CCM bila ufisadi inawezekana. Maneno hayo yalisemwa na Nnape akiongea na Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha St. Austine Mtwara. Aliwaeleza vijana hao kuwa historia ya chama chetu ni kuwatetea wakulima na wafanyakazi wanyonge. Sifa hiyo ya kihistoria imechafuliwa na mafisadi wachache sana.Hivyo ni jukumu letu vijana wa CCM kurudisha heshima ya chama chetu kwa kuwa kataa mafisadi ndani ya chama chetu.