Ccm, chadema, serikali, mashirika ya haki za binadamu.

Logo

JF-Expert Member
Jan 26, 2011
588
48
Habari Wana JF,
Nina masikitiko makubwa na majonzi makubwa sana, nimejaribu kufuatilia kwa kila hali kutaka kujua CCM, CDM, Serikali au mashirika yanayojihusisha na haki za binadamu yanasemaje kuhusu "VIFO VYA NDUGU ZETU IGUNGA"??

1. Mimi ni ndugu na mmoja wa marehemu kati ya hao waliofariki, nimeumia sana na nina mchungu sana. Ukweli unaokuja kuniuma ni pale tu ninavyofikiria jinsi gani wametutoka, na hasa vifo vya tabu walivyovipitia. Inauma sana wacha nianze na moja baada ya nyingine:-

CCM,
Najua CCM wameshinda uchaguzi na sasa wanasherehekea lakini sisi tumefiwa na ndugu zetu na wala hatujasikia tamko lolote wala pole wala hatujapewa pole na chama ambacho kimeshinda. Kuna nini? vifo hivi CCM wamevifanya kwa makusudi?

CHADEMA,
Mimi nakiheshimu sana chama hiki cha CDM kwa vile kilikuwa mstari wa mbele sana kutetea haki za wanyonge na ndiyo maana hata hawa ndugu zetu tuliwashwishi zaidi ili wajenge matumaini na Chama hiki. Imekuwaje CDM wako kimya sana na suala hili la kinyama? Nina shaka kuwa inawezekana hata CDM inatuhuma nzito katika uchaguzi huu, wanaogopa kufukua mengine yaliyolala. Kwanini wasiitishe maandamano nchi nzima? kwa hali hii tunangoja nini? tayari tumeshamwaga damu tena kinyama kabisa si mara mia tufe tunampinga rais aliyeko madarakani? CDM mkinyamaza hivyo nawaapia 2015 mtakosa watu kabisa, teteeni haki ya watu wenu wote. Na sasa naomba tamko kutoka kwenu CDM juu ya ndugu zetu waliokufa kwa suala ambalo linawahusu nyinyi zaidi.

SERIKALI,
Mbona kimya? Angekufa hivyo mtoto wako wewe JK ungependa? hata kama angekuwa kiongozi yeyote wa watoto wake au ndugu yake akafa hivyo unadhani kingetokea nini?

MASHIRIKA YA HAKI ZA BINADAMU
Mbona kimya? mbona hampigi kelele juu ya hili? Namshukru Mungu kuna mwanasheria mmoja hapa nchini amekubali kutusaidia kuongea na Ocampo aje afanye mambo yake nina imani watu wengi sana watalala ndani. Inauma sana

Tumeonewa, familia yetu imejaa machozi inauma sana.
 
Back
Top Bottom