CCM bado ni chama imara na chenye nguvu Tanzania: Dk BANA

Ntaramuka

Senior Member
May 2, 2008
169
27
Mhadhiri mwandamizi wa sayansi ya siasa-UDSM dk Benson Bana amesema Chama Cha Mapinduzi bado ni imara ukilinganisha na vyama vingine. Hoja yake ameijenga kwa vigezo hivi:
1. Chama kina ofisi za shina hadi taifa ambako kuna umoja wa vijana, wanawake, wazazi nk
2. Maslahi ya taifa. Katiba, sera, ilani nk ya CCM zinaeleza vizuri sana maslahi ya watanzania. Tatizo la Ccm ni kwenye utekelezaji, tatizo ambalo si la Ccm peke yake kwani ccm siyo ya malaika. Je, unadhani yuko sahihi? Kwa nini? Thibitisha
 
Gamba wa kutupa huyo kamwe hawezi kuacha kufagilia magamba. Inaelekea 2015 atawania jimbo na si ajabu kwenye ndoto zake anaweza kuukwaa uwaziri. Ukweli wa hali ilivyo nchini mwetu haujifichi kama ni mfuatiliaji wa mambo mbali mbali yanayohusu uongozi wa Taifa changa la Tanganyika naamini utanielewa namaanisha nini.

Mhadhiri mwandamizi wa sayansi ya siasa-UDSM dk Benson Bana amesema Chama Cha Mapinduzi bado ni imara ukilinganisha na vyama vingine. Hoja yake ameijenga kwa vigezo hivi:
1. Chama kina ofisi za shina hadi taifa ambako kuna umoja wa vijana, wanawake, wazazi nk
2. Maslahi ya taifa. Katiba, sera, ilani nk ya CCM zinaeleza vizuri sana maslahi ya watanzania. Tatizo la Ccm ni kwenye utekelezaji, tatizo ambalo si la Ccm peke yake kwani ccm siyo ya malaika. Je, unadhani yuko sahihi? Kwa nini? Thibitisha
 
kila mtu ana njia yake ya kuhakikisha ccm inapotea katika ramani ya siasa tz.
Dk Bana anaipaka ccm mafuta kwa mgongo wa chupa!
 
Hassy kitine ameivua ccm nguo kabisa!anasisitiza chama kimepoteza mwelekeo,kimekuwa cha mafisadi na wenye hela,dr banna amenywea,tehtehteh, Ayoub ryoba is so smart.
 
Huyu ni mtafiti wa CCM kupitia REDET, lakini kwa mwendo huu atapotosha uongozi wa CCM. Neno imara kwa lugha ya wenzetu ni "strong", sasa kama alikuwa ni mwanafuzi wangu wa PhD na yupo mbele yangu to defend his thesis kwamba 'CCM is Still Strong', ningemuuliza anithibitishie by taking into account kwamba being strong means:
-Firm;
-Impregnable;
-Potent;
-Secure;
-Immune from attack;

Baada ya kuthibitisha haya ndio ningetoa recommendation for him to be awarded a PhD based on his thesis.
 
Mhadhiri mwandamizi wa sayansi ya siasa-UDSM dk Benson Bana amesema Chama Cha Mapinduzi bado ni imara ukilinganisha na vyama vingine. Hoja yake ameijenga kwa vigezo hivi:
1. Chama kina ofisi za shina hadi taifa ambako kuna umoja wa vijana, wanawake, wazazi nk
2. Maslahi ya taifa. Katiba, sera, ilani nk ya CCM zinaeleza vizuri sana maslahi ya watanzania. Tatizo la Ccm ni kwenye utekelezaji, tatizo ambalo si la Ccm peke yake kwani ccm siyo ya malaika. Je, unadhani yuko sahihi? Kwa nini? Thibitisha

Yeah kinavyo hivyo sababu ya NGUVU lilivyo navyo wakati wa CHAMA kimoja; Kila mtu alikuwa anakatwa kiasi cha

Mshahara wake kuendeleza hayo mashina ya CCM; Na wanachi walichangia CCM kilikuwa na KILA kitu Majengo, Mahoteli

Viwanja, Majumba Sasa hivi NGUVU zote za kiusalama zinailinda CCM; kwanini kisibakie kuwa na NGUVU?

Yeah; Kilijengwa tofauti na KANU, Kenya; UNIP, Zambia;

* SASA KAMA KINA NGUVU Kwanini wasikubali
UCHAGUZI HURU? USIO NA UCHAKACHUAJI?
 
Nadhani amekiri mwenyewe kuwa kuna tatzo katika utekelezaji.hapo anamaanisha kuwa ufisadi na wizi ndio hasa vinavyoamalaki katika chama hiki na kuwa ndivyo vinavyoikwamisha ccm na huo hasa ndio udhaifu unaoiondolea ccm uwezo na uhalali wa kuendelea kutawala.ajiandae sasa kuisifia cdm.
 
