CCJ Kulikoni!?

Ukisoma between the lines, inaelekea CCJ ilikuwa inawatisha sana CHADEMA. Naona CHADEMA wanapumua kwa nguvu zote baada ya kuona CCJ wamefulia.

Mimi nilijua toka mwanzoni kwamba hao CCJ ni hoax tu toka mwenyekiti wao aliposemwa amekabwa Kariakoo. Mara ya pili walisema watawatambulisha vigogo, lakini hakutokea mtu badala yake hata viongozi wakachelewa kwenye mkutano.

Hiki ndio chama mnafikiri mtu makini kama Dr. Salim anaweza eti kukimbilia?

Naona Mpendazoe na mzee Mwanakijiji wamefulia big time.
 
CCM wameianzisha makusudi kuwatega wanasiasa wao watakaojiondoa kabla ya uchaguzi.....na wao (Sitta,Mwakyembe & Co) walistuka ndo maana wakamtanguliza Mpendazoe.....
 
CCJ mambo magumu

Imeandikwa na Wakuru Kuliga, Kibaha; Tarehe: 4th June 2010 @ 23:59 Imesomwa na watu: 278;

SIKU moja baada ya kuambulia wanachama 13 Dar es Salaam, Chama cha Jamii (CCJ) kimeshindwa kuwasilisha wanachama wake wa mkoa wa Pwani kwa ajili ya uhakiki.

Hali hiyo ilitokea jana katika vijii vya Picha ya Ndege na Kwa Mathias, Kibaha, ambako ndiko uhakiki ulikopangwa kufanyika kwa ajili ya kutambua wanachama wa mkoa huo.

Hatua hiyo pengine inatokana na kauli ya Mwenyekiti wa CCJ, Richard Kiyabo aliyoitoa juzi katika uhakiki wa wanachama wake wa mkoa wa Dar es Salaam uliofanyika katika viwanja vya Mwembe Yanga, Temeke, Dar es Salaam.

Katika kauli hiyo, Kiyabo alisema chama chake hakina imani na Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, John Tendwa, na hivyo kuhitaji vyama vya hiyari na waangalizi wa kimataifa kushuhudia uhakiki ili kujenga heshima kwa nchi na chama hicho.

Wachunguzi wa masuala ya siasa wanasema hatua ya CCJ kumkataa Tendwa, inaweza ikawa inaipotezea muda, kwani haitakuwa rahisi kwa ofisi nyingine kuendesha uhakiki huo kwa kuwa kisheria ofisi ya Tendwa ndiyo inahusika.

Kwa hali ya kawaida isingekuwa rahisi pia kwa chama kama hiki kilichoibuka kwa kishindo kukosa mwanachama hata mmoja mkoani Pwani, wakati kikijua kwamba uhakiki utafanyika katika mkoa huo ambao ni jirani na Dar es Salaam, yaliko makao makuu yake.

Hiyo inathibitisha kauli ya Kiyabo ya kususia uhakiki na hivyo inawezekana wanachama wakawa wamekatazwa kujitokeza kuhakikiwa, hali ambayo hata hivyo inakiweka katika hali mbaya ya kukosa usajili wa kudumu.

Timu ya uhakiki huo ikiongozwa na Tendwa, ilipowasili jana katika vijiji hivyo, haikukuta mwanachama, kiongozi wala kuona ofisi ya CCJ, mazingira yanayohatarisha usajili wa kudumu wa cghama hicho kilichopania kushiriki uchaguzi mkuu Oktoba mwaka huu.

"CCJ wamekuwa wakipiga kelele kwamba ofisi yangu inawahujumu, haitaki kuwahakiki, wanataka kuwahi uchaguzi, sisi tumejitolea kuwahakiki ili wafanye uchaguzi, lakini ninyi ni mashahidi hali halisi ya uhakiki ndiyo hii," alisema Tendwa.

