CCM Dodoma yapata viongozi wapya akiwemo mwenyekiti mpya Adam Kimbisa

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
[h=3][/h]

Mkoa wa Dodoma umepata mwenyekiti mpya ndugu Adam Kimbisa atakaye kiongoza Chama kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.

Ndugu Kimbisa amepata nafasi hiyo baada ya kupata kura 941 Kati ya kura 1196 zilizopigwa huku mbili zikiharibika.

Katika nafasi hiyo aligombea na wenzake watatu ambao ni mwenyekiti mstaafu wa CCM Mkoa wa Dodoma ndugu William Kusila aliyepata kura 216 na mwenyekiti mstaafu wa wilaya ya Dodoma mjini ndugu Denis Bendera aliyepata kura 30.

Akizungumza mara baada ya matokeo kutangazwa ndugu Kimbisa amewataka wanachama kuvunja makundi yaliyokuwepo wakati wa kampeni ili kwa pamoja waweze kujenga chama.

Awali akifungua mkutano huo wa uchaguzi Mkuu wa mkoa wa Dodoma Dr Rehema Nchimbi ambaye ndie aliyekuwa msimamizi mkuu aliwataka wananchi kuelewa kuwa CCM sio ngazi ya kupanda ili mtu apate uongozi kama ambavyo wengine wanadhani.

Amewataka wanaodhani hivyo kuelewa kuwa CCM sio chama cha kukimbilia Pindi watu wakitaka uongozi.

Leo kikao cha Halmashauri Kuu ya Mkoa kinaketi kwa ajili ya kuchagua Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Mkoa na Katibu wa Fedha na Uchumi.

Ambapo mpaka sasa matokeo yamekuwa ni katibu itikadi na uenezi wa mkoa amechaguliwa Donald Mejiti na katibu wa uchumi na fedha amechaguliwa Mohamedi Rashid Morama.
 
Katika kutathimini mgombea urais wa ccm 2015, nataka kujua kimbisa na mwenzake morama wapo kambi gani ya EL au BM ?
 
MWENYEKITI MSTAAFU? mtu bado anagombea eti ni mstaafu, Gamab ni gamba tu.
 
Lowasa damu damu,mpaka sasa edo kashavuna dodoma,arusha,geita,kgoma,mara...mzee wa kithembe membe ni lindi na dar,matokeo bado yanaendlea kwa mikoa mingne stay tuned.
 
Adam Kimbisa Vyeo Vyake
1. Mbunge wa Afrika ya Mashariki (KIONGOZI wa Hao Wabunge kwa Upande wa Tanzania)

2. Mwenyekiti wa Mkoa wa Dar-es-salaam

3. Udiwani
 
Adam Kimbisa Vyeo Vyake
1. Mbunge wa Afrika ya Mashariki (KIONGOZI wa Hao Wabunge kwa Upande wa Tanzania)

2. Mwenyekiti wa Mkoa wa Dar-es-salaam

3. Udiwani

mkuu udiwani alishaumaliza pamoja na umeya wa jiji la dar, toka 2010, lakini cheo chake kingine haujakitaja ni katibu mkuu wa TRCS (tz red cros society).
 
mkuu udiwani alishaumaliza pamoja na umeya wa jiji la dar, toka 2010, lakini cheo chake kingine haujakitaja ni katibu mkuu wa TRCS (tz red cros society).

Oh Yes... TRCS... Asante Sana!!!
 
Mzee Kimbisa yupo karibu sana na Watawala,kwa umri wake nilidhani kwamba atastaafu siasa kama rafiki yake wa karibu Abdulrahaman Kinana.Huko Mara Makongoro Nyerere ameshindwa kutetea nafasi yake ya Uenyekiti wa Mkoa wa Mara.Nako Tanga Mzee Shekifu ameshinda nafasi ya Uenyekiti wa CCM wa Mkoa.
 
pole sana kaka kusila mkono mtupu haulambwi, mtandao wa kimbisa na lowasa ni balaa, pia warangi wanaoishi dodoma wana umoja sana kuliko wagogo ambao wana makundi ( kundi la kusila, ndejembi,job lusinde na john mallecela na yote hayapendani)
 
Aisee pamoja na kuwa Kimbisa na Kinana ni marafiki wa kubwa but their two different people in ideology, kinana ni mwenye busara sana kuliko kimbisa, halaf kimbisa is after his interest, anahitaji mtu pale anapokuwa na shida yake baada ya hapo hana muda na wewe na kitu kilichomfanya ashindwe kutetea kata yake magogoni na umeya wa dar, ni mtu aliyegubikwa na ubinafsi kwa iyo usishangae tu kuto staafu siasa, hata nafasi ya kuajiriwa ya pale trcs bado anaing'ang'ania kwa umri huo alionao.
 
Thats true Sembuli and majority of them ni wagogo hapo Dom
 
hilo jina kusila linanitian kichefuchef mno nakumbuka alivyowadanganya wananch wa kigwe kwa kusambaza nguzo za cm then baada ya kushinda uchaguz akang'oa.cjaona jipya hapo
 
Aisee pamoja na kuwa Kimbisa na Kinana ni marafiki wa kubwa but their two different people in ideology, kinana ni mwenye busara sana kuliko kimbisa, halaf kimbisa is after his interest, anahitaji mtu pale anapokuwa na shida yake baada ya hapo hana muda na wewe na kitu kilichomfanya ashindwe kutetea kata yake magogoni na umeya wa dar, ni mtu aliyegubikwa na ubinafsi kwa iyo usishangae tu kuto staafu siasa, hata nafasi ya kuajiriwa ya pale trcs bado anaing'ang'ania kwa umri huo alionao.

kila anaeshinda mnasema yuko kambi ya lowasa.watu bana.
Leo kinana amestaafu ghafla kawa mzuri,wakati haohao walikua wanamponda.
Kha...!!unafiki umezidi dunia hii.
 
Back
Top Bottom