CCJ kuanza Charm offensive! - Ask your questions!

This might be a stupid question though I don't believe there is a stupid question...what does CCJ stand for? I know it has been mentioned somewhere but I forgot and I'm just being too lazy to look for it...
 
kwa kweli siwezi kuzungumzia hisia za mtu mwingine.. sijui yeye Tendwa anajichukuliaje.
nazungumzia reality na si hisia,kawekwa na Raisi na kama raisi akitaka msipewe usajili inawezekana,na kama mkipewa usajili,bado itabidi niendelee kufana utafiti kama ni mapandikizi ama la!



I will not claim that with such an absolute certainty.

Kwahiyo ni watu wa CCJ ambao walitoa taarifa za EPA nk?Ama pale mwembe yanga ilikuwa ni photocopy ya Slaa!Eeee Eh!Kaazi!



Well.. ipo misingi na ni misingi ya kiitikadi.
Ungekuwa specific,una maana ipo misingi ya kiitikadi ambayo inaweza kuwaunganisha ama itabidi muandae misingi hiyo...Maana kusema misingi ipo haimaanishi kuwa kuna chama mnachoendana nacho kiitikadi kwenye upinzani,sana sana mnaendana na ccm kuliko chama kingine chochote!


Thanks!However kama ulivyosema hapo juu,ni lazima kuwe na misingi ya kiitikadi,hilo daraja mtakuja jua siku ya kulijenga lini?Ni lini haswa tunaweza kujua kuhusu usajili wa kudumu?Pia kama ccm ndio chama kinachoendana zaidi na nyie kiitikadi,itakuwaje?
 
Wakuu wanaCCJ, mimi nina swali moja

kunako miaka ya 80 Tanzania ilikubali masharti ya mikopo/misaada ya nje hasa kutoka Banki kuu ya dunia na Shirika la Fedha(IMF), masharti hayo yamesababisha umilikishaji wa mali (privazatation) na mabadiliko mengine mengi yanayoongeza dhiki katika maisha ya kila siku ya mtanzania wa kawaida na kuzidi kuwaneemesha matajiri wa ndani na nje ya nchi. Masharti hayo pia yamepunguza au kuondoa nguvu ya dola katika kufanya maamuzi. kwa uelewa wangu misaada/mikopo hiyo ina changia zaidi ya asilimia 30 ya bajeti ya serikali lakini masharti yake kupitia mikakati kama MKUKUTA yana husisha bajeti yote kwa ujumla.

sidhani nchi inaweza kuboresha maisha ya maskini walio wengi kama maamuzi ya nini kinahitaji kufanyika ndani ya nchi ili kuinua maisha ya ho maskini yanafanywa kwa kuzingatia faida watakayopata matajiri wachache.

Je? CCJ ikiwa na itikadi za self reliance na kukomesha exploitation ya aina zote, ina mikakati au msimamo gani kuhusiana na suala hili la nchi kutegemea misaada/mikopo yenye masharti yanayonufaisha matajiri?
 
Mwalimu hakupenda maswali nadhani wame adapt na hilo,hilo lilipelekea anguko kwasababu alijipatia "mr yeses" sera zao nzuri tu kama za ccm,lakini hawaonyeshi kama wata act tofauti na kile kilichowaaangusha hapo awali!
Sasa ni fisadi gani ccm aliyekuwa akijulikana wakati wa kuanza siasa?every almost one of them had a point that nobody knew em before! Mtakavyo act nakubehave tofauti towards wananchi ndicho kitakachowaletea utofauti!
Na pointi yenu ya "free enterprise bado hamjasema how is it compatble with African socisalism?

Maana juzi tu hapa kulikuwa na mjadala unaohusiana na mandatory listing of shares from the foreign companies!
Ni vizuri mkawa "Humble" Kama kuna maswali yanayojeorpodize strategies zenu za kisiasa kwa wananchi,then just let the people know what are the implications,na kama hamtaki kuwa specific kwenye implications hizo,the just we cant tell you now for sure!kwasababu msi assume kila mtu ana nia mbaya na hivyo mkaona maswali hayafai,hayo yalipeleka members wengine kuamini kuwa hii ni foruma ya chadema!na kama pia mnadhani ni ya kipuuzi tuelezane wazi tu,siwezi kwenda personal kwasababu nitaheshimu maoni hayo coz i dont belive in human perfection,rather i blieve in "human excellency!" thats the one to strive for its achievable,perfection?Mnh! i dont believe in it!

