Elections 2010 CAG ajipanga kuvibana vyama vya siasa

Mkodoleaji

JF-Expert Member
Apr 27, 2008
458
138
Sadick Mtulya
MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Ludovick Utouh amesema ofisi yake imejipanga kukagua mapato na matumizi ya fedha zilizotolewa kwa vyama vya siasa na wagombea kwa ajili ya uchaguzi mkuu.

Kwa mujibu wa Sheria ya Gharama za Uchaguzi, ofisi ya CAG ina mamlaka ya kukagua mahesabu ya mapato na matumizi ya vyama vya siasa vinavyoshiriki uchaguzi pamoja na wagombea na kutoa taarifa ya ukaguzi huo.

Akizungumza na waandishi baada ya kufungua warsha ya siku nne ya mafunzo ya uwajibikaji, utawala bora na ukaguzi wa thamani ya fedha, Utouh alisema ofisi yake imeshajipanga kutekeleza jukumu hilo la kukagua matumizi ya fedha za uchaguzi.
“Ofisi yangu imekwishajipanga vizuri kupitia mapato na matumizi ya fedha yaliyofanywa na vyama vya siasa pamoja na wagombea wao katika mchakato mzima wa uchaguzi,’’ alisema Utouh.

Sheria hiyo mpya iliyosainiwa mapema Februari mwaka huu inavitaka vyama kuwasilisha taarifa za mapato na matumizi ya fedha kwa ajili ya uchaguzi ndani ya siku 90 baada ya kumalizika kwa uchaguzi mkuu, huku wagombea wakitakiwa kufanya hivyo miezi miwili baada ya uchaguzi na matokeo kutangazwa.
Utouh alibainisha kuwa atafanya uhakiki huo baada ya kupata nyaraka za mapato na matumizi ya vyama na wagombea kutoka kwa Msajili wa vyama vya Siasa.

“Kwa mujibu wa Sheria ya Gharama za Uchaguzi, Msajili wa Vyama ndiye anayepaswa kunipa nyaraka zote za mapato na matumizi ya fedha yaliyofanywa na vyama pamoja na wagombea. Baada ya miezi mitatu natarajia kuwa nimemaliza kazi ya ukaguzi huo na ripoti kuwa tayari kuwekwa hadharani,’’ alisema Utouh.
Sheria pia inatoa ruhusa kwa Msajili kukifikisha mahakamani chama au mgombea ambaye atashindwa kuwasilisha taarifa za mapato na matumizi kwa mujibuwa sheria.

“Ofisi yangu imewahi kukagua mahesabu ya CCM ya mwaka 2007/08, lakini nimesahau kama ilipata hati safi au chafu. Sijawahi kukagua mahesabu ya chama kingine cha siasa,’’ alisema.
Awali akifungua warsha hiyo inayoendeshwa na wakufunzi kutoka Taasisi ya CCAF ya nchini Canada, Utouh alisema imeandaliwa ili kuwafunza watendaji wa taasisi za serikali kukabiliana vizuri na utunzaji wa kumbukumbu za matumizi ya fedha.

“Wataalamu hawa watatoa mafunzo kuhusu dhana ya uwajibikaji, utawala bora na ukaguzi wa thamani ya fedha ikiwa ni pamoja na utunzaji mzuri wa kumbukumbu za mapato na matumizi ya fedha,’’ alisema
Alisema katika mafunzo hayo, maafisa wa serikali watafundishwa jinsi ya kukabiliana na hali ya misukosuko ya uchumi nchini na ulimwenguni kwa ujumla.
Utouh alisema hali ya ukaguzi wa mahesabu nchini ikiwamo utunzaji wa kumbukumbu inakwenda vizuri.

My take:
Hivi huyu jamaa wenzangu mnamuelewa kweli?
 
Aongelee Audit report after uchaguzi si muda wake sasa vinginevyo tutamuelewa tofauti.Hata kama alikagua ya CCM na bado hajui kama CCM walipata hati chafu/safi anaongelea nini hakuna tija
 
"Ofisi yangu imewahi kukagua mahesabu ya CCM ya mwaka 2007/08, lakini nimesahau kama ilipata hati safi au chafu. Sijawahi kukagua mahesabu ya chama kingine cha siasa,'' alisema.


Huyu ni mnafiki mkubwa.Mosi,anajifanya hakumbuki kama CCM ilipata hati chafu au safi,mbona anakumbuka kama mahesabu yake yalishakaguliwa?pili anataka kuionyesha jamii kuwa CCM,ndiyo chama ambacho kinaweza kufuata na kutii taratibu zilizowekwa kisheria!
 
Mkataba wake unakwisha mwaka huu, anajipendekeza aongezewe renewal.Ni bahati mbaya kuwa hawezi kusoma alama za nyakati kuwa utawala wa JK mwisho 31/10.
 
Back
Top Bottom