Alisema pamoja na nia njema ya ofisi yake kufanya uhakiki wa wanachama wa CCJ ili kama hesabu yao itatosha waweze kukipa usajili wa kudumu, chama hicho kimerudi nyuma na kushindwa kutoa ushirikiano kwa ofisi yake na kukosa wanachama katika mikoa kama yalivyokuwa makusudio yao.

"Sisi tumejitolea tuwahakiki wafanye uchaguzi, kama wao wanarudi nyuma tena, hiyo ni bahati mbaya kwao, nia yetu ni nzuri, tungekuwa na ushirikiano mzuri na wao tungemaliza hii vizuri, kama kungekuwa na mkwamo wowote tungeshirikiana kutatua matatizo hayo," alisema Tendwa.

Msajili alisema CCJ katika uhakiki wa Dar es Salaam juzi hawakufanikiwa, Pwani kwa Mathias na Picha ya Ndege hawapo kabisa, hakuna mtu yeyote anayewajua, hawana viongozi wala ofisi.

Alipoulizwa kuna haja gani kuendelea na uhakiki katika mikoa mingine wakati hali imeonesha kuwa mbaya, Tendwa alisema tayari walishapanga, baada ya CCJ kuleta barua iliyopanga maeneo ya kufanyiwa uhakiki waliyodai wanayamudu na kusisitiza kuwa lazima yote yahakikiwe.

Alisema leo watakuwa Ifakara mkoani Morogoro kuendelea na uhakiki na baada ya hapo, watakwenda Unguja na hatimaye watatoa taarifa ya uhakiki wao.

"Nimechukua jukumu hili mimi mwenyewe, nitatenda haki na kutimiza wajibu wangu, kama watashindwa kujitokeza na mikoa mingine, CCJ watakuwa wameshindwa kutekeleza wajibu wao kama chama cha siasa," alisema Tendwa.

Juhudi za kumpata Kiyabo azungumzie mazingira ya wanachama wake kutojitokeza Kibaha jana kuhakikiwa, hazikuzaa matunda kutokana na simu yake kuita bila kupokewa.

ccjusajili.jpg

Mwenyekiti wa Chama Cha Jamii (CCJ) Richard Kiyabo, akizuiwa na mlinzi wake wakati akielekea kwenye meza ya msajili wa vyama, John Tendwa kumlalamikia kuhusu zoezi la kuhakiki wanachama wa chama hicho viwanja vya Temeke Mwembeyanga jijini Dar es Salaam jana. Picha na Silvan Kiwale

Hivi kweli CCJ ina Wanachama halali 13 tu Dar nzima? Kaaz kwer kwer!
 
mimi nilikuwa nawaambia wenzangu hata ndani ya ccm kuwa CCJ is nothing!!!....

ukweli ni kuwa CCJ[SEMA, SISI JE? chama chaa mafisadi waliokosa fursa ya kufisadi ...wakabaki wanasema ....sisi je].....kiliitisha system kwa kuwa walifanya timing kilizinduliwa wakati ccm mgogoro unafukuta......operators wa usalama na chama walikuwa hawakijui kwa undani.....lakini sasa ccj sio ajenda tena....sana sana ...kimepunguza makali ya CUF na CHADEMA maana nao walikuwa wamebaki na butwaa..kumbe hollla!!

Jiulizeni kwa nini mpendazoe hadi leo mchahara wa bunge anapata na kiti chake kipo????....kabla ya mpendazoe kwenda SISI JE? ...CCM walikuwa hawakijui kwa undani.....ni baada ya mpendazoe kuingia pale ndio ccm wakapata kibri mbele ya ccj.....safari yetu kwa demokrasia ndefu........sana!!!

tuwaunge mkono CUF na CHADEMA ......KULIKO kuanza kujenga utitiri wa vyama sasa........hata CCM they need strong united opposition...na mwakani tutaona mengi kwani CUF wanaenda kushinda upande wa zanzibar...na chadema watapata viti vingi upande wa bara.....na ni wazi Kikwete atachinda tena....