Nilicheka sana alipodai kuwa kwa sasa "watanzania" wanataka vyama vya upinzani ambavyo vitatumia mikutano yake kuwahamasisha na kushirikiana na wananchi kwenye mikutano ya kusiasa kusomba mawe na kujenga mahospitali, mashule n.k. Eti kwamba uchaguzi uliisha 2010 na sasa ni siasa za ujenzi wa nchi na si mambo ya kukosoana. Na huyo ndiye mtaalamu wa sayansi ya siasa Tanzania!
 
anapigia jalamba u mkandala pale mliman ndo maana amejipofusha akili
 
imara kijijini kwao sigimbi,mwehu huyu,sie tunafikiria tunawatoaje hawa wapigaji uchaguzi ujao yeye analeta upuuzi wake,tukiwaachia waendelee kutuongoza tutatoka lini sasa,alaaaaa!!
 
haya mashina na ofisi nyingi za ccm zimebaki majengo tu,watu kwa maana ya wanachama hakuna,Kati ya kata 19 za Arusha mjini,ni kata moja tu ya sekei ofisi ya ccm inafanya kazi.Majengo hayo yamegeuzwa baa
Kwenye uchaguzi wa ndani ya ccm wa ngazi ya mashina wameshindwa kwa 45%hii ni nchi nzima
 
Kuna wakati huwa naona aibu kuwa aluminae wa UDSM kwa sababu ya pumba za dr. Bana. Nawaonea huruma wanafunzi wake wa political science. Yaelekea wasipoifagilia CCM anawakamata! Aibu!
 
Ulitegemea mtu kama huyo aseme nini? Mara nyingi huwezi kwenda hospitali kumwangalia mgonjwa mahututi na yule anayemuuguza akakwambia "hali yake ni mbaya" atasema tu "bado kidogo atapona" kumbe ndo yuko kufani!!!!!
 
Huyu ni mtafiti wa CCM kupitia REDET, lakini kwa mwendo huu atapotosha uongozi wa CCM. Neno imara kwa lugha ya wenzetu ni "strong", sasa kama alikuwa ni mwanafuzi wangu wa PhD na yupo mbele yangu to defend his thesis kwamba 'CCM is Still Strong', ningemuuliza anithibitishie by taking into account kwamba being strong means:
-Firm;
-Impregnable;
-Potent;
-Secure;
-Immune from attack;

Baada ya kuthibitisha haya ndio ningetoa recommendation for him to be awarded a PhD based on his thesis.

Well said Mkuu, msomi huyu anasumbuliwa na njaa. Kama ni kweli CCM iko "Strong" awashauri waitishe uchaguzi kaatika majimbo yaliyotangazwa kuwa wazi hadi sasa kuchakachua waone kitakachojiri. Kujipendekeza kwingine hadi kunatia kinyaa! ni huyuhuyu wa REDET inayotumiwa na CCM kuwatisha wapinzani kwa kuwatabiria CCM kushinda kama kuwaandaa kisaikolojia kwa zoezi la wizi wa kura kila wakati wa chaguzi? Binafsi simwamini hata chembe kwa sababu zifuatazo:
  • Hayo matawi ya CCM anayosema ni kama magofu yaliyohamwa lakini yanayofagiliwa na kupambwa wanapokuja viongozi, ushahidi ni pale "viongozi" wanapotaka kuongea na wanachama huhitajika nguvu za ziada za kuwalipa na kuwasafirisha wanaoitwa wanachama!
  • Zinapotokea chaguzi ndiyo kabisa hao "wanachama" wao (Wafu?) huwapigia kura wapinzani wao kiasi cha kuhitajika hila za wizi wa kura ili chama chenye mtandao hadi kwenye "mashina" kishinde, lakini mara kadhaa kimedondokea pua!
  • Chama "imara" na chenye mtandao sasa kimebanwa kiasi cha kuhitaji vyombo vya dola kukisaoidia kuendelea kuishi. Hebu tazama Mahakama, Polisi na usalama wa taifa vinavyotumika ki-jinai kukisaidia CCM kugandamiza haki za wenye mawazo tofauti na watawala wa CCM! Mifano iko wazi; hukumu za ajabu ajabu ambazo hata mwanafunzi wa darasa la saba anaweza kuhoji, kutumika nguvu iliyopindukia kuwanyamazisha wanaojaribu ku-register dukuduku zao kwa kuwapiga risasi za moto, kuwajeruhi na hata kuwaua, na kuwafanyia vitendo vya kihuni kama kuwaundia ajali, kuwatega, kuwateka nyara kuwajeruhi na pengine kuwaua kihuni wakosoaji wa serikali ya chama "imara" kunakofanywa na ki-mafia na vyombo vya usalama!
 
Na hivi karibuni ataibuka na NEW REDET baada ya kupata fungu CHOTWA toka NSSF aanze kupiga ramli.
 
Huyu Dr anatakiwa apelekwe MIREMBE haraka na familia yake hali yake inazidi kuwa mbaya kila kukicha.
 
mtumikie kafikiri upate ujira wako,ndicho anachofanya ila ni vyema akazinduka soon anaingia shimoni.
 
Back
Top Bottom