Mwanafalsafa.... CCM wamekuwa wakiwashinda wapinzani kwa mkakati tu hakuna wizi wala nini; safari hii na sisi tutawafunga kwa mkakati hivi hivi... goli ambalo tutawafunga litakuwa ni goli la kihistoria....
I wish Mzee MM statements kama hizi zingekuwa classified kwa sasa, Unakumbuka CUF walipokuwa wanatishia jino kwa jino, hapakaliki, damu itamwagika, statement kama zile ziliwafanya waoga wa CCM kuandaa vita na raia wake na wakati wa uchaguzi mwaka 2000, waliweka ulinzi wa kufa mtu, CUF hawakufanya vurugu japo walinyang'anywa ushindi wakaja fanya january 26 na 27 2001 na kusababisha maafa ambayo impact yake kwenye uchaguzi ilikuwa ndogo. Kama mambo yale yangefanyika kwenye uchaguzi yangevutia hisia za kimataifa na pengine leo hii tungekuwa na serikali ya mseto zanzibar kama Kenya.
Mtazamo ni kuwashitukiza: Yaani washitukie kitu kimejaa wakati wanatafuta mbinu za kukitoa kinazidi kujaa mpaka wanakubali yaishe.