CCK imepata usajili, tuwape hongera!

Huu utitiri wa vyama unasaidiaje kuondoa umasikini wa watanzania, wachumia tumbo tu hao hawana jipya.

Ukikosa kutambuliwa ndani ya CDM kwa vile si mwana ukanda husika, unalala mbele vyama vingine. Hiyo ni demokrasia!! Usiogope kwa vile unajua CDM itapoteza kura na baadhi ya wananchama
 
Mbona sisi kwetu asmara Hakuna chama cha siasa lakini Hakuna migomo wala matatizo ya Umeme ,,,,,;,,,,
Asmara Eritrea? Unadhani tumesahau juzi hapa wachezaji wa timu ya soka ya Eritrea walivyotolewa kwenye mashindano wakagoma kurudi kwao, wakazamia Tz?
 
Hebu nifafanulie hapa...Hao CDM si ndio walienda kunywa juisy Ikulu?( na wana mpango wa kurudi tena baada ya kunogewa)
Hao CDM si ndio wana viongozi wasio na msimamo? Leo wanapinga, kesho wanakubali!!

Embu funguka zaidi apo ni lipi na lipi walikataa na kukubali
 
kirefu cha cck ni nini? majina ya mwenyekiti na katibu ni nani? ofisi zao ziko wapi?
 
Nawapa hongera za dhati kabisa kwa kufanikisha kile ambacho kilishindikana - kwa hujuma za hali ya juu - kufanyika kabla ya uchaguzi mkuu. Hawa vijana wameonesha uwezo wa kubadili mbinu na mipango hadi kuweza kufikia usajili wa kudumu. Kwa ufupi bila ya shaka ni ujumbe tu kwa vyama vingine vya kisiasa nchini kuwa viendelee kuonekana vinaongoza mabadiliko kwani hawana haki miliki ya fikra za Watanzania. Michael Satta yule wa Zambia alifika mahali na yeye akaona well ngoja "nianze tofauti".

Swali kubwa ni kuuliza hawa wanasimamia nini na wanawawakilisha kina nani na kwanini?

Kusema tu kuwa "utiriri wa vyama" peke yake haitoshi kuondoa ulazima wa chama kingine kuwepo. Hata kama watu hawapendi au hawafurahii kuanzishwa kwa chama kingine haki ya kufanya hivyo haihodhiwi na wachache. Watanzania hawa wametumia haki yao kama wananchi na ni haki ambayo inastahili kulindwa.
 
Naam ni ushindi mkubwa kwa sisi tunaoamini katika kushamiri kwa demokrasia hapa nchini.....
 
Nani Mwenyekiti wa chama na Katibu Mkuu wa chama?
Ni mapema mno unaweza kuwa wewe au mimi au mwingine baada ya kuzisoma sera zao pengine tukavutiwa,hivi vyama tuliko ni kama makoti tu tukiona yanatubana bana bana ruksa kuyavua,tufikie hapo watz,vyama si baba wala mama zetu,tulikutana navyo barabarani tu!
 
Nilitaka kushangaa MMKJJ asionekane hapa.

Well, watu wameuliza sana "CCJ iko wapi" n.k na wengine kuhoji sana MM na CCJ wakiamini kuwa basi kila kitu kimeshindikana. Japo sasa hivi sijihusishi na CCK lakini ninaona furaha kuwa ushauri wa kwenda nje ya media na bila mbwembwe umefanikisha wao kupata usajili wa kudumu maana hakuna chama kilichohofiwa kabla ya uchaguzi mkuu wa 2010 na sasa hivi chaweza kuhofiwa sana kama CCK..

Binafsi naamini ni nzuri kwa upinzani nchini kwa sababu watu wengi zaidi wanaonekana kutokubaliana na CCM na hawa wameamua kufanya hivyo; sitashangaa nikisikia kina Hamad nao wameunda chama chao; Tanzania bado ina watu wengi sana wasio katika chama chochote.
 
Tatizo waumini wa siasa za vyama mnajipenda kupita kiasi,huwa mnasahau na sisi tupo..na ndio huwa tuna determine nani awe rais au mbunge,nyie mko wachache sana sema mna makelele mengi tu,sisi huwa tunawatizama tu.
 
Back
Top Bottom