CCM dhambi ya ubaguzi imeanza kuwatafuna, very soon watajizika wenyewe

Kuna mbunge mmoja alisikika siku za karibuni akitoa kauli za kibaguzi na kichochezi katika bunge la katiba (BMK) na kushangiliwa sana na wabunge wa CCM. Nilishangaa sana kuona wabunge wenye akili zilizotimia wakishabikia dhambi hii ya ubaguzi. Huyu ni mbunge wa CCM kutoka upande wa Zanzibar. Alisikika waziwazi akisema kwamba mapinduzi ya Zanzibar yalifanyika katika kisiwa cha Unguja na kwamba kule Pemba ilipelekwa bendera tu. Hakuishia hapo tu-aliendelea kuapa kwamba wale wasiotaka Muungano wa serikali mbili warudi "kwao". Aliendelea zaidi kudai kwamba hati ya muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar imepatikana, sasa hao watu (Wapemba) aliowataka warudi kwao (Uarabuni) sasa waanze kudai hati ya Unguja na Pemba. Na safari zote alipokuwa akitamka maneno haya alikuwa akishangiliwa kwa nguvu sana na wanaCCM wenzake!

Kauli za chuki na za kibaguzi kama hizi sio za kushangilia wala kushabikia hata kidogo. Inakuwaje wana-CCM wamshangilie mtu anayetaka kubomoa umoja na mshikamano wetu badala ya kumkemea eti kwa sababu ni "mwenzao" na kwa kigezo kwamba wao ndio wanaotawala na hakuna mtu wa kuwahoji? Nchi hii ikimwaga damu kwa sababu ya kauli za kiintarahamwe kama hizi ni nani atakyebaki salama? CCM mnapaswa wakati mwingine kujifunza kutumia akili badala ya kutumia viungo tofauti na ubongo. Mmepewa akili mzitumie kuchanganua mambo sio kufugia nywele!

Sasa endeleeni kuchezea amani, siku likibumbuluka msitafute mtu wa kumlaumu. Hatuwezi kuvumilia kuona wajinga wachache wakiitumbukiza nchi katika vita huku tukiwa tumekaa kimya. Ni wazi vita ikitokea ktk nchi hii watakaoathirika ni wananchi masikini wasiokuwa na uwezo wa kuikimbia nchi. Watu wa CCM mmeishavuna pesa za kutosha kupitia kwenye ufidsadi. Ikitokea vita mtapanda ndege na kukimbilia nje ya nchi. Mistake kupalilia chokochoko ambazo zitakuja kugharimu maisha ya walalahoi huku watoto wenu mkiwatorosha kwenda nje ya Tanzania.

Tafakari, chukua hatua!
:yield:
Umekaa ukaona kwako hii nayo mada ya maana wewe unatofauti gani na hawa.
 
Chadema ukabila umewala mpaka mmeanza kupakazia wengine mnaenda mpaka kuroga kibaha mlingotini lakini bado ccm inawagonga tu.
 
Mtahangaika sana kuichafua ccm chama kinachopendwa sana na watz wote lakini hamtafanikiwa

Labda kinapendwa na ukoo wa panya na wewe ukiwa kapanya kadogo. Watanzania wapi unaowasema? mimi ni mtz mbona nahisi kutapika nikisikia jina ccm, kila aliyenizunguka haipendi ccm wewe unaongea kwa niaba ya nani? labda ukoo wenu wa panya
 
Nyie ukawa mlipoanza dharau, kejeli, na mbwembwe mlidhaniaje. Siasa za Zanzibar ziko very complicated kuliko mnavodhani nyie. Wakitoka kwenye hoja ya serikali tatu watahamia kuhoji serikali ya mapinduzi ya Zanzibar. Hawawezi kuachiwa bila kuambiwa. Ni lazima wapashwe kwa lugha kali ili wafahamu kuwa hila zao zinajulikana. Wajumbe wa Zanzibar wanaoipigania serikali ya Tanganyika kinawauma nini? Kama wanaona maslahi yao yameisha waseme hawautaki muungano sio kutusemea sisi watanganyika, sisi tukiitaka hatuitaji msaada toka nje. Jussa na wenzake wafahamu.

Kama kimsingi Pemba ina haki kisheria ya kuwa ilitakiwa iungane na Unguja kisheria na haikuwa hivyo basi ni haki yao wahoji. Tena haraka. Na kufanya hivyo siyo dhambi. Ni kutaka mambo yaliyokosewa hapo awali yawe sawa. Sioni kwa nini tunawatisha watu hapo.

Nadhani hapa tishiao ni kauli za kibaguzi na za kejeli, kwa kuwaita wengine wapemba na waarabu. Hasa pale unayemwita hivyo akiwa ni mbunge aliyechaguliwa na anayewawakilisha watu. Hii ni kudharau mpaka waliomchagua au kumteua. Na hii ndiyo itakayoleta madhara. Siyo kudai uhalali wa na hati za miungano.
 
Ukiwa na mvuta bangi anafanya vibweka dawa yake ni moja tu, ni kumwambia wewe umevuta bangi ndio anarudi kwenye sense. Historia ya hawa kina Jussa kubeza mapinduzi haikuanza leo. Waliyabeza watu wakawakinai wajawapa za uso sasa wanalalamika. Kuhoji muungano sio kitu kibaya, kitu kibaya ni dhamira zilizojificha kwa wanasiasa ambazo tayari ziko wazi. Kina Jussa wanataka kudhoofisha muungano then wadhoofishe serikali ya mapinduzi wasiyoipenda. Wamejaribu kuingia direct wakashindwa sasa wanaingia indirect. Waunguja wanafuatilia kwa karibu kinachoendelea, Jamsheed amekaa kando anaangalia mpambano unavoendelea. Wananchi wa unguja lazima wawe na shaka as ardhi ilikuwa ya sultani. Wanastahili kuwa wakali.
 
