Mar 10, 2006
3,150
1,713
Dah,nimetoka mkutano wa ccm na bilal alikuwepo. Iringa wamechoka ccm na hawaoni aibu kusema hadharani kwenye mikutano. Hii ya leo AIBU, mama mbega lazma anataka kujiuzulu ni noma but encouraging.
 
Makosa walifanya wenyewe, acha hasira za wananchi ziwamalize. Nilisoma kwenye Blog ya Francis Godwin kwamba hata Ilembula hali ilikuwa mbaya. Tatizo ni kutoheshimu kura za maoni za wanachama, na hapo ndipo walipopoteza hata maana halisi ya kura za maoni. Ngoja tuone kama hasira hizo zitaonyeshwa 31/10.
 
Mlolongo mzima nafikiri niachie magazeti kesho. Ila jamaa wamezomea na kushout chadema utafikiri mkutano wa chadema. Ccm wakajaribu kumwondoa mpayukaji mmoja umati ukataka kuwavamia hao makada wa ccm hadi ikaitwa ffu.
Apologies kwa kutoa habari 'kihuni huni' lakini mimi mwana ccm kwaio siwezi andika kwa utashi sana naogopa conflict of interest. Ila iringa hawaitaki ccm! Na wana ccm hawamtaki mbega.
 
Hayo ndo mambo! hata shinyanga hatuitaki ccm basi tu! wanatupa elimu duni haswaaa mkoani kwetu hapa Shy, tunakila saababu ya kuitwa matajiri lakini ndo wa mwisho kila mwaka kielimu. Jamani chadema njooni shy muone uozo huu wa ccm, wanakusanya kadi za watu mitaani.
 
Dk. Bilal ajionea mpasuko Njombe






MGOMBEA mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Mohamed Gharib Bilal, ameshuhudia mpasuko mkubwa ndani ya CCM katika Jimbo la Njombe Magharibi.

Dk. Bilal alishuhudia jimbo hilo linalogombewa na Thomas Nyimbo wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), baada ya kuhama CCM kwa kile kilichoelezwa kupokonywa ushindi wakati wa kura za maoni ndani ya CCM.

Wagombea, Deo Filikunjombe (Ludewa) na Anne Makinda (Njombe Kusini), wote walipita bila kupingwa, wakati katika Jimbo la Makete, mgombea wake Dk. Binilith Mahenge, hali inaonekana kuwa shwari.

Dk. Bilal alipata mapokezi makubwa, lakini alikuwa akishangiliwa na watu wasiozidi 30, wengi wao wakiwa kimya, hali inayoashiria upinzani.

Umati huo wa wana CCM waiofika katika viwanja vya Ilembula, ambavyo Nyimbo amepanga kufanya uzinduzi wake wa kampeni Ijumaa ya wiki ijayo, wengi walisema shida yao ilikuwa kumuona na kumsikiliza Nyimbo.

Nyimbo alishinda katika kura za maoni kwa kupata kura 6,793, huku mbunge aliyemaliza muda wake, Yono Kevela akipata kura 3,434 wakati Lwenge aliambulia kura 2,971.

Hata hivyo, alisema sababu ya kumwengua Nyimbo na kushindwa kumpa mtu wa pili ni kutokana na wana CCM hao kuwa na makundi makubwa ya wanachama wanaowaunga mkono.
 
Wananchi waibana CCM Iringa Mjini

Na Venance George, Morogoro na Tumaini Msowoya, Iringa

JINAMIZI la uchakachuaji wa matokeo ya kura za maoni pamoja na migogoro ya ardhi katika maeneo mbalimbali nchini jana liliipa CCM mtihani mgumu baada ya wananchi katika maeneo tofauti kumzomea mgombea na katika eneo jingine kumpa wakati mgumu mgombea urais wa CCM, Jakaya Kikwete.

Mgombe wa ubunge wa jimbo la Iringa Mjini kwa tiketi ya chama hicho, Monica Mbega alikumbana na hali ngumu kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Uwanja wa Mwembetogwa wakati karibu nusu ya wananchi waliojitokeza mkutanoni hapo kutamka kwa sauti kubwa kuwa hawampi kura huku wakionyesha alama ya vidole viwili.

