CCM-CUF waungana kupinga mswada wa mafao ya wastaafu Zenj

Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,883
6,884
CCM, CUF wapinga muswada wa mafao ya viongozi

WAJUMBE wa Baraza la Wawakilishi kutoka CCM na CUF wameupinga muswada wa maslahi ya mafao ya viongozi wa kisiasa na kusema kwamba utawabebesha wananchi wa Zanzibar mzigo mkubwa.

Mwakilishi wa Jimbo la Magomeni ambaye pia ni Katibu wa wajumbe wa CCM katika Baraza la Wawakilishi Salmin Awadh alisema wananchi wameukubali mfumo wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa kwa matarajio makubwa ya kuimarisha hali zao za uchumi na maendeleo.

Lakini Salmin alisema kwa mujibu wa hali inavyokwenda inaonesha wazi wazi kwamba matarajio ya wananchi katika kupiga hatua ya maendeleo yameanza kuyeyuka kidogo kidogo.

“Mimi siungi mkono mswada huu kwa sababu hauna maslahi ya wananchi wa Zanzibar...huu si wakati wa kuanza kujipangiya maslahi makubwa ya viongozi wakitaifa wakati wananchi wetu hali zao ni duni,”alisema Awadh.

Mwakilishi wa Jimbo la Chonga kwa tiketi ya CUF, Abdallah Juma Abdallah yeye alisema wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wanavunja Katiba kwa sababu wanatakiwa kuupitisha mshahara wa Rais lakini kazi hiyo haifanyiw na wajumbe.

“Kwa mujibu wa Katiba, mshahara wa Rais unatakiwa kuidhinishwa na Baraza la Wawakilishi lakini mimi nipo mwaka wa 14 sasa sijapata kusikia kuidhinishwa kwa mshahara huo,” alisema.

Alisema wananchi wanakabiliwa na matatizo mbalimbali ambayo ni ya msingi ikiwemo huduma za afya na elimu ambazo bado hazijatekelezwa kwa ufanisi. Mwakilishi wa Viti Maalumu, Raya Suleiman (CCM) alisema huu si wakati muafaka wa kupitisha mafao makubwa na manene ya viongozi wastaafu wa serikali.

“Tusubiri hadi uchumi wetu utakapokuwa mzuri na kustawi ndipo tuanze kuwekeana maslahi makubwa ya mafao ya viongozi wastaafu wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar,” alisema Raya.
 
"Kwa mujibu wa Katiba, mshahara wa Rais unatakiwa kuidhinishwa na Baraza la Wawakilishi lakini mimi nipo mwaka wa 14 sasa sijapata kusikia kuidhinishwa kwa mshahara huo," alisema. ??????????
 
"Kwa mujibu wa Katiba, mshahara wa Rais unatakiwa kuidhinishwa na Baraza la Wawakilishi lakini mimi nipo mwaka wa 14 sasa sijapata kusikia kuidhinishwa kwa mshahara huo," alisema. ??????????


Dah!Kwa Mh. Salmin Awadh ni miaka kumi na nne, na kwa wengine wameona katiba ikikiukwa mara ngapi na ni hatua gani zimechukuliwa!..Je Tutafika kwa mtindo huu wa mtu kuapa atailinda na kuitetea katiba afu tena ndo anakuwa wa kwanza kuisingina...Lol!TUNAHITAJI MABADIRIKO YA KWELI...
 
kazi kweli, wanaungana mara ngapi kwani si walishaungana tangu wafunge ndoa yao ya mikeka
 
Dah!Kwa Mh. Salmin Awadh ni miaka kumi na nne, na kwa wengine wameona katiba ikikiukwa mara ngapi na ni hatua gani zimechukuliwa!..Je Tutafika kwa mtindo huu wa mtu kuapa atailinda na kuitetea katiba afu tena ndo anakuwa wa kwanza kuisingina...Lol!TUNAHITAJI MABADIRIKO YA KWELI...

Moto uliowashwa Zanzibar utavuka bahari hadi bara, mkulu wa Magogoni hadi kieleweke mshahara, posho na malupulupu yaeleweke kikatiba maana sisi walipa kodi ndio tunaonyongwa tujue pesa zetu zinavyotumika.
 
Mimi nadhani wako sahihi kwa sababu kuongoza mafao kwa wastaafu ni mzigo kwa mlipa kodi !
 
Back
Top Bottom