CCM, Chadema wachapana makonde mbele ya waziri

Akili ya panzi kabisa,siku hizi waziri yuko kwenye ziara za kiserikali anatembea na mabaunsa wa CCM,hapo kilichofanyika ni kupandikiza chuki,hata mm nimechukizwa na kitendo cha huyo dogo kupigwa pasipo sababu,ni uonevu huo,ni hali ya kujidai kuwa CCM wako juu ya sheria,ole wenu nyie CCM na ufisadi wenu,hakika Mungu hajala,na siku zenu zinahesabika

argument yako ni kitoto sana.kwani aliyeanza vurugu ni nani?au una mtindio wa ubongo brother.
 
Siyo kuvaa tu kijani bali alikuwa akitumia magari ya serikali kwenye shughuli za chama

wewe hata huelewi kinachoendelea,kaa chini wenzako wenye hoja za maana waongee.umeambiwa vijana wa chadema walianza kuuzomea msafara wa kiongozi ndipo vijana wa ccm waliovaa tisheti nyeupe wakawaangushia kipigo cha mbwa mwizi.
 
Kwa mujibu wa habari hii:

1 - Kwa nini mabaunsa wafanye kazi ya ulinzi wakati polisi walikuwepo?

2 - Ni kosa la kisheria kwa raia mmoja kumpiga raia mwingine au raia kupigana. Kwa nini aliyepelekwa kituoni ni kijana aliyepigwa na si waliompiga?

3 - Ukiangalia utaona kuwa hata waziri hafahamu utawala wa sheria; badala ya kuamuru wote waliohusika wakamatwe kwa mujibu wa sheria anabakia "kuomba" polisi waimarishe ulinzi haraka. Sheria inapovunjwa hakuna maombi, ni amri tu, ndiyo maana polisi wanaitwa law enforcers.

4 - Yaleyale ya kila siku, ziara ya kiserikali halafu wananchi wanaipaka rangi ya siasa na kiongozi mhusika anaangalia tu, bila ya kujua nini cha kufanya.


Ukiwa ni mwana CCM mpambe hata ukiua mtu Tanzania hakuna utawala wa sheria kwako .Kuna mifano mingi sana hapo Tanzania kuanzia wezi na wauaji lakini kwa kuwa ni CCM hawaguswi .Wahindi wote ni CCM unaona wanaguswa ? Wanauza hata madawa ya kulevya lakini umesha sikia hata wakiandikwa ? Mauaji mengi na hata OCD kule wapi alipigwa mtama na mgombea wa CCM hadi sasa hakuna lolote .Huu ndiyo utawala wa walio lewa madaraka mkuu .
 
Back
Top Bottom