CCM Arumeru- Siyoi hakuwa chaguo letu, sasa alikuwa chaguo la nani?

dosama

JF-Expert Member
Dec 25, 2010
912
957
Ccm Arumeru wameamua kujivua gamba na kusema siyoi hakuwa chaguo lao.

Mi najiuliza lilikuwa la nani? Jk, EL,Deadstone, chimpanzee........ Au
Source Mwananchi

Wakati hayo yakijiri gazeti la uhuru kinadai wananchi wamechagua upinzani kwa kufata mkumbo wa mabadiliko.

Sasa kama Wanaarumeru wa ccm walidai si chaguo lao, mara si raia wa tz, hakujui kwao, kurithishana madaraka, nk hawakuviona leo ccm inawakejeli wana Arumeru wanafata mkumbo kweli?
 
Ccm acheni unafiki, mtawadanganya Watanzania mpaka lini? Nape alishasema mmeshindwa kihalali na kuwapongeza watu wa Peoples power, hayo mengine yatoka wapi tena? Kifo cha nyani miti yote.......!
 
Kwanini viongozi wengi walienda Arumeru kama sio kumpa Support Sioi?Kwa vile ameshindwa sasa wanamruka?
Hawa ni wanafiki kabisa!!Sioi angeshinda wangesema hakuwa chaguo lao??
 
Hizo ni hila za kwapa kunuka bila donda, hakuwa chaguo lenu kwanini mkamnadi kwa gharama zote zile? mliamua kuwa komedian? Yawapasa kukubali matokeo pasi na visingizio.
 
mbaazi akikosa maua husingizia jua,mtaji wao umedoda kipindi hiki,wategemee makubw zaidi
 
Waache unAFIKI wa kijinga na kishetani kiasi hicho, hawana hata haya, nilisika huo ***** kwene Uhuru
 
Haaaaa,hawa watu wa ajabu kabisa.Wao wenyewe wamepigia kura nyingi mara ya kwanza.Mara ya pili wakamchagua kwa kishindo.Sasa chaguo lao lingepatikanaje kama sio kwa njia ya kura.Au wanataka kutuambia walipenda sana pesa muda ule wanapiga kura wakasahau kuchagua mbunge wanamtaka.
 
Inashangaza na kusikitisha jamani,.hawa hawa magamba walimpa support sana mgombea wao sioi mpaka na matusi yakatawala katika kuwashinikiza wana arumeru wamchague sioi na kumponda sana our lovely mbunge J. Nassari, leo hii wanageuka na kusema halikua chaguo lao, inamaana lilikua chaguo la nani?
 
Hili nalo neno
 
Whait hea kawamaliza!
Na walivyo maju.ha hawatachukua hatua yeyote, hadi awamalize na 2015.
 
Kifo hakikosi sababu...
utasikia siku ya mazishi kila mmoja akisema lake wakati wote wakijua kuwa amekufa kwa 'kaugonjwa fulani'. Vivyo hivyo hakuna mtu mwenye ujasiri wa kusimama ndani ya ccm na kukiri kuwa harakati za uraisi wa jk (back in 90s to-date) zimekiua chama.

Dr. Lwaitama aliposema kuwa ni 'mwana-ccm mfu' wakamcheka badala ya kujirekebisha sasa acha wafe wao

Wana ccm, meru mliipenda sana! lakini wana meru wameipenda zaidi.wameru walitoa,wameru wametwaa maamuzi yao yaeshimiwe.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom