Elections 2010 Campaign za CCM na usafiri wa maroli

comp

Member
Aug 18, 2010
24
0
Waungwana niko Mtwara leo, na kama nusu saa iliopita nikiwa kituoni nasubiri dala dala niendelee na mizunguko yangu, yamepita maroli yanawarudisha wana CCM majumbani mwao, kutoka kwenye campaign.

Katika kampaign hizo ambazo sikupata bahati ya kuhudhuria ninaambiwa kulikuwa na kikundi cha ze comedy katika kuongeza idadi ya wahudhuriaji.

Point kubwa iliyonifanya nilaunch hii thread ni usalama wa hawa watu wanaojazwa kwenye haya maroli.

Usalama wao unaangaliwa kwa umakini kweli hasa ukizingatia yale magari hayajawa designed kubeba watu? Pia nataka mnisadie kujua kama sheria inaruhusu kujaza watu vile kwenye maroli?

Naombeni wana JF tuliangalie hili limekaaje hasa ukizingatia kipindi hichi tumekuwa tukiripotiwa habari nyingi sana zinazohusu ajali za barabarani hapa TZ.
 
Kisheria hairuhusiwi kubeba watu kwenye lorry nyuma(ambayo ni sehemu ya mizigo) wala kwenye pickup kwa nyuma.Lakini kama ujuavyo,CCM iko juu ya sheria za nchi hii.Na ikitokea ajli wakafa,itakuwa kazi ya Mola manake ndo anayeendesha malori.
 
Kibunango, tunajua familia yenu iko ccm tokea enzi, kuna mambo ambayo hutakiwi kutetea, kupanda roli unaona ni sawa? Endelea kutetea ufisadi mzee, hatukuzuii. Ila siku moja watu wataingia msituni japo si leo.
 
Mie nataka wasafiri kwa
Image011.jpg
 
Kisheria hairuhusiwi kubeba watu kwenye lorry nyuma(ambayo ni sehemu ya mizigo) wala kwenye pickup kwa nyuma.Lakini kama ujuavyo,CCM iko juu ya sheria za nchi hii.Na ikitokea ajli wakafa,itakuwa kazi ya Mola manake ndo anayeendesha malori.

Duuuuh! hii kali
 
Ulitaka wasafari kwenye mikokoteni?

..kibunango thats too much ...huoni kuwa kunakuchwa......CCM itaendelea kuvutia wasikilizaji kwa usafiri,vitenge,fulana,na visenti hadi lini...tujiulize tunalipeleka taifa wapi kwa kuuwa uzalendo??

uzalendo uliokuwapo CCM ambapo watu walienda kwenye mikutano hadhara kwa usafiri wao...,walitembea maili kadhaa ....watu walifanya kazi za kujitolea wakachimba barabara,wakajenga viwanja vya michezo kote nchini kama sheik amri abeid,kirumba,jamhuri,samora,vita,..uliishia kwa kujenga uwanja wa ALI HASSAN MWINYI TABORA...ambavyo leo hii hadi serikali itenge budget...hiyo ndio CCM wengi tuliokuwa nayo ...tukiimba halaiki na kucheza magwaride ....bila kuppewa chochote....siku hizi hata mahalaiki watoto hawaendi mazoezini hadi walipwe effu 2,000 kwa siku.....huku hazina ikiambiwa wanalipwa elfu 5,000 kwa siku.....tunaelekewa wapi???

je uzalendo huo sasa umehamia kwa wapinzani ambapo waananchi huenda mikutanoni kwa kujitegemea ........na hata ukiwaona wamechangamka toka moyoni....na si uchangamfu wa kununua.....,na mikutano ya wapinzani unakuta wananchi hadi wanachangia pesa .........

CCM inakoelekea ni kujichimbia kaburi ...maana inajiweka mbali na wananchi .....kwa kuendekeza hali hii ya posho na usafiri!!...sijui mwaka 2015 itakuwaje.....nadhani gharama za uchaguzi zitaifanya CCM iendelee kutumia gharama kubwa sana......na kujikuta kila baada ya uchaguzi inakabiliwa na kesi mfano wa EPA....mwisho wa siku wafanyabiashara wanaochangia nao watachoka ...watafanya kama kule KENYA ambapo baada ya kuchoka na michango ya KANU wafanyabiashara waliamua kuchangangia KIBAKI.....Maana ipo siku wafanyabiashara wetu watagundua pesa wanazotoa CCM ni bora wangelipa kodi halali.........ikifika hapo basi!.....wakichoka na tabia ya ccm na viongozi wao kuwageuza wafanyabiashara ATMs...
 