Naamini kama mtaendelea na "Madharau yenu na kufavor just vijimaswali rahisi vyenye kua analyze more what you actually going to dovijimaswali ambavyo vilipelekea eventuall JK kuambiwa amnunua waandishi flani flani ama maswali ya kuandaliana na wanaojuana,itikadi's are just in papers simlar to how TANU and later ccm did,this time you sholud do it differentlymwalimu was trulyy excellent but not perfect,Jesusu Christ himself wasnt,coz chini ya mwalimu,kutokukubaliwa/kutokuuliza kwa maswali muhimu was based on the fear of being called a traitor to a Nation by just asking hard questions, and the "belief of perfection"then we're trouble if you dont change that cause,you should also comply to real questions on real changes
 
MKJJ taratibu mkuu...CCJ ni changa sana, pamoja na hayo naona kuna usanii wa kibongo hapa, hao wanaojulikana kama viongozi waanzilishi wa chama wanasema wao wametumwa tu (tunaambiwa wenyewe wamejificha nyuma yao) kwa hiyo hao waliojificha bado ni kitendawili tulicho achiwa tutegue, MKJJ unajaribu kukisifia lakini katika maelezo na majibu yako naona pia umepigapiga tu...Madudu ya Chadema, CCM, CUF, , NCCR, TLP, n.k yanajulikana baada ya wao kuwa kwenye ligi kwa muda. Sasa hiki CCJ (ukiondoa Mh. Mpendazoe) eleza ni vipi chama kichanga kama hichi kilicho anzishwa haraka haraka huku hao waasisi wakiwa wamejificha kinavyoweza kujijenga chenyewe within 6 months, kuchukua nchi na kufanikiwa kutekeleza sera zake kikamilifu au kuendesha nchi.. support ya MKJJ pekee siyo kigezo cha ubora wa chama, mtu anaweza kuwa na interest zake kwenye chama hicho...ubora utategemea hao waliojificha kama kweli wanauwezo wa kutekeleza hayo mnayo tuambia.....isije ikawa mbinu tu ya kukusanya wanachama, kitu ambacho ni hatari sana, chama kimeanza kwa kasi na kinawezapotea kwa kasi hiyo hiyo...
 
Mzee Mwanakijiji,
Nimesubiri sana maelezo yako naona kimyaaaa lakini hata hivyo yanibidi kuweka dukuduku zangu. Kwanza ni lazima mfahamu maneno haya - Umoja ni nguvu, Utengano ni Udhaifu.
Ujio wa CCJ unazidi kutugawa Watanzania zaidi na kuondoa kabisa maana ya Demokrasia ktk misingi ya Mrengo. Demokrasia inahusu zaidi uhuru wa ushindani baina ya mirengo ya vyama na sio kubasilisha sura za viongozi kujenga madhehebu ndani ya chama au mrengo kimoja.

Watakao furahia zaidi Ujio wa CCJ ni CCM ambao kwa uhakika CCJ itawahakikishia Ushindi. Nina hakika kabisa kwamba CCJ itachukua kura za Chadema,NCCR na CUF zaidi ya CCM wenyewe. Hata nchi magwiji wa Demokrasia wana vyama viwili vikubwa vyama vyenye mirengo miwili tofauti kisera na pale kinapoongezeka kimoja kuwa vitatu mshindi mara zote ni Conservative.

Tazama UK mimi naamini kabisa ujio wa nguvu wa chama cha demokrasia ilikuwa kugawa kura za Labour party pande mbili kwa sababu hakuna mpenzi wa Conservative anaweza pigia kura labour au Demoktratic isipokuwa vyama hivyo viwili kugawana kura zao. Kama ingekuwa ni Labour tu against Conservative nia hakika Conservative wasingeshinda kabisa.

