Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM = Chama cha mafisadi!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kalamunzu, Apr 18, 2011.

 1. K

  Kalamunzu Member

  #1
  Apr 18, 2011
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hapana shaka kwa kudai kujivua gamba CCM imedhihirisha kwamba ni "genge la mafisadi". Ukweli unaopatikana kwenye nukuu za viongozi waandamizi wa chama hicho unatoa taswira ya moja kwa moja kwamba CCM imemezwa na ufisadi. Japokuwa wameanza kujinadi na kujifanidi kwamba chama hicho hakiwaogopi mafisadi; bado ukweli utabaki palepale kwamba CCM inaendeshwa na mafisadi na mafisadi wamekishika chama hicho kwa "nguvu kubwa" na wanakitumia kwa maslahi ya kifisadi. Mwanzo nilitegemea kwamba, Mwenyekiti wa CCM Taifa angaliwataja na kisha kuwaamuru watu watatu wa mwanzo kuondoka CCM, nao ni:

  1. Rostam Aziz
  2. Edward Lowassa
  3. Andrew Chenge
  Hawa watatu wana mtandao unaoanzia kwenye mashina, matawi, kata, wilaya, mikoa na hata taifa. Na zaidi mtandao unaoongozwa na fisadi Edo Lowassa una mizizi yake kwenye UVCCM ya akina Beno Malisa. Msimsahau Hussayn Bashe (Msomali wa Nzega)...huyu kijana anatumiwa na Rostam Aziz katika kufanikisha mipango ya ufisadi wa kuutumia UVCCM kwa maslahi ya mtandao unaotamani kushika dola 2015.

  Pamoja na yanayoonekana wakati huu ndani ya CCM, ukweli utabaki palepale kwamba:

  • JK aliwapa muda mafisadi wamnufaishe kwenye kampeni zake;
  • JK amewahakikishia mtoko wa salama mafisadi kwa kuwaacha waamue kutoka au kubaki;
  • JK ametoa ruhusa kwamba kama CC na NEC wanaweza basi wawafunge pake kengele; na
  • JK anawaogopa mafisadi waliyemsaidia kupata alichotaka 2005 na kwa jinsi hiyo hawawezi.
  CCM imefikia ukingoni na changamoto za ufisadi na mafisadi zinakaribia kukimaliza chama hicho. Na kwa vyovyote viwavyo:

  CCM = CHAMA CHA MAFISADI!
   
 2. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #2
  Apr 18, 2011
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 12,918
  Likes Received: 1,160
  Trophy Points: 280
  1.ccm iwataje hao mafisadi na matendo waliyoyafanya wakaitwa mafisadi.2.jee hizo tuhuma kwa mafisadi ni kweli au laa?3.hatua walizochukua kama chama ni zipi juu ya mafisadi?vinginevyo wanajisafisha kiunafiki
   
Loading...