Kibunango, tunajua familia yenu iko ccm tokea enzi, kuna mambo ambayo hutakiwi kutetea, kupanda roli unaona ni sawa? Endelea kutetea ufisadi mzee, hatukuzuii. Ila siku moja watu wataingia msituni japo si leo.
Malkia Marie Antoinette wa Ufaransa alishawahi kuwa na majibu kama hayo. Kuna wakati wa miaka kama sikosei ya 1700, wafaransa walipatwa na njaa. Wakamfuata mfalme wao kumuomba mikate. Huyo malkia aliposikia wananchi wanaomba mikate, akashangaa na kusema, 'Kama hawana mikate, kwa nini wasile keki?' Wananchi hawakusahau majibu yake, na mara baada ya mapinduzi, yeye pamoja na mfalme walikatwa vichwa hadharani. Ole wenu nyie mnaowabeza wananchi...hukumu yao kali!
 
unajua hapo kama wangekuwa ni chadema wanafanya hivyo lazima wangekamatwa na traffic kwa kukiuka sheria na taratibu za usalama barabarani, sasa hatuombei ila incase ajali ikatokea, je nani wa kulaumiwa? wananchi wenyeqwe au hao waliowashawishi kwenda kwenye kampeni kwa kurundikwa kwenye malori ya mizigo? ni hayo tu wajameni
 
Ukifuata haki utaambiwa wewe ni mpinzani, ukivunja sheria wewe ni mwenzetu; na bado mtawachagua wavunja sheria na kudai haki :confused2:! Haiingii akilini hii kitu. Watanzania msiwe na akili mgando. Kwani CCM ni watu gani na Wapinzani ni watu gani, Msicheze mziki kwa kuwa watu wanacheza, sikiliza mdundo na kuelewa mandhari. Tanzania bila CCM inawezekana!
 
Ivi mumesahau wafuasi wa CUF walipanda lorry na wakakamatwa na traffic na huo usafiri ukapigwa marufuku.
CCM wako above the law bwana.
CCM wanaforce king
 
uzalendo uliokuwapo CCM ambapo watu walienda kwenye mikutano hadhara kwa usafiri wao...,walitembea maili kadhaa ....watu walifanya kazi za kujitolea wakachimba barabara,wakajenga viwanja vya michezo kote nchini kama sheik amri abeid,kirumba,jamhuri,samora,vita,..uliishia kwa kujenga uwanja wa ALI HASSAN MWINYI TABORA...ambavyo leo hii hadi serikali itenge budget...hiyo ndio CCM wengi tuliokuwa nayo ...tukiimba halaiki na kucheza magwaride ....bila kuppewa chochote....siku hizi hata mahalaiki watoto hawaendi mazoezini hadi walipwe effu 2,000 kwa siku.....huku hazina ikiambiwa wanalipwa elfu 5,000 kwa siku.....tunaelekewa wapi???
Mkuu naona unazungumzia zaidi CCM kabla ya vyama vingi, ambapo wananchi hawakuwa na chaguo la chama zaidi ya CCM. Sasa ni wakati mwingine na sidhani hayo ya kale kama yataweza kurudi chini ya CCM au Chama kingine chochote katika mfumo kama huu.
 
Malkia Marie Antoinette wa Ufaransa alishawahi kuwa na majibu kama hayo. Kuna wakati wa miaka kama sikosei ya 1700, wafaransa walipatwa na njaa. Wakamfuata mfalme wao kumuomba mikate. Huyo malkia aliposikia wananchi wanaomba mikate, akashangaa na kusema, 'Kama hawana mikate, kwa nini wasile keki?' Wananchi hawakusahau majibu yake, na mara baada ya mapinduzi, yeye pamoja na mfalme walikatwa vichwa hadharani. Ole wenu nyie mnaowabeza wananchi...hukumu yao kali!

Usitikishe kiberiti kilichojaa
 
waungwana niko Mtwara leo, na kama nusu saa iliopita nikiwa kituoni nasubiri dala dala niendelee na mizunguko yangu, yamepita maroli yanawarudisha wana CCM majumbani mwao, kutoka kwenye campaign.Katika kampaign hizo ambazo sikupata bahati ya kuhudhuria ninaambiwa kulikuwa na kikundi cha ze comedy katika kuongeza idadi ya wahudhuriaji. Point kubwa iliyonifanya nilaunch hii thread ni usalama wa hawa watu wanaojazwa kwenye haya maroli.Usalama wao unaangaliwa kwa umakini kweli hasa ukizingatia yale magari hayajawa designed kubeba watu? Pia nataka mnisadie kujua kama sheria inaruhusu kujaza watu vile kwenye maroli? Naombeni wana JF tuliangalie hili limekaaje hasa ukizingatia kipindi hichi tumekuwa tukiripotiwa habari nyingi sana zinazohusu ajali za
barabarani hapa TZ.
hakuna sheria yoyote ya usalama barabarani inayoruhusu kupakia abiria kwenye maroli isipokuwa kwa kibari maalum lkn najua ccm hutumia ubabe kuwasafirisha subiri mabaya yakitokea (ingawa siombei iwe hivo mungu epushia mbali)
 
Back
Top Bottom