CAG Utouh ameficha ufisadi wa Ofisi wa Rais Ikulu na Ofisi ya Waziri Mkuu

TUMBIRI

JF-Expert Member
May 7, 2011
1,933
1,199
Wakuu heshima mbele,

Nimekuwa nikiisoma Ripoti ya Serikali ya Mdhibiti na Mkaguzi wa hesabu za Serikali ya mwaka wa fedha uliopita (2010/2011) yenye kurusa 216 na nimekuwa pia nikiilinganisha na Taarifa zake za miaka ya fedha iliyopita hususani ya 2008/2009 na 2009/2010.

Katika ripoti ya 2008/2009 Jumla ya Wizara, idara na wakala wa serikali zipatazo 8 zilipata hati safi zisizokuwa na masuala ya msisitizo (Unqualified Audit Opinion without Emphasis of matters). Katika ripoti ya mwaka uliofuata yaani 2009/2010, jumla ya Wizara, idara na wakala wa serikali 21 zilipata hati safi zisizokuwa na masuala ya msisitizo (Unqualified Audit Opinion without Emphasis of matters). Na katika ripoti ya mwaka jana wa fedha yaani 2010/2011, jumla ya Wizara, idara na wakala wa serikali zipatazo 11 zimepata hati safi zisizokuwa na masuala ya msisitizo (Unqualifed Audit Opinion without Emphasis of matters).

Katika ripoti zote hizo tatu zinazofuatana ni taasisi mbili tu yaana Ofisi ya Rais Ikulu na Ofisi ya Waziri Mkuu ndizo zimejitokeza kupata hati safi katika miaka yote hiyo. Kuna baadhi zimepata hati safi kwa miaka miwili ya fedha lakini zikashindwa katika mwaka mwingine. Katika hali ya kawaida imekuwaje Ofisi hizi mbili zimekuwa zikipata hati safi mfululizo kwa kuzingatia kwamba masuala ya msisitizo ambayo yamekuwa yakisisitizwa katika Wizara, idara na Wakala nyingi ni yale yanayohusiana na hali ya kibajeti na Uchumi wa nchi.

Mfano hoja ambayo imeonekana kusisitizwa karibu kila taasisi iliyokaguliwa ni hoja ya Outstanding liabilities (Madeni) na Payment charged to wrong expenditure code ambazo zote kimsingi zinatoka na taasisi huzikuwa zinapewa fedha za kutosha. Sasa mimi najiuliza iweje Wizara nyingi ziwe na Outstanding liabilities alafu Ofisi ya Rais Ikulu na Ofisi ya Waziri Mkuu zisiwe nazo?

Ina maana zenyewe zilipewa migao yao ya fedha kutoka hazina kulingana na bajeti au? Na kama ndivyo iweje zenyewe zipate migawo yote kulingana na bajeti huku Taasisi zingine zikipata migawo ya asilimia 40% hadi 50% ya bajeti nzima?
Ina maana hadi kufikia siku ya mwisho ya mwaka wa fedha yaani saa tano na dakika 59 usiku wa tarehe 30/06/2011 hata ile kampuni ya kufanya usafi Ikulu ilikuwa imelipwa deni lake la kufanya usafi wakati tunajua Taratibu za manunuzi ya serikali zinasema huduma kwanza malipo yanafuata?

Twende kwenye hili swala la Payment charged to wrong expendire code. Kwa ofisi ya Rais Ikulu ni vigumu hii hoja isiwepo maana tumekuwa tukisikia wakisafiri mara kwa mara tena kwa misururu ya watu wengi. Ina maana wenyewe kila walipokuwa wakitaka kusafiri vifungu vya Per diem na Air tickets vilikuwa na pesa muda wote?

Utouh, kwa kweli katika hili umetudanganya. Tunaamini Ofisi ya Rais Ikulu na Ofisi ya Waziri Mkuu nako kuna madudu. Kosa hili ulilofanya tunalimjulisha na lile la Jairo. ''You can fool some people but you can't fool all people all the time''.

Kwa wale wanaopenda source hii hapa:
MDAs WITH UNQUALIFIED OPINION WITHOUT EMPHASIS OF MATTERS (WIZARA, IDARA NA WAKALA ZENYE HATI ZINAZORIDHISHA NA ZISIZOKUWA NA MASUALA YA MSISITIZO)
No
2008/2009
2009/2010
2010/2011
1
Commercial Court
Judiciary
Accountant General's Department
2
Drugs Control Commission
Community Dev, Gender and Children
Commission for Mediation and Arbitration (CMA)
3
Ethics Secretariat
High Court Commercial Court
Directorate of Public Prosecutions
4
Labour Court
High Court Land Court Division
Judicial Service Commission
5
President's Office – Cabinet Secretariat
Labour Court
Ministry of Communication, Science and Technology
6
President's Office – State House
Ministry of East African Cooperation
Ministry of East African Cooperation
7
Prime Minister's Office
Ministry of Livestock Development
Ministry of Finance
8
Vice President's Office
President's Office – State House
President's Office and Cabinet Secretariat
9
Prime Minister's Office
President's Office, State House
10
RAS Mara
Prime Minister's Office
11
RAS Shinyanga
Treasury
12
RAS Tanga
13
Tanzania Embassy Berlin
14
Tanzania Embassy Brasilia
15
Tanzania Embassy Bujumbura
16
Tanzania Embassy Geneva
17
Tanzania Embassy Maputo
18
Tanzania Embassy Newyork
19
Tanzania Embassy Ottawa
20
Tanzania Embassy Pretoria
21
Vice President's Office

 
Serikali yote imeoza na wote wameiba pesa nyingi sana ..hii serikkali imevunja rekodi na kikwete anajua anajua sana kuwa watu wake ni wezi na wanaiba na msije kushangaa hii pesa inaibwa kwa kujiandaa na uchaguzi wa mwaka 2015 msishangae kabisa rais mzima anawatetea mawaziri wezi ..rais ndio source ya matatizo yote kwa sababu hajachaguliwa na wananchi wake na yeye analijuia hilo
 
Nashangaa ni kwa nini watu hawataki kuyaona haya!!!!
Hakika ukitaka kumuua nyoka hautakiwi uponde kiwiliwili au mkia. UNAPONDA KICHWA
 
Hawakawii kukwambia mahesabu fulani ya Ikulu hayakaguliwi kwa sababu za "usalama wa taifa".
 
Hawakawii kukwambia mahesabu fulani ya Ikulu hayakaguliwi kwa sababu za "usalama wa taifa".

Hivi ndo maana hata ile ya kagoda ili2mika kwenye usalama wa serikali? Sio usalama wa taifa maana ingekua hivyo huku mburahati ni muda sasa camp za wahuni zinawindana na mapanga nje nje na wahanga ni raia maana wakija inaambatana na uporaji wa barabarani na maduka na kujerui watu ila hamna chochote kilichafanyika na sie 2mejizoelea na kuona ni sehemu ya maisha ye2 maana wenye usalama wao wapo Obey.
 
Nchi hii upigaji watu wanajifunza kutoka wapi kama sio hizo ofisi kubwa mbili. Usanii mtupu
 
Back
Top Bottom