Wananchi hao walifanya hivyo kutokana na mmoja wa makada wa CCM aliyejitambulishwa kwa jina la Mahamudu Madenge aliye kwenye msafara wa mgombea mwenza wa Kikwete, Dk Gharib Bilal kuuliza kama kulikuwa na mwanachama yeyote wa upinzani.

Madenge alidai kuwa jimbo la Iringa Mjini hakuna upinzani kama wao wanavyosikia wakiwa nje ya mkoa huo na hiyo inatokana na CCM ambayo alidai inatekeleza vizuri ilani yao.

"Manispaa ya Iringa hakuna upinzani kama tunavyosikia tukiwa jijini Dar es Salaam na kwingine tukiwepo... kuna mabadiliko mengi ya kimaendeleo yaliyoletwa na CCM ikiwa ni pamoja na barabara na sekta ya elimu. Kama kuna mwanachama wa Chadema hapa anyooshe kidole," alisema Madenge.

Lakini alikumbana na majibu ambayo hakutegemea. Nusu ya wananchi waliokuwepo walisema "tupo" na kunyoosha vidole viwili ambayo ni alama ya Chadema.
Hali ilikuwa mbaya zaidi baada ya Dk Bilal kumaliza hotuba yake na kundi la Tip Top Connection kupanda jukwani na kuimba wimbo wa kuisifia CCM.

Wimbo huo ulionekana kukera baadhi ya watu ambao walianza kufanya fujo huku wakirusha mawe na kupiga kelele za "Chadema, Chadema" na kusababisha polisi kulazimika kuingilia kati kuwatanya watu hao ambao walikwenda pembeni na kuendeleza kelele.

Wakati hayo yakitokea, mgombea wa Chadema alipita na gari lenye picha zake na kuamsha kelelza shangwe, lakini polisi walipiga king'ora ili kuwadhibiti watu waliokuwa wakifanya fujo, ikiwa ni pamoja na kuzomea magari ya CCM yaliyokuwa wakiondoka.

Wakati Dk Bilal alipojaribu kumnadi Mbega kabla ya kumaliza hotuba yake, watu wengi walikaa kimya huku waliopaza sauti kujibu walionekana kuwa wachache.

Katibu mkuu wa zamani wa Shirikisho la Soka (TFF), Frederick Mwakalebela alimshinda Mbega, ambaye anatetea kiti chake, kwa kura nyingi lakini siku moja kabla ya kupiga kura za maoni alihojiwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) akidaiwa kutoa rushwa ya Sh100,000 kwa nyakati mbili tofauti pamoja na mkewe. Tayari Mwakalebela na mkewe wamefunguliwa kesi ambayo inaendelea.

Mwakalebela alienguliwa kwenye kinyang'anyiro cha ubunge wakati wa kikao cha halmashauri kuu ya CCM ambacho kilimteua Mbega kutetea nafasi yake.
Wakati hayo yakiendelea, wakazi wa Kijiji cha Mvomero kilicho Kata ya Mvomero mkoani Morogoro wamemuomba mwenyekiti wa CCM, Jakaya Kikwete kuwarejeshea shamba linalodaiwa kumilikiwa na waziri mkuu mstaafu, Fredrick Sumaye lililo kwenye kijiji hicho.

Akiwasilisha ombi hilo kwa Kikwete, mgombea udiwani wa kata hiyo, Shiri Shomari ambaye alizungumza kwa niaba ya mwenyekiti wa kijiji hicho alisema kuchukuliwa kwa shamba hilo kumefanya wananchi kukosa ardhi ya kutosha ya kulima.

Shomari alipata fursa ya kuuliza swali hilo baada ya Kikwete kumtaka mwenyekiti wa kijiji hicho kujitokeza ili kueleza kero zinazowakabili wananchi wa eneo hilo mara baada ya kusimama kusalimia wananchi wakati akitokea Kilosa kuelekea Tuliani.

