Elections 2010 CCM: Elimu ya msingi hadi kidato cha nne

Gurudumu

JF-Expert Member
Feb 5, 2008
2,349
261
Leo mnamo saa 4:38 usiku, Jumanne Magembe ametangazia umma kupitia ITV kwamba CCM utatoa elimu ya msingi kuanzia darasa la kwanza hadi kidato cha nne.

Ilipitishwa lini na Bunge?
 
Yaani hata huyo waziri mwenyewe alipokuwa anaongea alionekana wazi hajiamini na anaona aibu fulani hivi. Nadhani atakuwa amelazimishwa kutangaza lakini moyoni haipo.
 
Mh! Kweli CCM wanatapatapa kwa wizi wa hoja za watu! Hii hoja ilikuwa ni ya Dr Slaa na aliyeinzisha kuhusu elimu ya msingi, tena yeye alitaka iwe hadi form six.

Sasa CCM wamekaa na kuiona na nzuri, wamekurupuka na kuamua kuifanya kuwa yao, siku 5 kabla ya uchaguzi. Wanaharakishia nini kama sio kutapatapa? Tatizo CCM hamjaelewa sisi wananchi tunataka kiongozi gani! Wananchi wa TZ wanataka kiongozi atakayetetea maslahi yao toka moyoni mwake na asiye na doa!

Nyie CCM ham-fit kwenye hivyo vigezo!! Kwahiyo hata mdanganye vipi, HATUDANGANYIKII!
 
Leo mnamo saa 4:38 usiku, Jumanne Magembe ametangazia umma kupitia ITV kwamba CCM utatoa elimu ya msingi kuanzia darasa la kwanza hadi kidato cha nne.

Ilipitishwa lini na Bunge?
Si hivi majuzi tu, hata wiki haijapita walikuwa wanasema elimu bure haiwezekani kwa bidii sana? Hii sasa ni comedy!:smile-big:
 
Wanahangaika, wanatapatapa, Huwezi amini eti juzi kiwazili fulani kinataka bei za vifaa vya ujenzi zishuke! what a joke!
 
Leo mnamo saa 4:38 usiku, Jumanne Magembe ametangazia umma kupitia ITV kwamba CCM utatoa elimu ya msingi kuanzia darasa la kwanza hadi kidato cha nne.

Ilipitishwa lini na Bunge?

Kwani ulikuwa hujui kama sehemu nyingi kwa kutumia zile shule za kata, asilimia 90 ya wanafunzi wa darasa la saba alikuwa wanaendelea sekondari. Tatizo ni walimu tu ambalo linashughulikiwa.
Hiyo ndio ilikuwa lengo la chama tawala kwa kuanzisha shule za kata.

Hilo lipo Zanzibar kwanini lishindikane TANZANIA BARA?

Hakuna jipya hapo. Au hukusoma hotuba ya mh Kikwete akiliaga Bunge. Ninayo hapa ukitaka naweza kukuwekea. wENZAKO WALILIKUBALI HILO HAPA jf, walicholaumu ni walimu tu. Lakini Rome haikujengwa kwa siku moja.
 
Maji mushingo watajiadhiri mpaka mwisho wa dunia ukikataa kitu kwamba hakiwezekani simamia hapo na sababu sasa wananchi wote watawadharau sana kwa kuonyesha kuwa elimu bure haitoshi na kuja kula matapishhi yao
 
Si hivi majuzi tu, hata wiki haijapita walikuwa wanasema elimu bure haiwezekani kwa bidii sana? Hii sasa ni comedy!:smile-big:

Rudia kusoma Thread, kwani wapi walipoandika ELIMU BURE.

kUTOA elimu toka Msingi mpaka Sekondari kidato cha nne maana yake kila mtanzania atawajibika kusoma mpaka kidato cha NNE. Ni kama serikali ilivysema kuwa mtoto akifaulu kwenda sekondari na mzee akmuozesha au akamkataza kwenda huko kwa sababu ya kuchunga Ng'ombe basi mzee atashitakiwa.
 
NIMEKUBALI: Nimekubali kuwa ahadi za dakitari Slaa zinatekelezeka. Kuna kamati ndogo imeundwa na govt kuanza kutekeleza ahadi za Rais mpya kabla ya kuapishwa.

1. Mabati na saruji vishushwe. Katibu mkuu Viwanda ameshatoa tamko. Ahadi ya dr. Slaa

2. Elimu ya ya lazma la1 mpaka fom6. Prof.magembe amesema walau mpaka fom4 mwaka2012. Ahadi ya dr.

3. Mshahara upande mpaka 325000 tsh. Serikali imepandisha 75% ya kiwango iki. Karibia 40% ya gross salary.

4. Mafisadi wakamatwe. Jeyk kawaweka baadhi pale kisutu!

5. Serikali ya kitaifa na demokrasia. Ukitokea mikumi kwenda kigogo kabla ya kuanza bonde kuna bango kubwa UMOJA WA KITAIFA.

