CCJ kuomba usajili wa kudumu leo; yakusanya wanachama 20,000!!

Sasa hapa ndio mizengwe mbele kwa mbele.. kuna agizo limetolewa wazi kuwa CCJ no usajili.. naambiwa ni kutoka kwa wenye kutoa maagizo hayo na kama watapewa basi ucheleweshwe ili wasiweze kushiriki uchaguzi. Lengo ati ni kutotaka kuua upinzani uliopo sasa kwani itakuwaje chama kije juzi juzi tu na kuweza kuchukua nafasi ya vyama vikongwe vya upinzani.. well.. kila kitu kina gharama..
 
Vyama vya upinzani vimetoa kauli gani kuhusu Wafanyakazi kutukanwa na rais wa Jamuhuri?

watu wengine wachokozi bwana, teh teh teh
Kwa hiyo unataka kusema vyama vya upinzani ni vipandikizi vya JK, ndiyo maana vinaelekea kugwaya kutia mgombea wa Urais.?
 
Ni kweli mkuu, kama mnataka kujenga nyumba moja kwa nini mpiganie fito? Je CCJ inakuja na lipi jipya ambalo CHADEMA, NCCR Mageuzi, CUF, TLP na vinginevyo halimo kwenye nia au dhamira ya kumkomboa mtanzania? Kadri vyama vinavyozidi kuongezeka ndiyo CCM inavyozidi kufurahi kwani bila kufikiria kuunganisha nguvu itakuwa ndoto kukiangusha Chama kongwe kama CCM.

YES, kama nikipata key issues ambazo CCJ inakuja ku-address kwetu ambazo CHADEMA na vingine vyote vimeshindwa ningefurahi zaidi, otherwise i'm not interested na hata taifa halifaidiki sana na ujio wa chama hiki, kusajiri vyama utitiri ni kuwachanganya watanzania.

Matokeo yake watanzania wanasema bora tuchague CCM zimwi likujualo.., na pia wahenga wanasema mkataa wengi ni mchawi - CCJ imewakataa wote hivyo lazima tuwe na wasiwasi nacho.

Wenda ni kwa sababu
Vyama vilivyopo ni vya kikampuni zaidi, na CCJ ni chama cha siasa. teh teh teh, subiri uone wanatenda nini ndo uhoji kwanini wanatenda vile na si hivi, sasa ninyi mnaanza kuhoji watatenda nini kama vile tayari hakuna cha kutenda na mambo yapo mstari.
 
Kama fisi kashindwa kula mfupa ina maana mbwa asijaribu; well.. yawezekana ni kweli ni mfupa ule ule lakini kila mmoja na mbinu zake!
 
kila la heri wanasiasa ila msije mkatuletea kauli za kutudhalilisha na kututukana
mkiwa marais kwani tukiwapa kura baadae mnasema hata tusipowachagua mtakuwa
viongozi sijui wanasiasa wa bongo mmelogwa au nimalimbukeni
 
Hawa huoni hata John Tendwa anawapiga chenga watakuwa wanaishia tu masijala pale, wakisogea sana ni kwa katibu muhtasi wa Tendwa na si zaidi. CCJ usajili 2011. Poleni.
 
[QUOTE=
Shalom dear, bila shaka umezaliwa juzi tu na hujui vyema historia na yale ambayo Mwalimu Nyerere alifanya kwa Taifa letu. Naomba nikumegee kiduchu. Pengine nifanye hivyo kwa kutoa mfano mmoja tu kuelezea sifa alizowahi kupewa Mwalimu kwa kufanya mambo muhimu kwa manufaa ya wananchi wa taifa alilokuwa akiliongoza.

Rais wa Benki ya Dunia alikuwa mmoja wa viongozi wa Kimataifa waliokuja kwenye mazishi ya Mwalimu Oktoba mwaka 1999. Huyu bwana katika salam zake za rambirambi alizozitoa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam alisema hivi:

"Wakati wachumi wa dunia walipobishana juu ya umuhimu wa kupima ufanisi wa mitaji, Mwalimu Nyerere alisema kilicho muhimu zaidi ni watu kuweza kusoma na kuandika, kupata maji safi na huduma bora za afya…." (Tafsiri hii ya maneno ya Rais wa Benk ya Dunia ilitolewa kwenye magazeti wakati ule wa msiba wa Mwalimu).

Si huyo tu, viongozi wote wa kimataifa, wa nchi za Afrika na nchi jirani waliopata fursa ya kutoa salam zao za rambiramba walisema maneno yaliyodhihirisha jitihada na kazi kubwa aliyoifanya Mwalimu kwa maendeleo ya watu wa taifa lake, kusaidia na kuharakisha ukombozi wa bara la Afrika na kutafuta haki na fursa sawa miongoni mwa mataifa yanayoendelea duniani. Hayo yaliyosemwa hayakuwa katika makaratasi bali katika vitendo vya Mwalimu.

Tukichukulia mfano wa maneno aliyoyasema Rais wa Benki ya Dunia juu ya yale ambayo Mwalimu aliyaona ndiyo ya muhimu zaidi kwa wananchi; tukianza na elimu: Wakoloni (Wajerumani na Waingereza) walitutawala kwa takriban miaka sabini. Hawakujali kabisa juu ya elimu ya wananchi waliokuwa wakiwatawala. Matokeo yake mwaka 1961 wakati nchi inapata uhuru na Mwalimu anashika uongozi kulikuwa na Madaktari 12 tu Waafrika nchini, Engineers wawili, kulikuwa hakuna chuo kikuu hata kimoja nchini. Waingereza walipotakiwa kusema watajenga lini Chuo Kikuu nchini walisema labda 1967 wakitoa visingizio kwamba ilikuwa ghali mno kujenga chuo, kusomesha wanafunzi na kwamba kulikuwa hakuna idadi ya wanafunzi wa kutosha kulazimu kuwepo kwa Chuo Kikuu .

1961 Mwalimu alianzisha Chuo Kikuu nchini kikianza na wanafunzi 17, wakati anaondoka madarakani kulikuwa na idadi ya wanafunzi 3,400 katika vyuo vikuu viwili – UDSM na Chuo Kikuu cha madaktari Muhimbili. Wakati huo huo akiongozwa na dira ya Siasa zake za Ujamaa na Kujitegemea, Mwalimu alijenga vyuo vingine – Chuo cha Ualimu Chang'ombe, Chuo cha madaktari Muhimbili, Chuo cha Ufundi (DIT) na vingine mikoani. Kwenye shule za Sekondari wanafunzi Waafrika walikuwa wachache mno kwa sababu ya kubaguliwa; kulikuwa na shule za Wahindi, Wazungu na za Waafrika. Utaratibu huo wa kuwepo shule kwa misingi ya rangi ya mtu ukafutwa mara moja ili idadi ya Waafrika kwenye shule za Sekondari iongezeke. Zilikuwepo pia shule za kidini hasa za kikristo ambazo zilikuwa zikisomesha wakristo peke yao. Mwalimu akafuta mpango huo nao na shule zote zikawa zinachukua wanafunzi wa dini zote.

1961 wanafunzi wa shule za msingi walikuwa 480,000. 1985 wakati Mwalimu anaachia uongozi kulikuwa na wanafunzi 3,660,000 kwenye shule za msingi nchini wakisomeshwa bure bila kulipa hata senti tano. Shule za Sekondari za Serikali 1961 zilikuwa na wanafunzi 11,832 (wazungu, wahindi na Waafrika) ambao walikuwa wakilipa ada kwa maana hiyo walikuwa ni watoto wa watu wenye uwezo kifedha – waajiriwa Serikalini na kwenye sekta binafsi na wafanyabiashara. Mwaka 1985 kulikuwa na wanafunzi 40,617waliokuwa wakisomeshwa na Serikali. High School – form V & VI 1961 kulikuwepo wanafunzi 236 mwaka 1985 walifikia 2,125.

Mbali ya hatua za makusudi kuchukuliwa kujenga vyuo na shule za Sekondari ili kuwapa fursa wananchi wengi kupata elimu kulikuwa na training institutions za kila aina chini ya Wizara ya Elimu ilikuwa na zake na wizara zingine nazo zilianzisha kulingana na mahitaji ya Wizara husika kwa mfano kwenye Wizara ya Kilimo kulikuwa na vyuo vya kilimo ili kusaidia kukuza kilimo bora nchini; na kadhalika. Mashirika la Umma nayo halikadhalika yalikuwa na vitengo vyao vya mafunzo mbalimbali kwa wafanyakazi. Majeshi nayo yalianzisha Shule za Sekondari ili kutoa fursa kwa askari kujiendeleza kielimu – kwa gharama za Serikali; ilianzishwa Institute of Finance Management (IFM), Police Colleges, Elimu ya Watu Wazima; you just name them .... Nchi nzima ilikuwa inanuka elimu kwa wote!

Kwa taarifa yako Shalom na wengine wasiojua mambo aliyofanya Mwalimu, elimu ilikuwa ni bure kwa kila mtu na hayo yote yalifanywa na Serikali kupitia mipango ya makusudi ya Maendeleo kwa ajili ya wananchi wote. Serikali ilikuwa na "Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano' na kila baada ya miaka hiyo tathmini ilikuwa ikifanywa kuangalia mafanikio na mapungufu.

Si elimu tu hata upande wa Afya Serikali iliyokuwa ikifuata itikadi ya Ujamaa na Kujitegemea ilifanya makubwa katika kukuza na kuwapatia wananchi huduma za jamii bure bila malipo yoyote. 1961 kulikuwa na jumla ya hospitali za mikoa na wilaya 98 nchi nzima 1985 zikawa 149, vituo vya afya 22 – mwaka 1985, 239. Zahanati 975 mwaka 1961 – 1985 zilikuwa 2,644. 1961 asilimia 11 ya idadi ya wananchi milioni 10 wakati huo walikuwa wanapata maji safi. 1985 asilimia 50 waliweza kupata maji safi majumbani mwao ama umbali wa meta 400 kutoka majumbani kwao. Wafanyakazi wa sekta ya Afya waliongezeka kutoka madaktari 12 wakati tunapata Uhuru – daktari mmoja kwa watu 830,000. 1985 walikuwepo madaktari 782 waliofuzu kiwango cha kimataifa. 1985 AMOs walifikia 436 ukilinganisha na 32 waliokuwepo mwaka 1961. Mbali ya hao walikuwepo jumla ya Medical Assistants na Rural Medical Aids 6,328 mwaka 1985. Infant mortality rate wakati tunapata Uhuru ilikuwa ni watoto 225 wanaokufa kwa kila 1,000 wanaozaliwa hai 1985 ilikuwa ni watoto 137. Life expetancy ilikuwa miaka 35 wakati wa kupata Uhuru, ikafikia miaka 51 mwaka 1985. Leo bila shaka imeshuka kutokana na Sera za kibebari tulizozikumbatia!

Haya niliyoyaorodhesha hapa si mambo ya kwenye makaratasi bali ni vitu real vilivyotokea na kutendwa na Mwalimu kama kiongozi wa nchi kwa manufaa ya Taifa. Maamuzi ya makusudi yalichukuliwa ili ‘keki' ya taifa igawanywe vizuri, wananchi wafaidi matunda ya Uhuru na kuwepo uwiano wa mapato kati ya viongozi na wananchi.

Wapo watu humu ukianza kusifu juhudi za Mwalimu wanakuja na hadithi za kupanga foleni ya sukari, sabuni, colgate etc etc. Vitu ambavyo hata leo hii kwa mwananchi maskini ni luxury kwao ambayo hawaipati na hata kama bidhaa hizo zipo bwelele madukani mwananchi hana uwezo kifedha wa kuzinunua tofauti na wakati wa Mwalimu ambapo wananchi walikuwa na fedha mifukoni mwao wakihaha kuzitafuta bidhaa hizo.

Wengine wanadai Mwalimu aliifilisi nchi kwa siasa zake za Ujamaa zilizopelekea atumie fedha nyingi kuwapa wananchi huduma za bure. Kama nchi ilifilisika kwa ajili hiyo basi ilifilisika kwa nia njema na kwa manufaa ya wengi na si kama ilivyo sasa ambapo nchi inafilisika kutokana na ufisadi na ulafi wa viongozi wachache na wananchi wasio waadilifu. Hakuna kiongozi ama mtu yeyote wa ndani ama nje ya nchi anayeweza kudai kwamba Mwalimu alitumia madaraka yake kwa manufaa yake ama ya familia yake na rafiki zake. Ndio maana hata alipofariki wananchi walimlilia sana, viongozi wa Afrika na Dunia wakiwemo viongozi wa Marekani (Reagan akiwemo) walisifu uongozi wake uliokuwa unajali sana watu aliokuwa akiwaongoza kuliko kitu kingine chochote.

Itoshe kusema Mwalimu alijali Maendeleo yanayolenga Watu. Tujiulize, je viongozi wetu wa jana, leo na kesho wanajali maendeleo yanayolenga watu (wananchi waliowapa dhamana ya kuwaongoza) ama wanajijali zaidi wao, familia zao na marafiki zao?

Hivi kiongozi akishahakikisha anawapa wananchi wake elimu (bure), tiba (bure) na pembejeo (bure) kwa wakulima, ili wavitumie kujikwamua katika umaskini, kipi kingine cha muhimu zaidi anachohitaji binadamu?

Shalom, hapo sijaweka idadi ya viwanda vilivyojengwa enzi za utawala wa Mwalimu vilivyokidhi kila hitaji na baadaye vikabinafsishwa na hatimaye kufa badala ya Serikali kuamua kuchukua hatua za makusudi za kuvifufua kwa manufaa ya Taifa. Kama Mwalimu aliweza kuvijenga kwa nini wao washindwe kuvifufua? Ukitaka nikuorodheshee mema ya Mwalimu tutakesha mtandaoni! Nimalizie kwa kusema kwamba Mwalimu kama binadamu naye alifanya makosa ya hapa na pale katika uongozi wake lakini si kweli kwamba "outputs' zilikuwa haba kama ulivyodai.

[/QUOTE]


Mkuu Mimi nakupongeza tatizo watanzania wachache wanaotumia muda wao kuweza kujua historia ya nchi yetu. Haya maneno yako ni maneno ya ukweli na siyo porojo. ubarikiwe kwa kutukumbusha
 
Mwenyekiti wa CCJ Mh. Richard Kiyabo akionesha risiti ya stakabadhi ya malipo ya kuwakilisha majina ya wanachama leo ofisi ya Msajili wa Vyama vya siasa jijini Dar


Viongozi wa Chama Cha Jamii (CCJ) wakimkabidhi majina ya wanachama wa bara na visiwani Mkuu wa Masijala katika ofisi ya msajili wa vyama vya siasa, Bi. Mwajuma Amir. Kutoka kulia ni Naibu Katibu wa chama hicho kwa upande wa Zanzibar, Mh. Ali Hatibu Ali, Katibu Mkuu wa Chama hicho, Mh. Renatus Muabhi, Mwenyekiti wa Chama hicho, Mh. Richard Kiyabo na Katibu Mwenezi Taifa, MNh. Costantine Akitanda. Makabidhiano hayo yamefanyika leo katika ofisi za msajili wa vyama vya siasaMtaa wa Shaaban Robert jijini Dar.
Viongozi wa kitaifa wa CCJ wakiondoka ofisi za Msajili wa Vyama baada ya kukabidhi majina ya wanachama wao wa bara na visiwani

Sidhani kwamba kuna ulazima wa kuitana Mheshimiwa. Naamini wana CCJ ni "Ndugu" zaidi ya Mheshimiwa!
 
Back
Top Bottom