Cameron: Kikwete kakubali maharamia wa kisomali kushtakiwa TZ!

Hiyo ni kutoka kwa mkutano wa London. Sasa tukae mkao wa kuliwa na ma Al shabab.
Hivi Ben yupo wapi kumfundisha huyu jamaa kusema "NO"?

Tanzania tuna matatizo mengi mengi mno, the last thing we need ni huu mzigo wa al-shabab. Kwa nini wasishtakiwe Ethiopia? au Hata Kenya wanakodai kuna UN-presence kubwa?
 
chanzo cha taarifa yako hakieleweki tutajuaje kama ni porojo. Ni wapi umepata taarifa hizi?
 
Tunaanza na yule Al-Shaabab Mkuu wa kule Tabora na kumdaka huyu kinara wao kabla hajatorokea kusikojulikana na vijisenti vyeti kupitia Malaysia.

And that is a VERY SERIOUS NOTE anyway!!!
 
Hiyo ni kutoka kwa mkutano wa London. Sasa tukae mkao wa kuliwa na ma Al shabab.
Hivi Ben yupo wapi kumfundisha huyu jamaa kusema "NO"?


Taarifa hii haijakamilika japo great thinkers watairukia na kuanza kutoa maoni bila kujali ina mapungufu. Haiko kamili kaitoa wapi?
 
kujiweka pembeni dhidi ya vita na alshabab haituondolei kupata athari zitokanazo na alshabab.
 
Usalama wetu uko mashakani hatuwezi kujitoa kwamba tukijitenga ndipo tutakuwa salama. Meli yetu ilishawahi kutekwa na watanzania kadhaa. El shabab wamechangia sana kupandisha bei ya mafuta kutokana na meli nyingi kukataa kufika pwani ya Afrika mashariki na Meli zinazokubali kupita bima imepanda bei endapo zitapata msukosuko.

Sina hakika kama Jk kakubali lakini tuna nafasi ya kutafakari kwa kina. Jambo hili linahusu usalama sio siasa.
 
hahaha
ALQAEDA=CIA PROJECT TO QONQUER THE MIDDLE EAST AND ARAB COUNTRIES
ALSHABAAB-CIA PROJECT TO QONQUER THE HORN AND EAST AFRICA
BOKO HARAM=CIA PROJECT TO QONQUER WEST AFRICA
COLUMBIAN REBELS AND MEXICO DRUG CARTELS= CIA PROJECT TO KEEP SOUTH AMERICA IN CHECK.

WE ARE SLOWLY INVITING THE AMERICANS, THE ENGLISH INTO OUR OWN SOVEREIGN DECISION BODIES, SLOWLY THEY WILL ACCESS OUR JUDICIARY, OUR MILITARY THROUGH SO CALLED MILITARY TRAINING.

JK BETTER WATCH ON THIS!!!!
 
Tukumbuke pia kwamba bila wao kama tutapata msukosuko wa el shabab watatutenga hapa ni muhimu kuchanganya karata. Wenzetu Uganda na Kenya wameshapata mashambulio ya el shabab hatujui zamu yetu ni lini.

Tafakari usalama wetu.
 
kujiweka pembeni dhidi ya vita na alshabab haituondolei kupata athari zitokanazo na alshabab.

Je, kujiingiza kwenye mgogoro wa Al-shaabab kutafunya tuwe salama? Wameruka nchi ngapi hawa wazungu mpaka waamue Tanzania? Na kwa nini Tanzania? Kama vyombo vyetu vya usalama hususan Jeshi la polisi linashindwa hata kuhimili maandamano watawaje kutuliza munkari wa al-shaabab? I just hope kama taifa hatutajuta kutokana na hii hatua!
 
Kukataa kuwashitaki el shabab Tanzania hakuna tofauti ya mbali na kukubali kuwashitaki Tanzania ....yote mawili hayatuhakikishii usalama wa nchi yetu.

Usalama wetu utakwenda sambamba na makubaliano mwengine yaliyofikiwa kwenye mkutano huo jinsi ya kuhakikisha nchi yetu haitapata athari na uamuzi huo lakini pia jinsi nchi tajiri zitakavyosaidia kulinda na kusaidia raslimali watu, mbinu na vifaa kama vitahitajika
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Back
Top Bottom