Ombi la mgombea huyo wa udiwani lilifanya wananchi kushangilia, jambo lililotafsiriwa kama ishara kuwa waliporwa kiwanja hicho na suala hilo limekuwa kero kubwa kwao.

Akijibu swali hilo pamoja na tatizo sugu la maji katika kijiji hicho, Kikwete alisema: "Suala la umiliki wa ardhi si suala la kukurupuka katika kulitolea majibu badala yake naomba jambo hili kulichukua; nawaahidi kulifanyia kazi."
Kikwete ambaye alimaliza ziara yake mkoani Morogoro kwa kuzungumza na wananchi wa Kata ya Mtibwa wilayani Mvomero, alisema ameulizwa maswali mengi yanayohusu migogoro ya ardhi katika maeneo mbalimbali ya mkoa humo.

Mbali na Mvomero katika kijiji cha Dumila wilayani Kilosa, Kikwete aliulizwa juu ya umiliki wa sehemu ya ardhi ya kijiji hicho iliyotolewa kwa mfanyabiashara (jina halikutajwa) bila serikali ya kijiji kushirikishwa.
Akijibu swali hilo Kikwete alisema kuwa serikali ya kijiji ni serikali yenye mamlaka na umiliki wa ardhi na kusisitiza kuwa mtu kupata ardhi lazima kijiji kitoe kibali.

"Kama kijiji hakikushirikishwa ni lazima kuchunguza ili kujua uhalali wa umiliki na kisha kutoa majibu stahiki," alisema Kikwete.
Wakati huohuo, Kikwete ameahidi kuwajengea nyumba za kudumu wahanga wa mafuriko ya mwaka jana katika wilaya hiyo. Baadhi ya watu walipoteza maisha na wengi kukosa makazi baada ya mafuriko hayo makubwa.
Akizungumza katika mkutano wa kampeni katika siku ya pili ya ziara yake mkoani Morogoro, Kikwete alisema kuwa ujenzi huo utakaofanywa na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) utaanza hivi karibuni.

Kikwete aliwaambia wakazi wa wilaya ya Kilosa kuwa ahadi hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa jitihada zinazofanywa na serikali kuhakikisha kuwa maisha ya wahanga yanarejea kama ilivyokuwa awali.

Alisema kuwa na ndiyo maana wahanga hao ambao ni zaidi ya 11,000 hawakuachwa bila kusaidiwa kwa kuwa serikali iliwapatiwa kila aina ya msaada, ikiwa ni pamoja na chakula na makazi ya muda.
"Mwanzo tuliwaweka katika mahema baadaye kwenye 'full suit' za bati, lakini lengo ni kuwajengea wote nyumba za kudumu," alisema Kikwete.

Kikwete pia alisema serikali imeanza mchakato wa ujenzi wa Bwawa la Kidete linalodaiwa kuwa chanzo cha mafuriko ya mara kwa mara katika mji wa Kilosa.

Mgombea huyo alisema kuwa bwawa la Kidete lilijengwa mwaka 1943 na kwamba lilijaa tope kiasi cha kushindwa kuhimili kasi ya maji yatokayo katika milima ya Mpwapwa, Kongwa na Kiteto.

Alisema mbali ya ujenzi wa bwawa hilo, pia serikali itajenga upya tuta la ukingo wa Mto Mkondoa ili uweze kupitisha maji kwa urahisi na kwamba fedha kwa ajili ya ujenzi huo zimeshatengwa na kinachosubiriwa ni kupatikanaji wa mkandarasi.

Awali katika uzinduzi wa kampeni za ubunge katika jimbo la Kilosa, mgombea ubunge wa jimbo hilo (CCM), Mustapha Mkullo alisema kuwa serikali inatarajia kutumia wastani wa Sh13 bilioni kujenga miundombinu hiyo ikiwa ni pamoja na kuongeza bwawa jingine na kufanya mtandao mzima kuwa na mabwawa mawili.

Chanzo: Mwananchi
 
Hivi JK alipita hapo Iringa au hakupita? Nadhani alishauriwa asipite kumkwepesha aibu.
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom