CCM Arusha sasa wajisalimisha kwa Pinda...

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,173
Leo kwenye taarifa ya saa moja usiku katika Channel ten...

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Arusha ameomba Waziri Mkuu kuingilia kati sakata la Umeya wa Arusha kwa kutoa ufafanuzi kama Katibu wa Mkoa wa CCM Arusha ambaye ni mbunge wa viti maalumu wa Mkoa wa Tanga anaweza kushiriki katika kupiga kura za kumchagua Meya wa Arusha kwa vile sasa ni mkazi wa Arusha badala ya Tanga.

Kauli hii ya CCM Arusha inatofautiana na ile ya Makamba ambaye kila mara amekuwa akisisitiza Chadema waende Mahakamani kuhoji uhalali wa Chatanda kushiriki uchaguzi huo...
 
why wanachanganyikiwa ina maana waliposheherekea Meya kushinda walikuwa hawajui sheria? mbona hawakuuliza hili swali kabla ya uchaguzi wa Meya. Mbona wana proof beyond reasonable doubt kwamba ni Vilaza na wanafanya mambo kwa kuburuzwa.

Kama swali hili limeonekana muhimu kipindi hiki ni hakika ni lugha ya kisiasa ya kumtema Chitanda kwani m/kiti wa mkoa huchaguliwa na wanachama kutoka ndani ya mkoa husika. katibu wa mkoa ni mwajiriwa wa CCM na siyo mwakilishi wa wana chama katika ule mkoa. Hii imekaa vizuri kama kweli Mr. chairman anataka kwa dhati huo ufafanuzi.
 
Vile vile waandishi wa habari wametoa kauli ya kupinga kauli chafu za katibu wa CCM wa Mkoa Mary Chatanda na kuasa hatua zichukuliwe dhidi yake............................................
 
inajengwa "hoja" ili wamteme chitanda, kimsingi amekiumiza sana chama kwa kufuata ujinga wa makamba
 
CCM Wanaweweseka tu hawana pa kushika kule maaskofu huku waandishi wa habari pale wanaharakati hapa wananchi na wana CCM wenyewe( Mzee malecela, na madiwani wanaohamia CHADEMA) yaani kazi kwelikweli.
 
Leo kwenye taarifa ya saa moja usiku katika Channel ten...

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Arusha ameomba Waziri Mkuu kuingilia kati sakata la Umeya wa Arusha kwa kutoa ufafanuzi kama Katibu wa Mkoa wa CCM Arusha ambaye ni mbunge wa viti maalumu wa Mkoa wa Tanga anaweza kushiriki katika kupiga kura za kumchagua Meya wa Arusha kwa vile sasa ni mkazi wa Arusha badala ya Tanga.

Kauli hii ya CCM Arusha inatofautiana na ile ya Makamba ambaye kila mara amekuwa akisisitiza Chadema waende Mahakamani kuhoji uhalali wa Chatanda kushiriki uchaguzi huo...
Ushauri wa nini tena wakati kesho wanasherehekea ushindi wa meya wa CCM, watapatapata sana mwaka huu.
 
wacha wajichangaje kwanza mwisho wasiku watakuwa kichwa chini miguu juu,kesho jamani twende kuwasindikiza mashujaa wenzetu NMC
 
Kwani aliingia kwenye kikao cha kuchagua meya kama nani?mkazi wa arusha au mbunge wa tanga?kama ishu ni mkazi wa arusha basi wakazi wote wa Ar wangeruhusiwa kuchagua meya.naamini eneo lake la uwakilishi ni Tanga.wanauliza sasa hivi baada ya watu kufa na kuumizwa!majuha kweli kweli.nina uhakika 100% hili jimbo wameshalipoteza kwa miaka mingi ijayo.
 
Wamesha jua kosa walilo fanya sasa wanatafuta namna ya kuchomoka bila kuhojiwa............yamewafika na watakataliwa kila kona ya nchi hii
 
Tatizo la huyu mkwere hafikirii mbali yeye anaangalia dini kwanza, Kilichomfanya amteuwe Makaamba si ujuzi bali yaweza kuwa ni dini yake:smile-big:
 
Things fall apart, center can no longer hold

"'When did you become a shivering old woman,' Okonkwo asked himself, 'you, who are known in all the nine villages for your valor in war? How can a man who has killed five men in battle fall to pieces because he has added a boy to their number? Okonkwo, you have become a woman indeed.'"
- Chinua Achebe, Things Fall Apart
 
Mpaka sasa kambi ya Mary Chatanda imebakiwa na ktb mkuu, mkuu wa propaganda na yeye mwenyewe tu! Mkuu wa propaganda anaweza kula kona muda wowote na ktb mkuu ataachia ngazi kwa kustaafu siasa.
 
Kuna kila sababu ya kuwapima hawa jamaa akili! Kwa kuanzia na yule anaye nukuu vifungu vya Biblia pasipo pake na kumdhihaki mola!
 
Back
Top Bottom