6.wenye dalili za kumwaga damu wakamatwe. Kisena Ccm kampiga OCD katiwa korokoloni.

7. Njama za kuiba kula Tunduma. IGP,kiravu hawakulala waliandaa taarifa kwa wanahabari siku inayofuata. MSIMAMO WANGU: IVI rais anaetoa order kwa sasa ni nani? Rais mtarajiwa au rais anayetawala! Teeh teeh teeh,angalia msije mkampa mbu kazi ya kutibu malaria! Ukiona umeula ujue umeliwa. Mjomba.

Ila angalia sana watawala uyu jamaa mh.SLAA atatoa order makusudi isiyo sahihi alafu dunia iwaone kituko. Slaa naomba uwadanganye kuwa Tz hatuna vita ivo una mpango wa kukodia silaha zote kule iran na Iraq,kesho utasikia wanatangaza tender kuuza silaha zote. Thee thee!uuuwii! Maweee!mbavu jamanii.

Mh.ila subiri ombi ili mpaka baada ya uchaguzi ili tupate ulinzi kwanza! Usku mwema. Bado cku4.
 
hawa hawaitaki

chadema_kids.jpg
 
Ni katika elimu ya lazma kuanzia std1 mpaka fom6. Serikali imetangaza mpaka fom4, by Magembe. Ela ZA EPA zarejea kwa mafungu, saruji ishushwe,apa katibu mkuu ameviagiza viwanda washushe, waleta fujo wakamatwe baada ya tamko Jwtz ,amekamatwa kisena ccm kumchapa Ocd. Du mengi sana na wewe jaza apa,nalala kidogo nkirudi namalizia. Inaletwa kwenu kwa hisani ya Gsana na watu wa JF.
 
Mkurungezi mtendaji wa mtibwa kushughulikiwa ndani ya siku 100 Dr Slaa akiwa madarakani, JK alipopita akaagiza ashughulikiwe.
 
Mama wee! Nimesikiliza sass hivi kwenye mapitio ya magazeti redioni, CCM wamesema elimu ya bure ilikuwa ni sera yao tangu zamani!

These people are very strange
 
Jana usiku nilipomsikia Prof. maghembe anaongea nilicheka mpaka familia yangu wakaniona kama nimepagawa hivi. Yaani kama unataka kuona watu wanafiki nchi hii basi ni CCM. Sera zilezile za CHADEMA ambazo kwenye majukwaa wanasema hazitekelezeki WAMESHAANZA KUZINYUMBULISHA. Yaani ni COPY AND PASTE!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! .

Ama kweli CCM mmeishiwa sera na hamna liolote jipya chini ya mbingu. Pisheni wanaume wa CHADEMA watuboreshee MAISHA mkaendelee na sera zenu za BORA MAISHA.
 
Rudia kusoma Thread, kwani wapi walipoandika ELIMU BURE.

kUTOA elimu toka Msingi mpaka Sekondari kidato cha nne maana yake kila mtanzania atawajibika kusoma mpaka kidato cha NNE. Ni kama serikali ilivysema kuwa mtoto akifaulu kwenda sekondari na mzee akmuozesha au akamkataza kwenda huko kwa sababu ya kuchunga Ng'ombe basi mzee atashitakiwa.

kumbuka sio mzee anamzuia ila hali mbaya ya uchumi mtoto akichaguliwa shule ya kata anatakiwa awe na minimum 70000/= kuweza kuanza shule kwa maisha yaliyowekwa na CCM mzee anakosa hela za kumsomesha ndio maana Slaa akasema Elimu bure kondoa uwezekano wa mtoto kuchunga ng'ombe
 
tofauti ni kwamba, kwa CCM elimu bure ni majengo, enrolment, na walimu wa vodafasta, watoto wahudhuria madarasani bila kujali wanasoma nini. kwa hiyo sidhani kama wametekeleza ilani ya chadema bali wanaichafua.
 
Kwani ulikuwa hujui kama sehemu nyingi kwa kutumia zile shule za kata, asilimia 90 ya wanafunzi wa darasa la saba alikuwa wanaendelea sekondari. Tatizo ni walimu tu ambalo linashughulikiwa.
Hiyo ndio ilikuwa lengo la chama tawala kwa kuanzisha shule za kata.

Hilo lipo Zanzibar kwanini lishindikane TANZANIA BARA?

Hakuna jipya hapo. Au hukusoma hotuba ya mh Kikwete akiliaga Bunge. Ninayo hapa ukitaka naweza kukuwekea. wENZAKO WALILIKUBALI HILO HAPA jf, walicholaumu ni walimu tu. Lakini Rome haikujengwa kwa siku moja.

Miaka 50 bado wanaijenga Roma? tupe CV yako mkuu tusije argue na na kilema wa shule!
 
Back
Top Bottom