CCM,CHADEMA wavutana Iringa

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,534
13,225
Mvutomkubwa unaotokana na itikadi za kisiasa, umeibuka mbele ya Makamu wa Rais, Dk.Mohamed Gharib Bilal kati ya wafuasi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), muda mfupi baada ya Mbunge wa Jimbo la Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa, kupanda jukwaani, akikituhumu CCM kuteka mikutano ya serikali hasa wanapokuwapo viongozi wa kitaifa.

Alidai kuwa CCM wamekuwa wakiweka bendera zao katika mikutano hiyo wakiwa wamevaa sare za chama hicho pasipo kujali mikutano hiyo inawahusu wananchi wote.

Msigwa aligeuka nyuma ya jukwaa hilo na kumwomba Dk. Bilal, na yeye awasilimu wakazi wa mji wa Iringa kwa salaam za Chadema, kwa kuwa wao hawakupata nafasi ya kuweka bendera zao wala kuvalia mavazi ya Chama chao katika mkutano huo.

Mvutano huo, uliibuka wakati Mchungaji Msigwa alipoombwa na Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Asseri Msangi kupita mbele ili awasalimu wananchi.
Alipomaliza kutoa tuhuma hizo, Msigwa alimwomba Makamu wa Rais, amruhusu kuwasalimu wananchi kwa falsafa ya chama chake na ndipo alipokunja ngumi na kuwasalimu wananchi hao kwa salaam ya ‘Peoples Power' huku wananchi waliokuwa wamefurika katika uwanja wa Mwembetogwa wakilipuka kwa sauti kubwa ya Power, Power!
Baada ya salaam hizo, alimweleza Makamu wa Rais kwamba kwa kuwa na yeye (Msigwa) ni Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Iringa, angeamua kuwaambia wananchi wake wabebe bendera zao au kuvalia kombati za chama chake ingekuwa balaa.

Hali hiyo haikuwapendeza viongozi wa CCM jambo ambalo lilimlazimu Katibu wa Chama hicho mkoa wa Iringa, Mary Tesha, kupanda jukwaani na kutoa ufafanuzi kuhusu bendera tatu za chama hicho zilizokuwa zikipepea uwanjani hapo sambamba na bendera ya taifa.

"CCM Oyeee! Mheshimiwa Makamu wa Rais siyo kweli kwamba tumekuwa tukiteka ziara wala kuipora mikutano ya serikali kwa kuweka bendera zetu. Hata mheshimiwa mbunge (Msigwa) anajua kwamba Makamu wa Rais amekuja kukagua miradi inayotekelezwa kwa ilani ya CCM…Hii ni fahari kwetu na lazima na sisi tuwepo kwa kishindo," alisema Tesha.

Source:Nipashe
 
Msigwa yuko :poa sana.
Anatakiwa mtu anayejiamini kwa kiasi cha juu namna hiyo, kuliko kuwa kondoo unayechekelea kila kitu...!
Who is makamu wa raisi hadi aogopwe kama SIMBA?

Peopleeeeeees....................Poweeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeerrrrr!
 
Msigwa yuko :poa sana.
Anatakiwa mtu anayejiamini kwa kiasi cha juu namna hiyo, kuliko kuwa kondoo unayechekelea kila kitu...!
Who is makamu wa raisi hadi aogopwe kama SIMBA?

Peopleeeeeees....................Poweeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeerrrrr!

nahisi kama ungesema haya mbele ya yanga, hasa sentesi ya pili kutoka mwisho.
 
Hongera msigwa kwa kuonyesha njia, yafaa viongozi wakiserikali wafanye mambo ya serikali na wala sio ya chama.hili limesababisha hata mvuto kukosekana kwa serikali kwani kiongozi anapokuja kwenye ziara ya shughuli za kimaendeleo anakuja kimagamba na wananchi wasio wa kimagamba wanasusia shughuli hizo.wawe serious na mambo yamsingi ngoja waendelee kuumbuka, i hope wataacha.
 
Mh. Msigwa hapo sawa mpaka kieleweke. Democracia mbele heshima ya kinafiki kwa makamu wa rais kwa cdm ni mwiko. Nimeipenda sana hii saikologia ya msigwa tofauti na yule mnafiki wetu Z. Kabwa anayekubaliana na magamba na kushirikiana nao bega kwa bega kana kwamba sera zao na itikadi yao ni moja ile hali sivyo.
 
I lyk this dude msigwa!! Worms ar now feasting in ccm genitals!! Jus a matter of time!!
 
Kamanda Msigwa ni jembe la kujivunia. Wana Iringa tusimame imara dhidi ya hila za huyu mwovu `ccm`. Free dom is comming to moro!!! Peoplesssssssssss...........!
 
Back
Top Bottom