ni dhahiri kushindwa kwa wabunge wengi wa ccm kunachangiwa na tabia ya kikwete ya kupenda kuwasulubisha mbele ya wananchi......hali ambayo imejenga hisia kuwa rais anafanya kazi kuliko wabunge na watendaji.....kwenye mikutano yeye huona raha kuwatoa sadaka wajibu maswali yanayoelekezwa kwake hali hawajajiandaa na hawana suluhisho....wanabaki kuzomewa..and thats spear the president....watu wa kawaida hubaki wanasema ...hawa wanamuangusha ...hawajui serikali ni the whole system!!!!
 
Nadhani CCJ hakuna kitu, upinzani utabaki kwa Chadema na CUF tu. mpendazoe ni bora uchague chama kingine kwani ni ndoto kwa CCJ kupata usajili wa kudumu mwaka huu.
 
Ukweli hawa jamaa hawapo serious na siasa, kama kweli wanataka kushiriki uchaguzi wangekuwa wamejipanga mapema kuepuka dosari.

Wanataka kutumia ajenda ya kuhujumiwa kujipatia umaarufu wasiostahili, wamemlaumu msajili kuwa anatumiwa kuwahujumu kwa kukataa kuwasajili, msajili amekubali kwa fedha hatujuwi zimetolewa wapi, wao wanaleta utani utani tu kwenye makweli, kama hawapo tayari kufanya siasa ni bora wakae pembeni wasituchafulie hali ya hewa ambayo tokea hapo si nzuri.
 
Nafahamu kuwa mmesusia zoezi,nachotaka kufahamu baada ya kususa what next,mnatoa tena tamko kali kama amabvyo huwa mnadai!au mnafanyaje siku ndio zasonga hivyo.
Hee hee heee! Mimi sipo huko, nilikuwa natania tu (kama muungwana alivyokuwa anatania kuhusu kitochi) !
 
Binafsi nilipouangalia ule mchezo wa juzi wakati wa kuhakiki niligundua kuwa msajili wa vyama ni PANDIKIZI tu la ccm katika kuvuruga demokrasia nchini. si rafiki kabisa na vyama vingine. Pia nimegundua kuwa CCJ ni chama tishio ndio maana kinapata shuruba hivi. Wadau msidhani kuwa hiki chama ni feki tu kwani ufeki wake unajenwa na haya mabavu yanayotumika hivi sasa, kisha mwisho wa siku kama mtu haukuwa mfuatiliaji mzuri utaamini kuwa CCJ walikuwa ni wababaishaji.

Hapa kuna jambo moja linatakiwa kufanyika. Ni kwa viongozi wake wale walio mafichoni kujiweka hadharani ili waokoe jahazi. Kitu kingine nilichoona ni kuwa wanachama wake wengi ni wale wenzangu na mie hapa pangu pakavu. Sijaona watu wa daraja la kati wala la juu katika mchakato mzima wa uhakiki. Mara nyingi hili daraja la chini ndio wahanga wakuu wa mambo mengi. Ni makafara kwani hata CCJ ikafanikiwa kupata usajili wa kudumu kwa kipindi hiki, watakaofaidi kwa uzuri ni wale wa kati na wa juu. CCJ itujibu katika hili. Mbona wanachama wa awali wengi wao ni wale wa chini kabisa?
 
CCJ mambo magumu

Imeandikwa na Wakuru Kuliga, Kibaha; Tarehe: 4th June 2010 @ 23:59 Imesomwa na watu: 278;

SIKU moja baada ya kuambulia wanachama 13 Dar es Salaam, Chama cha Jamii (CCJ) kimeshindwa kuwasilisha wanachama wake wa mkoa wa Pwani kwa ajili ya uhakiki.

Hali hiyo ilitokea jana katika vijii vya Picha ya Ndege na Kwa Mathias, Kibaha, ambako ndiko uhakiki ulikopangwa kufanyika kwa ajili ya kutambua wanachama wa mkoa huo.

Hatua hiyo pengine inatokana na kauli ya Mwenyekiti wa CCJ, Richard Kiyabo aliyoitoa juzi katika uhakiki wa wanachama wake wa mkoa wa Dar es Salaam uliofanyika katika viwanja vya Mwembe Yanga, Temeke, Dar es Salaam.

Katika kauli hiyo, Kiyabo alisema chama chake hakina imani na Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, John Tendwa, na hivyo kuhitaji vyama vya hiyari na waangalizi wa kimataifa kushuhudia uhakiki ili kujenga heshima kwa nchi na chama hicho.

Wachunguzi wa masuala ya siasa wanasema hatua ya CCJ kumkataa Tendwa, inaweza ikawa inaipotezea muda, kwani haitakuwa rahisi kwa ofisi nyingine kuendesha uhakiki huo kwa kuwa kisheria ofisi ya Tendwa ndiyo inahusika.

Kwa hali ya kawaida isingekuwa rahisi pia kwa chama kama hiki kilichoibuka kwa kishindo kukosa mwanachama hata mmoja mkoani Pwani, wakati kikijua kwamba uhakiki utafanyika katika mkoa huo ambao ni jirani na Dar es Salaam, yaliko makao makuu yake.

Hiyo inathibitisha kauli ya Kiyabo ya kususia uhakiki na hivyo inawezekana wanachama wakawa wamekatazwa kujitokeza kuhakikiwa, hali ambayo hata hivyo inakiweka katika hali mbaya ya kukosa usajili wa kudumu.

Timu ya uhakiki huo ikiongozwa na Tendwa, ilipowasili jana katika vijiji hivyo, haikukuta mwanachama, kiongozi wala kuona ofisi ya CCJ, mazingira yanayohatarisha usajili wa kudumu wa cghama hicho kilichopania kushiriki uchaguzi mkuu Oktoba mwaka huu.

"CCJ wamekuwa wakipiga kelele kwamba ofisi yangu inawahujumu, haitaki kuwahakiki, wanataka kuwahi uchaguzi, sisi tumejitolea kuwahakiki ili wafanye uchaguzi, lakini ninyi ni mashahidi hali halisi ya uhakiki ndiyo hii," alisema Tendwa.

Alisema pamoja na nia njema ya ofisi yake kufanya uhakiki wa wanachama wa CCJ ili kama hesabu yao itatosha waweze kukipa usajili wa kudumu, chama hicho kimerudi nyuma na kushindwa kutoa ushirikiano kwa ofisi yake na kukosa wanachama katika mikoa kama yalivyokuwa makusudio yao.

"Sisi tumejitolea tuwahakiki wafanye uchaguzi, kama wao wanarudi nyuma tena, hiyo ni bahati mbaya kwao, nia yetu ni nzuri, tungekuwa na ushirikiano mzuri na wao tungemaliza hii vizuri, kama kungekuwa na mkwamo wowote tungeshirikiana kutatua matatizo hayo," alisema Tendwa.

Msajili alisema CCJ katika uhakiki wa Dar es Salaam juzi hawakufanikiwa, Pwani kwa Mathias na Picha ya Ndege hawapo kabisa, hakuna mtu yeyote anayewajua, hawana viongozi wala ofisi.

Alipoulizwa kuna haja gani kuendelea na uhakiki katika mikoa mingine wakati hali imeonesha kuwa mbaya, Tendwa alisema tayari walishapanga, baada ya CCJ kuleta barua iliyopanga maeneo ya kufanyiwa uhakiki waliyodai wanayamudu na kusisitiza kuwa lazima yote yahakikiwe.

Alisema leo watakuwa Ifakara mkoani Morogoro kuendelea na uhakiki na baada ya hapo, watakwenda Unguja na hatimaye watatoa taarifa ya uhakiki wao.

