CCM Dar yapata Mwenyekiti Mpya; ni Ramadhani Madabida

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
SOURCE Faustine Ndugulile FACEBOOK

Results out: Ramadhan Madabida is the new Dar Es Salaam CCM chairman. Congrats!

Awali Madabida alijikuta katika wakati mgumu wakati akijinadi baada ya mjumbe mmoja kumuuliza swali kuhusiana na kiwanda chake kudaiwa kutengeneza dawa bandia za kupunguza makali ya Virusi vya Ukimwi za ARV.

Hata hivyo, Msimamizi wa uchaguzi huo, Assa Simba alimzuia Madabida kujibu swali hilo akisema kwamba haukuwa wakati wake.

Awali, akifungua mkutano wa uchaguzi huo, Makamu wa Rais, Dk Gharib Bilal alisema kuwa chama hicho kimelenga kurudisha majimbo yake yote yaliyochukuliwa na wapinzani katika Uchaguzi Mkuu wa 2015.

"Natumaini uchaguzi utakuwa wa haki bila vurugu zozote, nawaomba msiwe na wasiwasi kwani chama chenu kipo imara kuwakabili wapinzani," alisema Dk Bilal.

SOURCE: MWANANCHI
 
kambi ya Membe hiyo, guninita aliyeanguka alikuwa wa lowassa
 
Kazi sana...sasa atatengeneza ARV za sembe sasa!hakuna wa kumshika!si anakata fungu kwa mabwepande kuwawezesha kuendesha chama?aahh atauza sana sembe lake
 
Hawa CCm mbona wanashangaza sana yaani huyo muuaji anapewa uongozi tena wa jiji la Dar. Mtengenezaji ARV fake awa kiongozi to hell with magamba. Ukiwauliza watakuambia lete ushahidi wa uuaji wake. Ukweli ni kwamba watu wa Tz wanaelewa kuwa watawala (sio viongozi kwa sababu hatuna viongozi Tz) hawatutendei haki. Kwamba wanatumia mabavu, usanii, kiburi, pesa, na ubabe kuendelea kutawala. Yaani hawana political legitimacy. Wenyewe wanafikiri Watz ni wajinga sana I think the reverse is true and the day will come, it is just around the corner wakamwulize hayati mobutu kuku wazabanga.
 
mambo mengine ccm wanajitakia kulikuwa kuna ulazima gani wa huyu jamaa (r.madabida) si tu kumchagua kuwa m/kiti hata tu kupitisha jina lake kwenye hio nafasi ikizingatiwa currently scandal inayomkabili kama si kuendelea kujilimbikia kashfa na kukichafua chama
 
BILI KASHFA ccm hawakubali. chama chao kimekosa muelekeo hadi hawajui nini wanakitaka.wanasababu gani ya kumchagua mtu ambaye kwa upande mmoja amechafuka?? kweli sikio la kufa halisikii dawa.
 
Sasa ARV ataacha kudeal nazo?

Awali Madabida alijikuta katika wakati mgumu wakati akijinadi baada ya mjumbe mmoja kumuuliza swali kuhusiana na kiwanda chake kudaiwa kutengeneza dawa bandia za kupunguza makali ya Virusi vya Ukimwi za ARV.

Hata hivyo, Msimamizi wa uchaguzi huo, Assa Simba alimzuia Madabida kujibu swali hilo akisema kwamba haukuwa wakati wake.

Awali, akifungua mkutano wa uchaguzi huo, Makamu wa Rais, Dk Gharib Bilal alisema kuwa chama hicho kimelenga kurudisha majimbo yake yote yaliyochukuliwa na wapinzani katika Uchaguzi Mkuu wa 2015.

"Natumaini uchaguzi utakuwa wa haki bila vurugu zozote, nawaomba msiwe na wasiwasi kwani chama chenu kipo imara kuwakabili wapinzani," alisema Dk Bilal.

SOURCE: MWANANCHI

***Angalia
Sasa hata Makamu wa Rais anamwona Madabida anafaa pamoja na WIZI na Madawa fake...
 
Duh, CCM ina wenyewe wenye roho ya jiwe hata haya hawana, mtu mwenye 'tuhuma' nzito za dawa feki ilitakiwa ajiondoe mwenye kwenye uchaguzi na akibisha chama chake na viongozi wake hapa chini kilitakiwa kimuondoshe kwenye uchaguzi.

Mwenyekiti wetu kazi uliyonayo ni kurudisha majimbo yetu tuliopoteza
 
Hili ni pigo lingine kwa CCM...wao wanadhani wamepata kumbe wamepatikana.....wananchi si wajinga....mtu anatengeneza dawa bandia na kusababisha kupotea kwa uhai wa watu wao wanamchagua kuwa kiongozi... Si ni MAJANGA HAYA?
 
Back
Top Bottom