Kwa nini tunakua 'exited' wakati hawa sisiem wanapokutana kunywa kikombe cha kahawa!
Kwa nini tunakua 'exited' wakati hawa sisiem wanapokutana kunywa kikombe cha kahawa!
- The dataz ni kwamba wiki nzima hii Muungwana amekuwa akifanyia kazi Lumumba na bila kusema na mtu, ndio maana tunasema kuna jambo huko linakuja, au?
Respect.
FMEs!
Sijakata tamaa na JK ingawa hali ya uongozi wake inakatisha tamaa kila mtanzania mwenye matagemeo. I believe JK atafanya maamuzi ambayo hayajawahi kutokea tangu tupate uhuru. I believe mafisadi wamemshika pabaya sana na sasa yuko tayari kukubali fedheha kuliko kuendelea kujipakulia lawama za wananchi juu ya mafisadi.
JK sasa anafahamu fika kwamba mafisadi sasa wanafanikiwa kuteka JWT kwenye kambi yao.....patamu, tusubiri. JK will act...very soon.
Hivi unaweza kukata tamaa na uongozi wa mtu wakati unaendelea kuwa na imani naye kama kiongozi? Am confused.
Nafananisha kauli hii na ile ya REDET kuwa wananchi wana imani na utendaji wa Rais lakini hawana imani na utendaji wa Baraza la Mawaziri na wanasahau kuwa Rais ndiye mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri na ndiye anayesimamia utendaji wa baraza lake.
Ni wakati muafaka sasa kuhusianisha mtu na uongozi wake ili tuwawajibishe hawa pretenders.
Wildcard mkuu heshima mbele.
Kutawaliwa na CCM si kitu cha kushangilia hata kidogo, Hawa jamaa wote isipokuwa mmoja wanaangalia masilah yao na watoto wao tu na hawana kazi nyingine. Nchi yetu hali ni mbaya ukiangalia kwenye viashiria vyote vya Taifa Imara. Inflation 12% Ndullu yupo tu, Ada za shule za watoto wetu tunatakiwa kulipa kwa dola ( kama vile tuko marekani) wakati mishahara yetu ni kwa Shilingi. Malalamiko kila kona, ujambazi umeongezeka mwingine unawahusisha mapolisi (mfano ukerewe), ajali za barabarani zinaongezeka kila kukicha, wizi wa mali ya umma, Raisi kudanganywa hadharani kila siku (mfano Ufunguzi wa hoteli-Arusha, Kukabidhi Gari Ikulu, Uzinduzi wa malaria basi-THT na sasa Udanganyifu kwenye sheria iliyopitishwa na bunge). Raisi anatokea hadharani kwa mbwembwe kwa issue ambayo baadae inaonekana ni usanii mtupu.
Wildcard haya yote hayana wa kuyaongoza, kuelekeza, au kusimamia sheria. CCM ni kiama chetu sote Tunaoipenda na Tunaoichukia. usishangilie hata kidogo.
Hii inanikumbusha nikiwa JKT. Watu wanakamatwa na kuwekwa Lupango (jela ya jeshi). Wakiwa ndani ya Lupango, wanasikia kishindo cha buty na wanaanza kubishana:
Kuruta1. Huyo atakuwa Afande Manyirizu.
Kuruta2. Hapana huyo atakuwa Captain Wawa.
Kuruta3. Hamna kitu, huyo kwa vyovyote ni Afande Magwega.
Si tusubiri tu siku ifike tutasikia kilichotokea? Na hasa CCM ambayo siku hizi vikao na mafaili yao yanamatundu yanayovujisha habari bila hata ya kuombwa. Sijui huwa wanauza hizi habari au wenyewe tu wanabadilishana na Waandishi wa habari kwa makubaliano kuwa waje wapigiwe debe?
Mkuu Fidel, hivi inakuwaje hii tabia ya kufunga mtaa mzima eti kwa sababu fulani yuko jengo fulani au anapita? Mtaa unakuwa umefungwa muda wote wakati yeye yupo pale au kwa muda tu?
Dr. Slaa, hivi CHADEMA mna mpango gani wa kuja kupanga muda ambao POLISI wanaweza kufunga barabara wakati kiongozi fulani anatarajiwa kupita? Hii tabia ya kufunga barabara ambazo mkuu fulani atapita kwa kweli inaumiza sana wananchi. Wakati Kigogo ndiyo kwanza anaingia bafuni kuoga, aje apate kifungua kinywa na ndiyo aondoke, Polisi huku wao tayari wameshafunga barabara. Hivi haziwezi kufungwa dakika 5-15 kabla? Si itatosha kabisa kusimamisha na kuweka magari pembeni? Ikibidi, basi Chadema wapendekeze Rais anunuliwe Helcopiter. Na mwisho itakuwa safi tu maana anapenda sana kuruka. Kuna haja sheria za ufungaji barabara ziwepo na si watu wanajiamulia tu kufunga kwa muda wanaotaka kwa sababu tu hawataki kufanya kazi ngumu/kazi ya ziada. Na kama sehemu hiyo si salama, basi watafute sehemu iliyojitenga na salama na wafanyie vikao vyao/mikutano.
JK must wake up, and I pray he does. He must appreciate absence of life-long friend or enemy in politics. In politics friends can be just as deadly as enemies and so they should be treated....kama mafisadi wamefikia hatua ya kupata support ya wanajeshi crisis bells must go off and president must act. I live to think he will act, I don't want to think otherwise.
I wish you all the best as you continue with your day dreaming. Huwezi kumbadilisha chui madoa yake kwa kuomba dua.