CCJ Kulikoni!?

Ndibalema

JF-Expert Member
Apr 26, 2008
10,956
4,648
Jana katika vyombo mbali mbali vya habari niliona habari juu ya baadhi ya wanachama wa CCJ waliokuwa wana hakikiwa na msajili wa vyama kuwa walighushi, na uanachama wao ni batili.

Cha ajabu nilimwona mwenyekiti wa CCJ akifoka kwa hasira "huyu mzee (Tendwa) ameshindwa kazi, ni bora ajiuzuru"

Huku mwenyekiti huyo akisisitiza kuwa zoezi hilo lighailishwe, lisiendelee tena kwa maeneo mengine.

Maswali yangu kwa CCJ:

1) Nini tatizo kwa hao wanachama (inaosemekana ni) batili
2) Nakumbuka CCJ ilikuwa ikisubiri kwa hamu zoezi hili la uhakiki; Kulikoni tena mnataka zoezi lisiendelee?
3) Mkono wa CCM upo wapi haswa kwa wanachama wanaosemekana ni batili?
 
Kwa kweli hii ishu inachanganya sijui sasa nani kasababisha mambo haya yote!
 
Mimi nakuambieni tutasikia mengi mwaka huu....Hata kama kuna walakini kwenye uhakiki lakini...si amini kama mkono wa siisiiem upo mbali
 
Nilipoiona CCJ mwanzo, niliudharau na kuiona its a hoax, comming to put just another junk on the game ambalo tayari limeshajaa junks!. Alipoingia Mpendazoe, nikajua amekurupuka na kuhama CCM kwa jazba, nilipomsoma Mzee Mwanakijiji, ndipo nikapata shauku ya kweli kuanza kuiamini CCJ might be something realy, something serious and for realy war, japo mpaka sasa sijabahatika kujua ukweli wa who is who is a really CCJ, wanaambiana, wanaitana, na wanajiunga, huku wengine tukishawishiwa kwa ushawishi kuwa CCJ sasa ndio chama mbadala.

Tusiilaumu bure CCJ, kuna uwezekano Tendwa amewashtukiza (surprise check) hivyo walikuwa hawajajiandaa kama walivyo puliza baragumu, ila kama wakipata muda wa kujiandaa vizuri, they'll put their house in order kabla mgeni hajafika.

Lakini pia tusirule out uwezekano wa hii CCJ inayokaguliwa ndio CCJ halisi, achilia mbali CCJ ya kwenye ma Press Conference na wasemaji wake kibao. Kama hii inayoibuka ndio CCJ kweli na halisi, then I was not wrong. CCJ is a hoax!.
 
Mimi nakuambieni tutasikia mengi mwaka huu....Hata kama kuna walakini kwenye uhakiki lakini...si amini kama mkono wa siisiiem upo mbali

Kama mkono wa CCM haupo mbali, upo wapi? kwa tukio la jana CCM imehusikaje?
 
Mimi nakuambieni tutasikia mengi mwaka huu....Hata kama kuna walakini kwenye uhakiki lakini...si amini kama mkono wa siisiiem upo mbali

Bila shaka uko mkono wa CCM. Pengine tatizo ni kwamba CCJ ilivyokuwa launched ilitangazwa sana na kuonekana tishio (iwapo hili ni sahihi au la) kwa CCM. Nandiyo maana Msajili aliagizwa kukihakiki kwa kutumia darubini kali.

Mimi sidhani iwapo chama hicho kingeomba usajili kikawaioda tu kama vile vyama vingine uchwara -- ingepata bila kusita. Tusisahau mwaka 1994 wakati CUF ilipogomea kushiriki uchaguzi mdogo katika jimbo la Kwahani kulikuwa hakuna chama kingine kilichokubali kushiriki dhidi ya CCM, ambayo ilihofu mbele ya jamii la kimataifa kwamba nadharia nzima ya serikali yake kuanzisha kwa demokrasia ya vyama vingi ilikuwa mashakani katika zoezi la kwanza tu la demokrasia hiyo.

Hapo Msajili aliagizwa kukisajili chama cah Dr Che Mponda (TPP) ambacho kilisajiliwa na kupewa usajili wa kudumu ndani ya siku saba tu. ilielezwa eti Dr CheMponda aliweza kupata udhamini wa watu 200 huko Pemba wakati hakuwa ameuza hata kadi moja kule, kufuatana na ripoti za magazeti. alikuwa hata bado hajaprinti kadi za uanachama.

Ni dhahiri serikali ya CCM kama hakitaki chama kusajiliwa, basi hakisajiliwi, na kama itaona kunufaika, basi itasajili vyama vyovyote vile -- tena kimya kimya. Mara ngapi tumeshtukia chama flani etc kimepata usajili wa kudumu. Vyama visivyokuwa na lolote na baada ya kutangazwa tu kupata usajili havisikiki tena.

Ofisi ya Msajili wa Vyama na Tume ua Uchaguzi -NEC -- ni mawakala wa CCM kwani huteuliwa na Mwenyekiti wao, kitu ambacho hata CCm yenyewe inalifahamu na haipewndi kul.ijadil.i kwa kina kurtokana na ukwseli wake.
 
Jana katika vyombo mbali mbali vya habari niliona habari juu ya baadhi ya wanachama wa CCJ waliokuwa wana hakikiwa na msajili wa vyama kuwa walighushi, na uanachama wao ni batili.
Cha ajabu nilimwona mwenyekiti wa CCJ akifoka kwa hasira "huyu mzee(Tendwa) ameshindwa kazi, ni bora ajiuzuru"
Huku mwenyekiti huyo akisisitiza kuwa zoezi hilo lighailishwe, lisiendelee tena kwa maeneo mengine.
Maswali yangu kwa CCJ.
1)Nini tatizo kwa hao wanachama (inaosemekana ni) batili
2)Nakumbuka CCJ ilikuwa ikisubiri kwa hamu zoezi hili la uhakiki
Kulikoni tena mnataka zoezi lisiendelee?
3) Mkono wa CCM upo wapi haswa kwa wanachama wanaosemekana ni batili?

Kaka mimi pia nina maswali kama yako sipati majibu kamili - sasa CCM ndiyo ilikuwa inachapisha majina? kwamba kwenye Kitambulisha Juma Bakari kwenye daftari la uhakiki Bakari Salum na kwenye kadi ya CCJ Salum Abubakhari - hapa nafikiri kuna uzembe ulifanyika.

a) Kwa nini Chama kisingeakiki chenyewe kwanza ndani kabla ya kumwita msajiri?
b) Ningekuwa mimi tendwa ningewaambia wamalize kuhakiki majina yao kwanza then waniite nipite mikoa iliyobakia.

Tungepata mtu wa CCJ atuthibitishie kuwa hili la majina feki ni kweli hujuma za CCM na Tendwa mwenyewe kutotaka wasishiriki uchaguzi mkuu ingekaa vizuri zaidi.

Hiki ndicho chama mbadala kama kinavyojiita ambacho kinataka kuchukua uongozi wa taifa hili hata kuhakiki majina ya wanachama wao tena wa Dar tu ni shughuli? Guys...
 
Tusubiri maana walisema watafanya kile ambacho wengine wameshindwa kufanya
 
Wajitokeze CCJ wenyewe kama wapo. Vinginevyo hawa ma-novice wa siasa waliowatanguliza wanawaharibia saana tu.
 
tusiutafute mkono wa sisiemu kwa kuangalia matukio ya jana
tukumbuke kuwa hiki chama, 'sisiemu' si chama cha siasa kwa mtazamo wa ndani zaidi,
ukikitafakari sana na kukichambua, muundo mpaka mwenendo wa siasa zake,
utagundua kuwa ni chama cha kijasusi, hapo kipo kama kawaida kinacheza mchezo wake,
mchafu.
 
Bado tunarudi pale pele, CCM kinacheza mchezo mchafu, sawa. Wapi?
Swali halijibiwi inakuwa tunakariri tu kuwa CCM inacheza mchezo mchafu.
Mtu athibitishe basi kwa hili la CCJ.
 
Bado tunarudi pale pele, CCM kinacheza mchezo mchafu, sawa. Wapi?
Swali halijibiwi inakuwa tunakariri tu kuwa CCM inacheza mchezo mchafu.
Mtu athibitishe basi kwa hili la CCJ.
Mkuu Ndibalema,
ushahidi unao utaka hapa hutaukuta, wala usitegemee kuuona openly kama unvyotaka kuuona.

Kitu ninachoweza kukupa, labda ni kukumbusha kuwa sisiemu ndiyo iloshika serikali hivyo imemeza taasisi nyingi sana, ikiwa jeshi lapolisi, mahakama n.k vimeshikwa na serikali ya sisiemu; vipi kwa Tendwa?

Kwa macho ya nyama na masikio huwezi kuuona uchafu wa hiki chama, ni mpaka uruhusu fikra zako kuchungulia ndani zaidi, Bunge tu halina ubavu kwa sisiemu, tume za uchaguzi tu hazina ubavu kwa sisiemu awe Tendwa?

