CAG: Ukaguzi wa EPA ulininyima usingizi

Josh Michael

JF-Expert Member
Jun 12, 2009
2,523
77
MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh amesema hakuwahi kupata usingizi baada ya kukabidhiwa jukumu la ukaguzi wa wizi wa fedha kutoka kwenye Akaunti ya Malipo ya Madeni ya nje (EPA), katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Jumla ya Sh133 bilioni zilibainika kuchotwa na baadhi ya makampuni nchini kutoka katika mfuko huo.

Utouh alisema pamoja na wakati mgumu waliopata katika suala hilo, ofisi yake ilikamilisha uchunguzi huo na kutoa ripoti ambayo haikuwa na dosari ya aina yoyote.

Utouh aliyasema hayo juzi katika kipindi cha ‘Tuambie’ kinachorushwa na kituo cha Televesheni cha Taifa (TBC 1).

“Kwa kweli nilipokabadhiwa jukumu la kuchunguza suala nzito la wizi wa fedha za EPA, katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT), sikupata usingizi.

“Lakini nashukuru pamoja na hali yote hiyo hadi sasa hakuna malalamiko wala dosari yoyote iliyojitokeza katika ripoti yetu ya ukaguzi.” alisema Utouh

Pamoja na mambo mengine, Utouh alisema kazi yao ni hatari na kwamba pia inajenga uadui na watu.

“Kazi yetu ni ya hatari na inaleta uadui na watu,’’ alisema Utouh.

Tayari watu wanaotuhumiwa kuchota fedha za EPA wamepelekwa mahakamani.

Ufisadi katika EPA, kwa mara ya kwanza ulibainika baada ya ukaguzi wa

Kampuni ya Deloite & Touche ya Afrika Kusini, iliyofanya uchunguzi katika akaunti ya EPA, ilibaini ufisadi Sh 40 bilioni, ambao ulidaiwa kufanywa na kampuni ya Kagoda.

Hata hivyo, BoT ilisitisha mkataba na kampuni hiyo. 

Baada ya mkataba huo kusitishwa, serikali iliipa kazi hiyo Kampuni ya Kimataifa ya Ernst and Young, ambayo katika uchunguzi wake, ilibaini upotevu wa Sh 133 bilioni katika akaunti ya EPA.


Ripoti ya uchunguzi ya Kampuni ya Kimataifa ya Ernst and Young ilibaini kuwa wizi huo ulichangiwa na kukosekana kwa udhibiti wa programu ya kumbukumbu za madeni hayo.
Ripoti hiyo, ilieleza kuwa kumbukumbu za madeni ya EPA ziliwekwa kwenye programu ya kumbukumbu ya kompyuta ya Akwera, (Akwera Database) nje ya Mfumo Mkuu wa Udhibiti wa Hesabu za BoT (CBS) ambako ni rahisi mtu kuchezea mahesabu.
 
kumbe kuna uwezekano ziliibwa fedha nyingi sana zaidi ya hizo bilions 133?
kampuni ya kwanza kuchunguza ilipigwa chini, ikaja ya pili ndipo CAG nae akaingia, manake hapo pesa zilizoibwa ni maradufu ya hizo tunlizoambiwa...
 
Back
Top Bottom