"tumechoka ubaguzi, hatuwezi kuwa sehemu ya kundi la intarahamwe linalohamasisha ubaguzi ndani ya tanzania" prof. Lipumba-2014 ndani ya bmk.
 
mtei na chadema yake iliyojaa wakristo wanawabagua waislamu na watu wasio katika kabila la wachaga wasiotoka kaskazini. Lukuvi anaogopa uislamu usije kuwa na nguvu zanzibar, huku anawatukana wapemba. Kweli wakristo wengi mmeiva sana kwa mafunzo ya chuki na ubaguzi mnayofundishwa kanisani.

acha udini weeee simama kwenye hoja. Jazba jazba jazba zinakukimbizia kuwaza udini!! Hata hiyo dini yenyewe upo bora liende...acha wenye imani zao waseme. Ebooo!!!
 
ilikuwepo au imepatikana? imepatikana kutoka wapi ilhali miaka yote hii kuna watu wanadai angalau waione na wameambulia patupu? wameipata kutoka wapi?

kama kawaida yao baada ya kumaliza kuichakachua ndipo wameitoa hadharani. hawa watu ni wa kuogopwa kama ukoma!
 
Karum e alifanya referendum ya Muungano wa Tangayinka na Zanzibar kupitia RADIO Zanzibar, kwa kuwauliza Wazanzibari wote mara 3 kama wanautaka Muungano? Wazanzibari wote wakaitikia kwamba NDIYO tunautaka muungano. (mjumbe mmoja wa BMK kutoka Zanzibar). Ili upate raha ya kichekesho hiki, operating word ni RADIO na kuitikiwa NDIYO!

heee! ama kweli hawa watu wameishiwa hoja. wanaropoka utadhani vichaa waliotoroka tiba kutoka milembe!
 
Kumbukeni wenje,bashe,ulimwengu waliambiwa sio raia wa tanzania wali baguliwa

mwisho wa ubaya ni aibu. sasa uchochezi, ukasuku, unafiki na uzandiki wa CCM umebainika wazi--wanatafuta mahali pa kuficha nyuso zao hawapaoni. na kila mtu wanayekutana naye wanamuona mbaya.
 
Tatizo mntaka mseme ninyi tu..... Wakisema engine mnalalamikaje!!! Kilichoonyeshwa name kusemwa na wana CCM ZANZIBAR ni like ambacho KIKO MIOYONI MWA WAZANZIBAR KWA KARNE KADHAA. hofu wanayoiongelea wanna ccm Zanzibar, ni hofu iliyodumu mioyoni mwao kwa miaka mingi.remember..." It's not the fear of death but it's the fear of living"" hat a nyie wajinga mnalijua hili lakini kwa sababu dhamira yenu ni kuona nchi ikiwa destabilized....... Hatuwashangai.
Safari hii hamtapata Democratic privileges eti HAKI YA KUANDAMANA!!!! we will wipe you from the streets and annihilate you completely

halafu mkiitwa INTARAHAMWE mnakataa mi nadhani mna majivu sehemu inayotakiwa kukaa ubongo.
 
ilikuwepo au imepatikana? imepatikana kutoka wapi ilhali miaka yote hii kuna watu wanadai angalau waione na wameambulia patupu? wameipata kutoka wapi?

Hahahaha!!! Nimependa imepatikana kutoka wapi? Ilikuwa kwa interahamwe.
 
Kwa ufupi CCM itaendelea kuitawala nchi hii miaka mingi ijayo kwa kuwa wanaoshindana nao ni waoga wa hoja.

Wale ukawa hoja zao zinanguvu sana bila wao hakuna katiba.ukawa siyo woga ni jasiri sana wangekuwa woga wasingelitoka ndani ya bunge la katiba.waoga ni ccm wanaopingana na maoni ya wananchi.

Waulize hao ccm wako wanaogopa nini kuvunja bunge twende kwa wananchi tukawaulize hayo maoni ni ya kweli au uongo? Kama siyo waoga wambie waje kwetu mtaani wajilidhishe waupate ukweli.ukawa wamesema wanakwenda kwa wananchi kama wangekuwa waoga wangeenda kwa wananchi? Nakuuliza wewe chuki? Njooni kwa wananchi tupate muafaka acheni kutafuna posho
 
Tatizo mntaka mseme ninyi tu..... Wakisema engine mnalalamikaje!!! Kilichoonyeshwa name kusemwa na wana CCM ZANZIBAR ni like ambacho KIKO MIOYONI MWA WAZANZIBAR KWA KARNE KADHAA. hofu wanayoiongelea wanna ccm Zanzibar, ni hofu iliyodumu mioyoni mwao kwa miaka mingi.remember..." It's not the fear of death but it's the fear of living"" hat a nyie wajinga mnalijua hili lakini kwa sababu dhamira yenu ni kuona nchi ikiwa destabilized....... Hatuwashangai.
Safari hii hamtapata Democratic privileges eti HAKI YA KUANDAMANA!!!! we will wipe you from the streets and annihilate you completely

kwa hivyo huyu mCCM aliyetoa kauli za kichochezi alikuwa anataka ku-destabilize nchi? kwa manufaa ya nani? bunch of twits!
 
Chadema ukabila umewala mpaka mmeanza kupakazia wengine mnaenda mpaka kuroga kibaha mlingotini lakini bado ccm inawagonga tu.

kuna huna hoja ni bora ukakaa kimya. ina maana haya maneno ni ya kupakazia? hayajawahi kutamkwa mahali popote? a twit at work!
 
Back
Top Bottom