Usishangae akawa ana represent kile kilichoaandaliwa na sisiemu kwa manufaa yake, ila ushahidi unaotakuona hapa, mimi nina hakika huwezi kuupata kwa mtazamo wako.
 
CCJ watoe kwanza kibanzi katika jicho lao kabla ya kuonesha boriti iliyokatika jicho la CCM!

Mimi hapa sioni mantiki ya CCJ kulalamikia Mkono wa CCM kwenye zoezi hili, ni wazi hakuna ushahidi na wala maelezo yao hayawezi kukidhi haja ya mtu mwenye kufikiri sawasawa, kuvurugika kwa lile zoezi CCJ have themselves to blame, there is no need of CCJ to start witch hunting in CCm or somewhereelse, the witch they are looking for is inside their part! Ni uzembe wao wenyewe, kama walishajua kuwa kuna mbinu chafu toka mwanzo si wangejiridhisha wenyewe kwanza kuwa kilakitu kiko sawa kabla ya kumuita Tendwa!

Ni upuuzi kwa CCJ kuendelea kuinyooshea kidole CCM kwa makosa yao wenyewe, mimi nahis CCJ wants to seek for public sympath by pointing a finger to CCM! Jamani not all evil doings are devils acts, some of them are from our own feelings and desire! Siipendi CCM, sio shabiki wa CCM, lakini kwa hili hapana!
 
Kazi kweli kweli, mi narudia kauli ya KIDUMU CHAMA, hii imekuwa kama ngao yao ya kufanya kila hali kisitoke madarakani. CCJ inabidi wapigane kiume ili kupata usajili, si umemsikia Makamba alivyosema jana, kasema na bado tutaonana oktoba.
 
CCJ watoe kwanza kibanzi katika jicho lao kabla ya kuonesha boriti iliyokatika jicho la CCM!

Mimi hapa sioni mantiki ya CCJ kulalamikia Mkono wa CCM kwenye zoezi hili, ni wazi hakuna ushahidi na wala maelezo yao hayawezi kukidhi haja ya mtu mwenye kufikiri sawasawa, kuvurugika kwa lile zoezi CCJ have themselves to blame, there is no need of CCJ to start witch hunting in CCm or somewhereelse, the witch they are looking for is inside their part! Ni uzembe wao wenyewe, kama walishajua kuwa kuna mbinu chafu toka mwanzo si wangejiridhisha wenyewe kwanza kuwa kilakitu kiko sawa kabla ya kumuita Tendwa!

Ni upuuzi kwa CCJ kuendelea kuinyooshea kidole CCM kwa makosa yao wenyewe, mimi nahis CCJ wants to seek for public sympath by pointing a finger to CCM! Jamani not all evil doings are devils acts, some of them are from our own feelings and desire! Siipendi CCM, sio shabiki wa CCM, lakini kwa hili hapana!

Walikuwa wanahangaika na kujibu matamko ya kwenye vyombo vya habari kwanza. Wekeni CVs za hawa viongozi wa muda wa CCJ. Mimi naona tatizo linaanzia kwa hawa.

Wanababaika, wanahamanika, hawajiamini, hawazijui siasa za bongo, wanajifunzia UONGOZI hapa, sasa hivi.
 
Inasikitisha kuona hawa CCJ wameshindwa kuorodhesha na kuhakiki wanachama wao 200 kwa Dar tu, ilhali ni wao ndio wamemladhimisha Tendwa aje kuwahakiki wako tayari na wanachama 2,000 Dar, acoording to their chairman. Sasa hapa mwenyekiti wao analalamika Tendwa hawezi kazi ilhali wanachama wao feki na real hawafiki hata 150 hapo mkutanoni. Na hata yeye na katibu wake hawana kadi!

Huu ni uzembe wa hali ya juu, period.

Kuna mtu awali alilinganisha na chama cha chemponda in 1994, sasa kweli wakati ule ccm ilikuwa inajaribu kulazimisha vyama vingi na kufungia macho those things, we are in 2010 tunataka responsible upinzani ambao wataweza kuorganise na kutetea jamii yenye watu takriban 40 million, sasa kama hata kuorganise watu 200 inakuwa taabu, jee siasa za kitaifa wataweza kweli?

Na sioni namna ccm inahusika na uanachama batili, ccj iombe ushauri cuf jinsi ya kuorodhesha wanachama na kuhakiki, wana uzoefu mkubwa hasa visiwani.
 
Back
Top Bottom