Maombi yangu siku zote ni muungano wa vyama vya Upinzani na maadam haikutokea hivyo nguvu zangu zote nimezihamishia kwa mgombea URAIS jambo ambalo pia linaanza kunitumbukia nyongo kwani Wadanganyika wamejaa UJINGA na ULIMBUKENI ulowakwaza ktk umaskini. Na bahati mbaya sina uwezo mkubwa wa kujieleza nikapokelewa kimawazo pamoja na kwamba ukweli upo wazi kabisa.. Ujio wa CCJ ni Uhakika kwa CCM kushinda uchaguzi huu na nitasema tena Kikwete atapita bila kupingwa kutokana na Ujinga kama huu.

Mkuu wangu kama CCJ ina vigogo ndani yake wanaotaka kuiondoa CCM ni lazima wajiunge ktk mapambano na vyama vya Upinzani hata kama wana vichwa kama Malecela, Salim, Butiku, Mwakyembe au Mpendazoe. CCM wanajua sana kuwamaliza watu kama hawa kisiasa na itakuwa kazi ndogo sana kuzigawa kura baina ya CCJ,Chadema,CUF na NCCR.. Vyama vinavyozidi kuwa vingi ndivyo kunarahisisha ushindi wa chama tawala. Hakuna nchi hata moja duniani imeweza kukiondoa chama tawala kwa Ushindani wenye vyama zaidi ya vitatu..Na hasa inapokosekana chama Mbadala cha Upinzani kinachokosa baraka za Wapinzani.

Nitarudia kusema hivi, Ujio wa CCJ ni Ushindi mkubwa wa CCM na Kikwete na pengine ndio maana JK alisema hana haja ya kura za wafanyakazi akijua wazi kampeni zinazoendelea sii kumwangusha yeye bali kujikanyaga sisi wenyewe..JK ana kazi moja ndogo sana anatakiwa kuifanya na nina hakika ataifanya wala sii muda kurudisha Umaarufu wake. Just wait...U all loosers! Kama mwaujua huu, Mkwere ajua kupekecha kwa nyuma.
 
Hii ni technically "ccm b" ama "ccm minus mafisadi" ama wenye kula!Lakini kama vile vijitabia vya viongozi wanafiki wa ccm vikiendelezwa humo ccj,"naona kuna dlili hizo"then hatwendi mahali coz tatizo ni uongozi,watu wa ccj mna confidence ya hali ya juu,lakini msipojibu maswali inavyotakikana mnadhani itakuwa vipi? chadema wamekuwa wakiandamwa na issues kuhusu ukabila,lakini hawajajibu vya kutosha kutokana na seriousness na jinsi issue hiyo inavyotumika dhidi yao na wapinzani kuhusu tuhuma za ukabila,kelele ziko nyingi sana zenye ku justify mabadiloko flani flani ili kuondoa mzozo unawao wacost wapiga kura walio wengi,nao nadhani ni yale yale ya nyuma ya viongozi wa "ccm A" wanazoziona kuwa wako perfect ama hazina umuhimu kwasababu wana amini si kweli AMA HAZIWANUFAISHI WALIOKO MADARAKANI.....

Nadhani back to ccj,wengi ni wale waumini wa ile kauli ya mwalimu kuwa "ccm ndiyo itatoa upinzani wa kweli" Pengine MWALIMU akihofia itikadi zake kufa moja kwa moja,na pia akiamini kuna wanafuzni wake ie kina Mkapa watafanya vyema, Thats true,lakini mwalimu huyo huyo alituwekea Mkapa ambaye naye aliyulet down all the way,SI KWELI WENYE KUKUSIFU TU NA BILA KUULIZA MASWALI MUHIMU BASI NI VIONGOZI WAZURI kama ilivyoelekea mwalimu kuamini,mwalimu alikuwa na tatizo la kuwatambua wakweli na wanaoamini itikadi zale kiukweli, sema aliogopa kwamba maswali magumu ama too much questioning leads to rebelion! ama a traitor who just wana beleive in western mescenaries..i believe in mwalimu lakini nataka kujua ni yepi ya tofauti kwenye yale madhaifu yalimomwangusha mwalimu na ambayo mna mpango wa kuyafanyia kazi ama marekebisho! is it so hard?
 
Nyani Ngabu usijidai eti ulikuwa hujui kirefu cha CJJ,all the details ulizonazo ambazo mwananchama mwanzilishi anakubaliana na wewe mnaonyesha biasness hapa,ndivyo mlivyo,Huwezi kuleta propaganda hapa JF,JF ni kipimo cha the highest level of all kinds and ways of thinking!Sikuchagulii cha kuuliza dont get mi wrong!Lakini based on your previous postings,kama ni kweli ulikuwa hujui maana ama kirefu cha ccj,basi lingekuwa swali lako la kwanza....Yale yale tu!Ndivyo mlivyo!
 
Nyani Ngabu usijidai eti ulikuwa hujui kirefu cha CJJ,all the details ulizonazo ambazo mwananchama mwanzilishi anakubaliana na wewe mnaonyesha biasness hapa,ndivyo mlivyo,Huwezi kuleta propaganda hapa JF,JF ni kipimo cha the highest level of all kinds and ways of thinking!Sikuchagulii cha kuuliza dont get mi wrong!Lakini based on your previous postings,kama ni kweli ulikuwa hujui maana ama kirefu cha ccj,basi lingekuwa swali lako la kwanza....Yale yale tu!Ndivyo mlivyo!

Mangi wewe sijui leo umebugia vikombe vingapi mbege? Hiki chama ni kipya na sitashangaa kama watu wengi hawajui kirefu chake. Hizo itikadi mimi nimekuwa nazo hata kabla ya kujua kuna mtu anaitwa Mwanakijiji. Sasa sijui "biasness" inatoka wapi na propaganda zinatoka wapi katika mimi kuuliza kirefu cha CCJ. Na huwezi kunipangia mpangilio wangu wa kuuliza maswali. Mimi nauliza kwa kadri yanavyonijia kichwani.

Punguza jazba na hisia. Upokeaji wako wa mambo ni wa kihisia zaidi kuliko kiakili. Nimeuliza kwa nia njema kabisa ya kutaka kujua kirefu chake baada ya kugundua kuwa siifahamu. Sasa Mwanakijiji amesema tuulize yote ambayo tungependa kujua kuhusu CCJ. Ubaya uko wapi kwa mimi kuuliza kirefu chake ni nini kama sikijui?
 
Kwa sasa hatuwezi tegemea mengi kutoka kwa hiki chama. Mimi nadhani hii miaka mitano ijayo mpanga uchaguzi wa 2015 utakuwa muda mzuri wa kuona mwelekeo wa chama. Mimi binafsi sijachukua kadi ya uwanachama mpaka nione mwelekeo wao ndani ya miaka hii mitano ijayo. Watanzania tuache kulimbukia, tuwe na misimamo na uwezo wa kuangalia chuya ziko wapi na mchele uko wapi. CCJ mpaka sasa hivi bado ni chama changa sana, swali je wataweza kukidondosha CCM na vyama vingine vya siasa vilivyobaki jina tu, kama NCCR, TLP n.k

Tusome katiba ya chama, tukielewe manake hapo watapokuja kututembelea wakijitambulisha tuwe na maswali ya msingi, sio kuwasikiliza tu na kusema ndio mzee. Lazima tuwabane, na namna pekee ni kuijua katiba yao vizuri lasivyo tutabuluzwa tu. Vyama vya siasa bongo mtelezo kwani sisi wananchi hatufanyi homework zetu kujua nini kinaendelea.

Vijana FM | Karibuni
 
Mangi wewe sijui leo umebugia vikombe vingapi mbege? Hiki chama ni kipya na sitashangaa kama watu wengi hawajui kirefu chake. Hizo itikadi mimi nimekuwa nazo hata kabla ya kujua kuna mtu anaitwa Mwanakijiji. Sasa sijui "biasness" inatoka wapi na propaganda zinatoka wapi katika mimi kuuliza kirefu cha CCJ. Na huwezi kunipangia mpangilio wangu wa kuuliza maswali. Mimi nauliza kwa kadri yanavyonijia kichwani.

Punguza jazba na hisia. Upokeaji wako wa mambo ni wa kihisia zaidi kuliko kiakili. Nimeuliza kwa nia njema kabisa ya kutaka kujua kirefu chake baada ya kugundua kuwa siifahamu. Sasa Mwanakijiji amesema tuulize yote ambayo tungependa kujua kuhusu CCJ. Ubaya uko wapi kwa mimi kuuliza kirefu chake ni nini kama sikijui?
"unnanana sana na mwanakijiji" unajitahidi sometimes "wewe si yeye" naamini kuna watu wana majina mawili mawili kwasababu ya unafiki!wanajidai wao ni perfect kwasana na badala ya kutumia majina yao wanayoheshimika nayo na kuwa real watever da ef case,wanakuwa macowrds na kuwa feki kuandika ujinga na matusi!i havent bought it,lakini i dont really give a rat ass about mi,i am real and i'ma ef satayin da ef real 4ever, im mi so wat?na sina haja ya kutumia many than one name about it,eti hisia zaidi ya akili,wewe ndio unahisi niko juu ya mbege na kuhisi kwamba naendeshwa na hisia! we mdosi tu very out of touch!

We ni mtu wa mtandaoni na hauna mwelekeo wa kuwaza kama mwananchi wa kawaida,mwananchi ambaye hata chama hicho chama cha ccj ndiyo kina watarget zaidi.

Nilishakwambia kuwa sikupangii nini cha kusema lakini bado umerudia kusema kuwa nakupangia cha kusema! Si unaongozwa na "kwenda personal all the time mtu anapo question somthing on your post!

Logically kama uko very interested na mambo mengine kabla hata ya jua jina la chama(kwasababu majina mara nyingi hubeba mwelekeo wa chama) mategemeo ni kwamba ungeshajua tayari jina la chama,maswali uliyoyauliza hapo nyuma yanatoa mwelekeo kwamba ulitakiwa uwe ushajua info hiyo,na si hisia....we cjui mtanzania gani?mara nyingi unapost out touch "shit" fareal! Na kama mtu unayeshinda hapa JF kujidai kwamba hujui ni nafiki mtupu,tulikuwa kule kwnye mjadala wa kuhusu ccj na maelezo yalitolewa wazi kabisa kuwa ccj stands for chama cha jamii,na wengine kuanza kuspeculte "sisije?"

Mwisho kwasababu ya anynomity kuruhusiwa hapa JF, STILL I AINT NO PUBLIC FIGURE,or a celebrity we unahisi evry day mi ni mchaga,na mimi sikutaka kuhisi kwamba wewe ni mwanakijiji,mgoni ama ama mwenyeji wa mtwara, i always that aint da case coz yu sound flani hivi msikufiche!

Yani wewe unakubaliana na mwanakijiji kwamba ni hisia watu wanaongozwa nazo ukanitolea mimi mfano na yeye hapo awali akidai eti hajui hisia za Tendwa kwa maana akiamini kuwa anaongoza kwa hisia,lakini kwasababu ya ushabiki wako wa "kishoga shoga" ushanigeukia mimi na kudai naongozwa na hisia badala ya si akili, hapo sishangazwi coz nilisha mention biasness yako,na vijimaswali vyako rahisi rahisi ambavyo ni vya kufurahishana kama vile viko pre arraanged,mtapewa nchi watu ambao hamjui namna ya ku react?aaegh,halafu tusije kushangaa na fikra zako za "Kinyani" ukapewa uongozi ama kaposition flani hivi kifisadi fisadu,bado safari ni ndefu kama eti we ndo mwenye akili!

Ukiona hivyo basi perfomance yetu ya uelewa ni ya kushtusha!
Very out of touch on real and normal Tanzanians lives,mtandao peke yake hautoshi kuyajua mambo flani flani.
Kwa kusema natumia hisia bila akili huo ni us**** wa kiakili!

Sometimes una vijimaneno vya "kishoga shoga" sikufichi mkuu,neat pickin*2 za kipuuzi puzi tu,mara sijui how i type,eti sijui mangi kuwa hivi ama vile,ooh cjui grow up and all dat ef crap,unapenda kupeleka watu personal sana,unajuwa wewe umefungiwa mara ngapi kwa mambo ya kipuuzi?Juzi tu umetoka kwenye "Ujulius" na kurudia "Unyani" wewe ndiye ambaye you dont grow up,n you still ef da same,huna haja ya kuniambai eti you had itikadi kabla ya kumjua mwanakijiji,under you anyonymity your ass can be enybody" so dont fool me "fool."

Acha upuuzi subiri majibu,nilishakwambia sikupangii cha kusema na we ndo "mjinga" kwa kutokusoma postings za wenzako vyema,hujui kuna watanzania wa tofauti humu we ni muhindi unayejibambikizia Utanzania na kuinsult uafrika,halafu ukijidai eti hiyo ndo akili!
:brick:
Mwanakijiji naye anadai eti hajawhi kukishabikia cama chochote cha kisiasa ccj ndo cha kwanzaa!eti nini?
Halafu pia anadai nisiseseme for a certain kwamba Dr Slaa ametoa mchango mkubwa sana kuhusiana na kuibuliwa kwa issue za ufisadi na kuwa na msimamo ule ule wa kizalendo hadi sasa,usiyo yumba,kamwe hatuwezi kuwatupa wazalendo eti kisa kuna chama kipya na watu wasiojibu maswali hapa,na kwamba eti kutokujulikana kwao ndo jambo zuri?Slaa anaheshimu watu humu ndani he's down to earth licha ya umaarufu wote alionao na anajibu maswali vyema bila vijimadharau,hao viongozi wa ccj wanamtumia mwanakijiji kwasababu wao anadai eti wamo humu lakini nadhani kwa majina bandia ama kama guests!
Tutasimamia misingi na hoja za maswali yetu tukipewa nafasi hiyo!

BTW your "ass" backwards....Unasoma kitabu kabla ya title na labda mwandishi?Acha uzembe Nyani na kuita wenzio wajinga maana wewe ndo tafsiri hiyo uliyoiweka hapo juu kuhusu mimi!
 
Unafanana sana na mwanakijiji,unajitahidi sometimes kujionyesha kwama "wewe si yeye" naamini kuna watu wana majina mawili mawili kwasababu ya unafiki!wanajidai wao ni perfect kwasana na badala ya kutumia majina yao wanayoheshika nayo kuwa real watever ef case,wanakuwa macowrds na kuwa feki kuandika ujinga na matusi!i havent bought it,lakini i dont really give a rat ass about mi,i am real and i'ma ef ef satayin da ef real 4ever, im mi so wat?na sina haja ya kutumia many than one name about it,eti hisia zaidi ya akili,wewe ndio unahisi niko juu ya mbege na kuhisi kwamba naendeshwa na hisia!

We ni mtu wa mtandaoni na hauna mwelekeo wa kuwaza kama mwananchi wa kawaida,mwananchi ambaye hata chama hicho chama cha ccj ndiyo kina watarget zaidi.

Nilishakwambia kuwa sikupangii nini cha kusema lakini bado umerudia kusema kuwa nakupangia cha kusema! S unaongozwa na "kwenda personal all the time mt anapoquestion somthing on your post!

Logically kama uko very interested na mambo mengine kabla hata ya jua jina la chama(kwasababu majina mara nyingi hubeba mwelekeo wa chama) mategemeo ni kwamba ungeshajua tayari jina la chama,maswali uliyoyauliza hapo nyuma yanatoa mwelekeo kwamba ulitakiwa uwe ushajua info hiyo,na si hisia....we cjui mtanzania gani?mara nyingi unapost out touch "shit" farea!

Mwisho kwasababu ya anynomit kuruhsiwa hapa,mimi si public figure,hivo hunijui,hata hivyo bado unahisi everyday mimi ni mchagga,na mimi sikutaka kuhisi kwamba wewe ni Nwanakijiji,i wish its bot that,kwasababu unasound ka mdosi flani nsikufiche!
Veru out of touch on real and normal Tanzanians lives,mtandao peke yake hautoshi kuyajua mambo flani flani.
Kwa kusema natumia hisia bila akili huo ni us**** wa kiakili!

Sometimes una vijimaneno vya "kishoga shoga" sikufichi mkuu,neat pickin*2 za kipuuzi puzi tu,mara sijui how i type,eti sijui mangi kuwa hivi ama vile,ooh cjui grow up and all dat ef crap,unapenda kupeleka watu personal sana,unajuwa wewe umefungiwa mara ngapi kwa mambo ya kipuuzi?Juzi tu umetoka kwenye "Ujulius" na kurudia "Unyani" wewe ndiye ambaye you dont grow up,n you still ef da same,huna haja ya kuniambai eti you hadi itikadi kabla ya kumjua mwanakijiji,under you anyonymity your ass can be enybody" so dont fool me fool.

Acha upuuzi subiri majibu,nilishakwambi sikupangii cha kusema na we ndo "mjinga" kwa kutokusoma postings za wenzako vyema,hujui kuna watanzania wa tofauti humu we ni muhindi unayejibambikizia Utanzania na kuinsult uafrika,halafu ukijidai eti hiyo ndo akili!
:brick:
Mwanakijiji naye anadai eti hajawhi kukishabikia cama chochote cha kisiasa ccj ndo cha kwana!eti nini?
Halafu pia anadai miseseme for a certain kwamba Dr Slaa ametoa mchango mkubwa sana kuhusiana na kuibuliwa kwa issue za ufisadi na kuwa na msimam ule ule wa kizalemdo hadi sasa,kamwe hatuwezi kuwatupa wazaoendo eti kisa kuna chama kipya na watu wasiojibu maswali hapa,Slaa anahehimu watu humu ndani he's down to earth licha ya umaarufu wote alionao na anajibu maswali vyema bila vijimadharau,hao viongozi wa ccj wanamtumia mwanakijiji kwasababu wao anadai eti wamo humu lakini nadhani kwa majina bandia ama kama guests!
Tutasimamia misingi naja za maswali yetutukipewa nafasi hiyo!

Brevity is the soul of wit. Remember that...Lol

Kama nafanana sana na Mwanakijiji hilo si kosa langu wala lake. Na sijui ndio una imply kwamba mimi ndio yeye. Mimi sio yeye na wala sitaki kuwa yeye. Kufanana kwa maono ya kiitikadi ni kitu cha kawaida na hakumaanishi mimi na yeye kuwa ni mtu mmoja.

Asante kwa mitusi yako. Unazidi kuthibitisha kile nilichokisema kuwa unapokea mambo kwa hisia zaidi. Najitayarisha kupokea matusi zaidi.
 
Siwezi kuamini kwamba mzee Mwanakijij hujui kuwa CCJ sio chama mbadala kwa Tanzania yetu labda kama anatusanifu tu.
 
Siwezi kuamini kwamba mzee Mwanakijij hujui kuwa CCJ sio chama mbadala kwa Tanzania yetu labda kama anatusanifu tu.

Huyo Mwanakijiji ana cheza na akili za watu humu,hivi hapa wana JF mliopo nchini mnaozunguka mitaani manzese ,kariakoo, kimara na vijijini watu wangapi wanaiunga mkono CCJ?Mimi nazunguka sana vijijini watu wana hata habari ya CCJ wapo busy kujisajili kwenye matawi ya ccm kwa ajili ya kupiga kura za maoni kwa wana ccm!
Watu humu wanarushiana maneno wana chezewa akili na mwanakjiji tu!
 
Brevity is the soul of wit. Remember that...Lol

Kama nafanana sana na Mwanakijiji hilo si kosa langu wala lake. Na sijui ndio una imply kwamba mimi ndio yeye. Mimi sio yeye na wala sitaki kuwa yeye. Kufanana kwa maono ya kiitikadi ni kitu cha kawaida na hakumaanishi mimi na yeye kuwa ni mtu mmoja.

Asante kwa mitusi yako. Unazidi kuthibitisha kile nilichokisema kuwa unapokea mambo kwa hisia zaidi. Najitayarisha kupokea matusi zaidi.

Hakuna pahalz nimekutukana,wewe si una akili na unatumia akili all the time?ama mdosi ni tusi?na hakuna lolote kuhusu hisia kwenyeposting yangu ya mwisho,we si unapenda hivyo?na nilishasmea niliji conkludia kuwa we si mwnakijiji kwasababu sipendi iwe hivyo so mostly bcoz of anyonymity!which i respect na hivyo siwezi kuhisi mtu ni kabila flabi ama ni mtu flani aliyejiunga hapa JF,sheria za JF zinawalinda wote wenye majina huru na ya ukweli,kumbuka uhuru ndo kipimo kiku cha mwanadamu mweny:painkiller:e fikra huru.
sina haja ya matusi wewe usha imply kuwa mimi ni mjinga kwamba situmii akili yangu bali hisia! kama hutumii akili to me it amounts to ujinga so it doesnt matter whats da substitute of akili, coz i dont c it!lama hutumii akili yako weye ndo "mjinga!"
 
Mimi nazunguka sana vijijini watu wana hata habari ya CCJ wapo busy kujisajili kwenye matawi ya ccm kwa ajili ya kupiga kura za maoni kwa wana ccm!

!
Nakubaliana na wewe katika hili, lakini kwa nini miaka 18 baada ya mfumo wa vyama vingi kuanzishwa bado watu wako busy kujisajili na CCM na sio vyama vingine vya upinzani?kwanini wananchi bado wanaendelea kuamini kuwa uchaguzi mgumu zaidi ni ule wa kura za maoni ndani ya CCM na sio uchaguzi mkuu?na je tukate tamaa kwa sababu hiyo?...la hasha.

Tusiwasingizie wananchi katika hili, wananchi wapo tayari na wana hamu ya mabadiliko lakini vyama vya upinzani havijafanya vya kutosha kuweza kuchukua matarajio ya wananchi hawa na kuwajengea imani kuwa nchi itakuwa bora zaidi na salama mikononi mwao.
 
Ninafurahi kwamba mgawanyo tunaoutaka ndio unaendelea kuwepo. Wale wanaoamini Chadema, CUF au vyama vya upinzani vilivyopo ndiyo vinawakilisha matamanio yao na njozi zao wana haki kabisa ya kuendelea kuwemo humo na kuviimarisha; wale wanaoamini kuwa CCM ndiyo suluhisho la matatizo ya Watanzania na kuwa ndio chama pekee chenye uwezo wa kutuletea maendeleo nao wana haki ya kuendelea kuunga mkono na kujiunga nacho. LAKINI si haki kujaribu kuwataka watu wote wajiunge na upinzani wa zamani au chama tawala ati kwa sababu chama kipya hakieleweki, hakijulikani n.k n.k Hakuna ratiba ya kuundwa chama ili kikubalike; hakuna masharti ya chama kiwe kimeundwa kwa muda gani ili kiwe kinavutia watu; chama ni itikadi na muundo. Hadi hivi sasa hakuna chama kwenye upinzani huu zamani chenye itikadi ya CCJ, period. Sasa kutaka watu wa CCJ au mashabiki wake kujiunga na vyama vya upinzani wa zamani ili mradi tu wasiwe na chama chao ni kujaribu kuweka mawazo huru ya watu kwenye chupa moja ya upinzani.

Naomba nipendekeze; wale mnaoamini Chadema, CUF au vyama vya upinzani vya zamani kuwa ndio uchaguzi wenu endeleeni tu kwani ni sehemu ya demokrasia. Kama watu hamkubaliani kiitikadi, mtazamo au mapendekezo yenu ya kitaifa hamuwezi kuungana. Sielewi kwanini CCJ wanatakiwa kujiunga na vyama vingine wakati hawakubaliani navyo kiitikadi, mtazamo au malengo! Hatuwezi kujiunga na vyama vingine ili "kuiondoa CCM madarakani"; Muungano wa namna hiyo ni muungano dhaifu kwani unaundwa katika lengo la udhaifu. Huweji kuwa na lengo la kuondoa CCM madarakani kama msingi wa muungano!

Wale walioridhika na CCM waendelee hivyo hivyo na wale ambao tunataka kuleta pendekezo jipya kwa wapiga kura na WAtanzania, pendekezo lenye misingi ya historia yetu kama taifa basi tutafanya hivyo. Yawezekana tusifanye vizuri kama tunavyotaka kwenye uchaguzi huu lakini tunachotaka ni kuwa na sisi wenye mawazo tofauti na yale ya CCM au upinzani uliopo sasa tuwe na nafasi katika siasa za nchi yetu? Je hili linawatisha sana hadi mtushauri tujiunga na watu ambao hatukubaliani nao kiitikadi, mfumo, mtazamo au usuluhishi wa matatizo ya kitaifa? Tuungane nao ili nani afurahi?
 
Back
Top Bottom