CCM Arusha waanza kuparurana kuhusu Arumeru Mashariki

Joseph Peter

Member
Oct 18, 2011
40
39
Jamani hii siasa wanayo icheza CCM ya Leo ni ya ajabu sana. Maana itakumbukwa kwenye Kikao cha kamati ya siasa ya Mkoa wa Arusha cha kujadili wagombea ubunge wa Arumeru Mashariki, wajumbe wa Kikao walimwomba RC wa Arusha awapelekee nyaraka mbalimbali kuhusu ufafanuzi wa masuala ya rushwa na uraia wa Sioi na hii ni kwa Kuwa kwa mujibu wa taratibu za ccm RC ni mjumbe wa kamati ya siasa ya Mkoa.

Lakini cha kushangaza Mara tu baada ya RC kukabidhi nyaraka hizo tukashusahudia kuvuja kwa nyaraka hizo kwa kasi ya ajabu. Tukajiuliza kulikoni mwenyekiti wa ccm Mkoa wa arusha ndugu Onesmo Nangole ang,ang,anie kuonyeshwa nyaraka hizo? Kumbe yeye na kijana wake mtumwa wa mafisadi James Millya walikuwa na Lao jambo. Walipanga kuvujisha ili ionekane Kuwa Sioi anaonewa na aweze kipata huruma ya wana Arumeru Mashariki. Huu ni upuuzi mtupu. Lazima wajue Kuwa wana Arumeru Mashariki hawadanganyiki.

Hivyo kuna tetesi Kuwa Onesmo Nangole na James Millya watahojiwa kwa kuvujisha Siri za vikao vya CCM.
 
Asante Mulongo kwa ushirikiano.
Nangole na Millya ni watumwa wa Lowassa hawawezi kumuumbua kijana wao bitoz Siyoi.
Mulongo na Chatanda walijionyesha live kutoka mwanzo kuwa hawamkubali Bitoz.
Hongera Mulongo kwa kutusaidia!
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom