Cars From Japan & Analysis of Free Car Giveaway!!!

myplusbee

JF-Expert Member
Jul 8, 2016
3,612
6,153
Wadau, hivi sasa kuna shindano linaendelea kwa jina la Free Car Giveaway. Hili ni shindano ambalo Mshindi mmoja atazawadiwa gari moja na washindi wengine 105 watazawadiwa kuponi. Baada ya kuona shindano hilo nikalazimika kulifanyia utafiti ili nijiridhishe nalo kabla sijaleta habari zake hapa.

Pamoja na yote hayo, hapa naomba niseme jambo moja. Sitaki kusema shindano hili ni halali/legit kwa 100% lakini nilichofanya kabla ya kuleta mada hii ni kuichambua kampuni inayoendesha shindano husika. Assumption ni kwamba, ikiwa shindano husika linaendeshwa na kampuni halali basi HUENDA na shindano lenyewe likawa halali. Nilichofanya mimi ni kutumia taarifa zilizotolewa na kampuni husika kisha nikazichunguza kwa kupitia external sources.
Ikiwa utahitaji kulisoma kwa makini shindano lenyewe na ikiwa unataka kujaribu, basi linapatikana hapa Free Car Giveaway:

UTAFITI WANGU & SUPPORTING EVIDENCE

1. Physical Address: Kwanza nilichukua physical address iliyowekwa na hiyo kampuni. Adress yao ni hii hapa chini:
Fact I.png


Nikataka kufahamu ikiwa kweli hiyo address ipo na hiyo kampuni inapatiakana kwenye hilo jengo. Nilipo-Google, nikajiridhisha kwamba ni kweli hiyo kampuni ipo na inapatikana kwenye hiyo physical address. Hata ukiangalia namba ya simu waliyotoa kwenye screenshot ya kwanza hapo juu, ndiyo hiyo hiyo waliyoweka hapo kwenye picha ya gari (screenshot ya 2).
Fact II.png


Fact IIB.png



EVIDENCE 2: Japan Used Motor Vehicle Exporters Association (JUMVEA):

Sawa na title inavyosomeka hapo juu, JUMVEA ni Muungano wa Wauzaji Magari Nje ya Nchi huko Japan. Ukitaka kuufahamu UHALALI wa JUMVEA unatakiwa kusoma angalizo la Ubalozi wa Kenya nchini Japan. Angalizo hili walilitoa kutokana na kuongezeka kwa idadi ya matapeli wanaojifanya kama exporters wa Japanese Cars. Screenshot na link ya habari husika ni hii hapa.
Fact III.png

Fact IIIB.png

Kwahiyo hapo utaona Ubalozi wa Kenya unawaasa Wakenya kabla hawajaagiza magari kutoka Japan basi wahakikishe dealer husika ana uhalali wa kufanya kibiashara na amesajiriwa na JUMVEA. Bila shaka ushauri huu ni muhimu hata kwetu sisi Watanzania.

Kutokana na hilo, nikataka kujiridhisha ikiwa kampuni inayooendesha hili shindano imesajiriwa na JUMVEA. Unaweza kuthibitisha wewe mwenyewe lakini taarifa zao ndani ya JUMVEA zinawakilishwa na hii screenshot hapa chini:

Fact IV.png

Ikiwa hadi hapo umeridhika na ungetamani kujaribu bahati yako, hilo linafayika kwa kutumia hii link: Free Car Giveaway

Kama vipi, tuendelee na uchambuzi wetu. Ukiangalia kwenye hiyo screenshot, unakuta hao Car From Japan ni Safe Trade Member. Kwa mujibu wa JUMVEA, Safe Trade Member ni yule ambae anakuhakikishia usalama wa pesa yako wewe mnunuaji hata kama pesa umeshamtumia lakini gari haijasafirishwa. Bila shaka, kampuni inayoingia kwenye hili group ni lazima ithibitishwe ina uwezo wa kufanya biashara bila magumashi.

Fact IVB.png

Kwa mara nyingine, hata kama huna haja ya kujaribu hili shindano kumbe tayari na wewe utakuwa umefaidika na taarifa hiyo hapo juu siku utakapotaka utakapotaka kuagiza gari kutoka Japan. Ili kujihakikishia usalama wa pesa yako, hakikisha dealer husika ni member wa Jumvea Safe Trade. Kwa maelezo zaidi, hawa ndio JUMVEA

Kwa hofu ya kuifanya thread kuwa ndefu sana, naomba niishie hapa lakini sina shaka wengi wetu tutakuwa tumejiridhisha kwamba shindano husika linaendeshwa na kampuni halali inayofanya biashara kihalali na inatambuliwa na mamlaka husika. Kwahiyo, ikiwa unataka kujaribu bahati yako, unaweza kufanya hivyo kupitia link: Free Car Giveaway.
 
  • Thanks
Reactions: MTK
Back
Top Bottom