"Nimechukua jukumu hili mimi mwenyewe, nitatenda haki na kutimiza wajibu wangu, kama watashindwa kujitokeza na mikoa mingine, CCJ watakuwa wameshindwa kutekeleza wajibu wao kama chama cha siasa," alisema Tendwa.

Juhudi za kumpata Kiyabo azungumzie mazingira ya wanachama wake kutojitokeza Kibaha jana kuhakikiwa, hazikuzaa matunda kutokana na simu yake kuita bila kupokewa.

ccjusajili.jpg

Mwenyekiti wa Chama Cha Jamii (CCJ) Richard Kiyabo, akizuiwa na mlinzi wake wakati akielekea kwenye meza ya msajili wa vyama, John Tendwa kumlalamikia kuhusu zoezi la kuhakiki wanachama wa chama hicho viwanja vya Temeke Mwembeyanga jijini Dar es Salaam jana. Picha na Silvan Kiwale

Hivi kweli CCJ ina Wanachama halali 13 tu Dar nzima? Kaaz kwer kwer!
Siasa si lele mama, Kugomea kujitokeza na kuhakikiwa na wakati awali ulishakubali na ukatahadharishwa kama hukutokea zoezi litaendelea hii ni kupoteza muelekeo.

Hata kama Tendwa ana lake jambo lkn kitendo cha viongozi wa CCJ kutotokea kwenye uhakiki ktk maeneo ambayo walikubaliana kuhakikiwa inaibua maswali mengi kuhusu umakini wa viongozi na chama chenyewe.

Hakuna mapambano rahisi hasa ya kidemokrasia. Viongozi kuamua kuingia mitini na kuwahamasisha wanachama wasijitokeze kuhakikiwa imeonyesha hali ya kupoteza dira na kutokomaa kifikra na huku ni kufeli kwa hali ya juu. Viongozi kuamua kuingia mitini na hata ofisi hazionekani kunaleta picha ya kwamba hawa viongozi wa CCJ ni wababaishaji na hawakuwa wamejiandaa kuendesha chama.

Wao walifikiri kuendesha siasa ni tambarare na hakutakuwa na dhoruba yeyote. Inasikitisha sana!
 
KNKU, CCJ walishasitisha zoezi la kuhakikiwa baada ya kugundua alichofanya Tendwa Mwembeyanga. Walitangaza kuwa kwa upande wao zoezi hilo lisingeweza kufanyika. Msajili alijua hivyo lakini aliamua kwenda kuhakiki wanachama ambacho chama chao kimewaambia zoezi limesitisihwa na CCJ haitatoa ushirikiano.. Msajili alitarajia kukuta kina nani huko?
 
Waungwana hapa kuna mkono wa sisiemu angalia news hizi-:)

CCJ kumburuza kortini Msajili vyama vya siasa

NA MOSHI LUSONZO
6th June 2010

Wabaini namba za wanachana kubadilishwa

Uongozi wa Chama Cha Jamii (CCJ), umeibuka na kutoa madai ya kufanyiwa hujuma baada ya kugundua namba za wanachama wake zilizokuwa ndani ya fomu za Msajili wa Vyama vya Siasa nchini zimebadilishwa.

Akizungumza na Nipashe jana, Katibu Mkuu wa CCJ, Renatus Muabhi, alisema kutokana na kubainika kwa kasoro hiyo, wamepanga kumfikisha Msajili wa Vyama vya Siasa, John Tendwa mahakamani Jumatatu (kesho) ili asiendelee na zoezi la kuhakiki wanachama wao hadi hapo hali hiyo itakaporekebishwa.

Muabhi alisema, baada ya kuvunjika kwa uhakiki wa wanachama wa Mkoa wa Dar es Salaam kutokana na watu wengi kuonekana sio halali, uongozi umegundua fomu alizokuwa nazo Tendwa nyingi zimebadilishwa namba pamoja na majina ili kuhakikisha kinashindwa kupata wanachama wa kutosha na kunyimwa usajili ya kudumu.

"Kwa kweli tumebaini kuna njama zimefanyika kwa kubadilisha namba kwenye fomu alizokuwa nazo Msajili, lakini hilo litamalizwa kisheria kwa sababu tunatarajia kwenda mahakamani kupinga mchakato wote wa kuhakiki wanachama hadi hapo totakapokaa na kumaliza tatizo hili," alisema Muabhi.

Katika zoezi hilo lililofanyika Jumatano iliyopita katika Viwanja vya Mwembeyanga, wanachama 40 waliofanikiwa kuhakikiwa kabla ya zoezi hilo kusitishwa, 27 walishindwa kutambuliwa na Msajili baada ya kuonekana sio halali na 13 pekee ndio waliotambuliwa.

"Kitu hiki bado kinatuumiza kichwa sisi kama viongozi wa CCJ, haiingii akilini tuwe na wanachama 13 tu ikiwa tulikuwa na maandalizi ya kutosha kabisa, hili jambo lazima tutakwenda mahakamani ikiwa ni pamoja na kumzuia Tendwa asiendelee kuhakiki wanachama wetu bila ridhaa yetu," alisisitiza.

Aidha, alisema ametoa agizo kwa viongozi wa mikoa yote itakayotembelewa na Msajili kutotoa ushirikiano wowote kwa sababu wao wamejitoa.

Aliwataka wanachama wa chama hicho kutulia kwa kuwa ana matumaini makubwa suala hilo litatatuliwa haraka ili uhakiki huo urudiwe kwa mara ya pili.

Hata hivyo, Tendwa alipozungumza wakati akiendelea na zoezi la uhakiki wa chama hicho Ifakara mkoani Morogoro, alisema fomu alizokuwa nazo ni halali kitu ambacho hata viongozi wa CCJ wanakitambua, bali kinachofanyika sasa ni kulidanganya taifa.

Alisema, anachoendelea kukiona katika ziara yake hiyo ni kitu ambacho hakukitarajia, kwani kuanzia uhakiki wa Mkoa wa Pwani hadi alipofika Ifakara jana hakuweza kumpata hata mwanachama mmoja.

"Nadhani CCJ wanaliongopea Taifa, hawa watu hawana wanachama kama wanavyodai, jambo hilo ndilo nakumbana nalo kwenye ziara yangu kuanzia jana (juzi) Kibaha na sasa Ifakara hali ni hiyo hiyo, japokuwa huku nimeona ofisi yao," alisema.

CHANZO: NIPASHE JUMAPILI
 
Tatizo la vyama vyetu vya siasa ni kufikiri CCM watakuja kuwapisha madarakani kirahisi. Siasa ni mapambano. CCJ walipaswa kujua kwamba kuna uwezekanao wa kuchezewa shere na wajiandae kuzuia. Hapa tayari mchezo umekwisha. Wanaenda mahakamani, kesi itatajwa Januari 2011, na itaanza kusikilizwa Mei 2011, Halafu?

Halafu wamelipiga mno debe tupo hadi linawatisha washika mpini. Kulikuwa na ubaya gani kufanya haya silently halafu mnaibuka mkishasajiliwa. Sasa mnatisha kabla hamjazaliwa si mnafanya muendelee kubaki mimba, MM hata wewe hii michezo unashindwa kuisoma?
 
Watanzania hakuna tunaloliweza; tunashindwa hata kupata watu 200 ambao sio mamluki halafu tunaomba tupewe uongozi wa nchi? Very disapointing!

Mbona unageneralise issue!!! imekuwa Watanzania how? kama wewe huwezi ni wewe bwana sio wote!!! come on!!!:angry:
 
kweli inasikitisha sana,kama CCJ wako sawa na wanachosema huyu TENDWA na CCM yake wanatia aibu..........
 
Hizo ni habari za mfa maji haishi kutapatapa, wamakosa umakini wenyewe kwa kukurupuka tena kwa kumlazimisha msajili afanye uhakiki kwa muda wanao taka wao navilio vingi kuwa wanaonewa. msajili kakubali wameboronga wenyewe sasa wanatafuta umaarufu wa huruma kuwa wanaonewa huu ni upuuzi, kibaya zaidi wanakimbilia kusitisha zoezi, jamani humu hamna kitu ni kujaza tu utitiri wa vyama ambavyo havina tija kabisa.sitaki kuamini kama kweli hiki ndio chama watu makini kama dr salmin sita sumaye nk wanaweza kuingia hii ni danganya toto
 
KNKU, CCJ walishasitisha zoezi la kuhakikiwa baada ya kugundua alichofanya Tendwa Mwembeyanga. Walitangaza kuwa kwa upande wao zoezi hilo lisingeweza kufanyika. Msajili alijua hivyo lakini aliamua kwenda kuhakiki wanachama ambacho chama chao kimewaambia zoezi limesitisihwa na CCJ haitatoa ushirikiano.. Msajili alitarajia kukuta kina nani huko?

MMM unanishangaza sana, sasa Tendwa asingefika Kibaha si CCJ wangesema Tendwa hajaenda huko au? Sasa ulitaka Tendwa asikilize Kaulizi za Mdomo za Kiyabo kwamba hamtaendelea na Zoezi
 
Kifupi ni kwamba CCJ wameshindwa kufanya siasa,walidhani ni rahisi kama kunywa maji.Kumkimbia Tendwa hata kama hawakuwa na imani na Tendwa ni kuionyesha jamii kuwa hawawezi mapmbano na yale maneno ya Mwanakijiji kuwa eti CCJ itafanya yale ambayo vyama vya upinzani vimeshindwa kufanya kwa miaka 15 sasa yanatimia..Pamoja na Ujinga wote wa chama cha PPT Maendeleo lakini wao waliweza kufikia masharti..CCJ ilipaswa kuprove kwa Tendwa kwamba wanachama wanao wa kutosha.Wangekubali tu waionyeshe jamii kuwa wanao kwa huo Mkoa wa Pwani na kwingineko..Chama cha Mahakamani,Mtikila part II.
 
Tatizo la vyama vyetu vya siasa ni kufikiri CCM watakuja kuwapisha madarakani kirahisi. Siasa ni mapambano. CCJ walipaswa kujua kwamba kuna uwezekanao wa kuchezewa shere na wajiandae kuzuia. Hapa tayari mchezo umekwisha. Wanaenda mahakamani, kesi itatajwa Januari 2011, na itaanza kusikilizwa Mei 2011, Halafu?

Halafu wamelipiga mno debe tupo hadi linawatisha washika mpini. Kulikuwa na ubaya gani kufanya haya silently halafu mnaibuka mkishasajiliwa. Sasa mnatisha kabla hamjazaliwa si mnafanya muendelee kubaki mimba, MM hata wewe hii michezo unashindwa kuisoma?

siasa za chini chini hazistahili namna hii.. mambo ya chini chini na kutowaambia wananchi nini mtakifanya ndicho kilichowapa CCM kichwa. Watch and Learn.. .the boldness of change..
 
Kifupi ni kwamba CCJ wameshindwa kufanya siasa,walidhani ni rahisi kama kunywa maji.Kumkimbia Tendwa hata kama hawakuwa na imani na Tendwa ni kuionyesha jamii kuwa hawawezi mapmbano na yale maneno ya Mwanakijiji kuwa eti CCJ itafanya yale ambayo vyama vya upinzani vimeshindwa kufanya kwa miaka 15 sasa yanatimia..Pamoja na Ujinga wote wa chama cha PPT Maendeleo lakini wao waliweza kufikia masharti..CCJ ilipaswa kuprove kwa Tendwa kwamba wanachama wanao wa kutosha.Wangekubali tu waionyeshe jamii kuwa wanao kwa huo Mkoa wa Pwani na kwingineko..Chama cha Mahakamani,Mtikila part II.

GS... watch and learn... the boldness of change...
 
Back
Top Bottom