Ndoa
JF-Expert Member
- Dec 2, 2011
- 1,033
- 253
leo nimeamini kwamba viongozi wengi wa ccm ni wajinga na mbaya zaidi wameamua kupambana na lowasa mwerevu.
How comes viongozi wa ccm (wakiongozwa na nape) wanamwogopa hivi lowasa? Kama lowasa ni mchafu hivi iweje viongozi wa ccm ( sitta, chiligati na nape) wanatumia njia za majungu, fitna, njia zisizokuwa za moja kwa moja kupambana na lowasa?
1. Juzi tumeshuhudia ccm wakifanyia mabadiliko katiba yao wakiweka vihunzi vingi lakini kwa mjanja ukiangalia lengo ni kupunguza nguvu za lowasa kuelekea 2015, hivi lowasa asipogombea urais 2015 kwa sababu yeyote ile ( aaamue, afe au hata augue) ccm watarudi kurekebisha katiba yao tena? Kama wanaamini kwamba lowasa ni mchafu kiasi hicho kwa nini wasimkamate au kumfukuza uanachama badala yake wanatumia njia za kumvizia/ uoga huu una nini? Au wamegundua aliye mchafu si lowasa?
2. Tumeona kura za maoni arumeru mashariki jinsi sioi sumari alivyotakiwa kutoswa kisa eti ana unasaba na loawas. Hivi chama chenye jeshi, polisi, mahakama, takukuru kimefikia hatua ya kuogopa kivuli cha lowasa kwa namna hii kweli? Walianza akina nape na kina chatanda kupiga majungu ya utata wa uraia wa sioi lengo lao likiwa kumtosa mkwe wa laigwanan wa kimasai. Cc nayo ikaingia mkenge ila ikatumia busara kidogo ya kurudia uchaguzi huku wakiamini kwamba sioi angeshindwa. Mpaka nimefikia sasa na mimi naanza kuamini kwamba tatizo la lowasa si ufisadi bali urais 2015 na kuna watu wameshagundua "werevu wa mtu huyu"
nape, chiligati, mwigulu onesheni uanaume wenu acheni kutumia indirect method kupambana na lowasa kama hamna uhakika na tuhuma zake mwacheni.
Kuna mpuuzi mmoja leo ameleta mada juu ya lowasa kuumbuliwa na takukuru arumeru, mada ilichangiwa na watu wengi sana wakiamini utunzi wa mpuuzi yule.
Wajanja walishagundua kwamba akina nape walishagundua nguvu ya lowasa wakaanza kuleta propaganda zao ili baadae sioi akishinda ionekane ni nguvu za pesa.
Hivi kweli lowasa atume sms kuagiza mtu akatoe rushwa? Lowasa ambaye ccm ya akina sita inatafuta namna ya kumtoa ccm lakini inashindwa?
Haya sasa sioi ameshinda ni jukumu sasa la akina nape kwenda kushirikiana na lowasa kuhakikisha kwamba mkwe wa lowasa anashinda arusha
kitu pekee ninachokiona hapa na mods naomba muweke maneno yangu haya kama kumbukumbu " mwaka 2015 lowasa ahatagombea urais ila ccm itamtegemea sana lowasa kama ilivyomtegemea mwalimu nyerere kushinda 1995" sina lengo la kumfananisha lowasa na mwalimu ( lowasa ni mchafu kama walivyo wachafu wote wa ccm) la hasha ila kwa sasa ndani ya ccm loawas ndiye mwana siasa mwenye mvuto ndani ya ccm na amini usiamini nyota yake imeng'azwa kwa fitna za akina nape, sita, mwakyembe na wengine na amin amin nawaambia katika wote hao hakuna anayeweza kuthibisha uchafu wa edward pasipo kumhusisha nwenyekiti wa chama ndiyo sasa wameamua kutumia njia za uoga kupambana na lowasa
hata nyere pia alikuwa mchafu wa siasa, alichangia kubatilisha ushindi wa wapinzani kule zanzibar.