Cag: Serikali inachangia wanafunzi kufeli mitihani

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,314
33,108

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh.
Matokeo duni ya shule za Sekondari yanasababishwa na Serikali kutoshughulikia matatizo yanayochangia wanafunzi kufeli.
Hayo yalielezwa mjini hapa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh, alipokuwa akitoa taarifa ya ukaguzi uliyofanywa na ofisi yake kubaini chanzo cha kushuka kwa ufaulu nchini...
CAG pia alifanya ukaguzi wa thamani ya fedha za umma katika vituo vya afya, mazingira na malipo ya wastaafu wa Serikali.

Kuhusu ufaulu duni, alisema pamoja na kwamba Serikali imekuwa ikifanya utafiti wa suala hilo, imekuwa haiyafanyii kazi matokeo ya uchunguzi hasa kuziba mianya ya tatizo zima.

Kutokana na hali hiyo, CAG ameitaka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, kushughulikia matatizo yanayosababisha kushuka kwa elimu hasa ufaulu hafifu katika masomo ya Sayansi na Hisabati.

Utouh alisema katika sekta ya afya, imebainika kuwa mgawanyo wa rasilimali kama dawa, vifaa tiba na watumishi katika vituo vya afya hauzingatii hali halisi.

Utouh alitoa mfano kuwa kituo cha afya kinachopokea wagonjwa 380 kwa siku kimekuwa kikipata Sh. 1,755,000 za kununulia dawa kwa miezi mitatu wakati kituo kingine kinachopokea wagonjwa 18 kwa siku kinapatiwa Sh. 2,000,000 kwa kipindi hicho. Aidha, eneo lingine lililofanyiwa utafiti ni uchafu wa mazingira katika miji mikubwa na manispaa ambapo ilibainika kuwa uwezo wa ukusanyaji wa taka katika kila Halmashauri ni asilimia 28.

Alisema hali hiyo imelifanya tatizo hilo kuwa kubwa siku hadi siku na kutahadharisha kuwa iwapo hatua madhubuti hazitachukuliwa, madhara makubwa yanaweza kutokea.

Kuhusu mafao ya wastaafu wa Serikali Kuu na Serikali za Mitaa, Utouh alisema kumekuwepo na ukiritimba wa kulipa wastaafu kutokana na utamaduni uliojengeka wa kutotunza kumbukumbu.

Alisema uchunguzi uliofanywa kwenye Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF) na mfuko wa watumishi wa Serikali za Mitaa (LAPF), umebaini kuwa jambo linalochelewesha malipo kwa wastaafu ni utunzaji duni wa kumbukumbu za wanachama.

CHANZO: NIPASHE
 
Back
Top Bottom