Mbu
JF-Expert Member
- Jan 11, 2007
- 12,753
- 7,844
Hebu niambieni akina mama/dada wenzangu.Pengine nina rafiki nataka kupeleka mahusiano katika hatua nyingine labda ndoa tuseme.Na huyu mlengwa pengine ana tabia fulani au tuseme mazingira fulani ambayo nisingependa awe nayo katika hiyo level nyingine.
Kwa mfano ni mwizi/jambazi,mlevi,Fukara(hana hela wala kazi-naweza kusema ni mvivu) na mambo kama hayo.
Na pengine nishamwambia kuwa sipendi 1,2,3......ya hizo tabia na akaahidi kuwa atabadilika.
Vilevile katika interraction mbali x2 na marafiki hasa wanaume mara nyingi nimekuwa nikiwasikia wakisema kuwa MWANAMKE anauwezo mkubwa wa kumbadilisha na kumtengeneza mwanaume katika mahusiano the way anataka awe.
Sasa swali langu ni kuwa Is this true?
Wakina kaka pia mnaweza kuniambia eti mnaweza kubadilishwa na wanawake mkawa waume wema wenye kuonyesha mfano mwema?
Chrispin naomba usiingie kwenye hii thread inakuhusu
...huwezi kumbadilisha, ni yeye pekee mwenye uwezo wa kubadilika (akitaka.) Unachoweza kumsaidia ni 'kugundua' chanzo cha tabia zake mbaya. Jadiliana nae na tena akubali udhaifu wake, kisha mwenyewe ('labda' kwa msaada wako) aanze mkakati wa kubadilika kuelekea kiwango ambacho nyote mtaafikiana nacho.
Be patient ('Ukitaka.') Relationship's about compromising, tunatofautiana tabia, uwezo na maamuzi.